Kaboom
JF-Expert Member
- Nov 6, 2011
- 10,828
- 14,996
Habari zenu Wapendwa
Kuna huyu bosi wangu amekuwa akinisumbua kwa muda sasa..Baada ya mbinu zake za kunitaka kimapenzi kugonga mwamba akaamua kuniletea visa na fitna ofisini..Ni fitna zake ndo zilizopelekea hata nikapewa uhamisho wa kikazi..
Kabla ya kuondoka nikaona si vyema nikamuacha hivi hivi..Nikaenda Bagamoyo kwa nia,dhumuni na lengo la kumtengeneza..Nikakutana na Mtaalam zen nikampatia Jina la huyo kiumbe..Baada ya mtaalam kufanya mambo yake akaniambia huyo mtu hamuoni kwenye system zake..Akajaribu kufanya kila linalowezekana lakini ikashindikana..
Kuna jamaa yangu ni mfanyabiashara..Anapiga trip za Dar-Congo mara kwa mara..Akaniambia Congo kuna jamaa yuko vizuri sana labda tukajaribu huko..
Ikawa siku jamaa ana safari ya huko,ikabidi niongozane nae..Tulipofika bila hata ya kupoteza muda tukanyoosha moja kwa moja hadi kwa Mtaalam
Baada ya kumpatia Mtaalam jina na kufanya mambo yake akaniambia mbona nampatia jina la mtu aliyekufa..Nikamkatalia na kumwambia mtu huyo yuko hai..Jamaa ikabidi arudie tena na tena..Lakini kila akifanya manuva,system inamletea makaburi tu..Akaniambia huyo mtu hayupo duniani na amefariki muda mrefu sana..
Hayo majibu yakanichanganya sana..Ila nilivyojaribu kuoanisha majibu ya mtaalam wa kwanza na wa pili nikaona kama yanalingana hivi..Hapo ndipo nilipopata shauku ya kufwatilia undani wa huyu Boss wangu..Ndo kuja kugundua kuwa anatumia vyeti vya mtu aliyefariki na hata kupata kazi hapo ofisini hakutumia utaratibu rasmi..
Sasa wakuu mi ni muumini wa Jino kwa Jino..Huyu Kiumbe siwezi kumuacha hivi hivi..Nifwate utaratibu gani ili apate adhabu stahiki???