DOKEZO Kero RITA Kilombero na Ucheleweshaji Vyeti na Rushwa

DOKEZO Kero RITA Kilombero na Ucheleweshaji Vyeti na Rushwa

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
RITA Kilombero (Ifakara) wanachelewesha sana kutoa vyeti, halmashauri nyingine vyeti vinatoka haraka ndani ya siku 1-4 lakini kilombero inaweza kuchukua hadi mwezi.

Kuna mazingira ya rushwa pale rita kilombero, niliwahi kutuma maombi kupitia erita, ili nikachukulie cheti pale rita kilombero, cheti kilikaa wiki 3 bila kutoka, ikabidi nifunge safari kutoka mlimba hadi ifakara ni zaidi ya kilometa 100, wakati nipo kwenye foleni kwaajili ya kwenda kutoa malalamiko yangu ya kucheleweshewa cheti kuna mtu akaniambia hapa ili upate cheti mapema ni lazima uwashikishe mkononi elu 10 ili wakupe kipaumbele, aliendelea kuniambia kwamba yeye alituma maombi siku ya kwanza akawashikisha maofisa wa rita kilombero tsh. 10,000 then siku ya pili ameambiwa akachukue cheti chake.

Maofisa wa rita kilombero wana stationery zao mtaani na wengine wameingia makubaliano na baadhi ya stationery ambazo ukituma maombi ya cheti kupitia stationery hizo unapata cheti kwa haraka zaidi ya wale wanaotuma maombi kupitia simu zao AU kupitia stationery nyingine.

Changamoto ni kwamba kilombero ni kubwa sana inahudumia hadi halmashauri ya mlimba, imagine mtu atoke tanganyika masagati hadi ifakara umbali wa zaidi ya kilomita 150 ili akafanye maombi ya cheti kupitia stationery zao wakati alitakiwa tu atumie simu yake akiwa huko huko nyumbani kwake akatuma maombi then baada ya siku mbili AU tatu cheti kikawa tayari kimetoka anapakua form yake ya nida mtandaoni akajaza na kuisainisha kwa mtendaji akaenda nayo ifakara, kule anachukua cheti chake cha kuzaliwa then anapanga folen ya nida, yaani anakuwa amefanya mambo mawili kwa wakati mmoja.

RITA Kilombero ni kero sana kwa wananchi, wanatanguliza rushwa mbele, hafanyii kazi maombi ya vyeti kwa wakati.


Gemini_Generated_Image_2zeg3q2zeg3q2zeg.png
 
Tena yule mama mtu mzima anamajibu mabaya sana. Mimi nafutilia cheti cha kifo hapo wananizingua tuu. Yule maza anajibu km hataki.
 
Back
Top Bottom