Kwa mtazamo wangu ACT Wazalendo wangeleta faida UKAWA kwa hoja zifuatazo
1. Umoja ni nguvu
Kama wapinzani wote wangekuwa wamoja pamoja na hawa ACT WAZALENDO umoja huo ungesaidia katika kuuza sera na ilani ya mgombea wa UKAWA kwa kiasi kikubwa hivyo kupunguza mgawanyiko wa kura.
2. Umahiri wa kuongea
Watanzania wengi wanataka mtu anaeongea kwa ufasaha na umahili mkubwa katika kuuza sera ili kuwavuta na hatimaye kushawishika. Ukweli miongoni mwa wanasiasa wanaoweza kuongea kwa ufasaha na kueleweka mmojawapo ni ZZK. Hivyo basi muungano huo ungekuwa na tija. Najua wengi mtakuja na kusema mbona wapo akina Mnyika nk lakini still na hawa jamaa kutokana na 'shughuli pevu ya watu 32 ya CCM' ilibidi wakomae sana majimboni mwao kujinusuru hatimaye UKAWA wakawa wanawategemea watu waliotupiwa virago CCM. Kama kungekuwa na watu wa aina ya ZZK, CCM ingekuwa na kazi ya ziada
3. Kuwekeza kwa ACT WAZALENDO
Hiki chama bado kichanga hivyo kwa mtazamo wangu hawa wanaangalia mbele hawakuwa na matarajio makubwa sana ya kushinda viti vingi ila kukijenga chama kuanzia ngazi ya chini vilevile kukitambulisha nchi nzima. CCM inatusumbua kwa sababu ina mizizi, imejijenga kuanzia chini na hili naona UKAWA bado hajalitambua ndo maana wanasumbua coz wanajua wao kuanzia vijijini wameshika. Sasa hawa ACT WAZALENDO ndo maana wamehakikisha wanasimamisha wagombea wao ngazi zote na kwa idadi kubwa
Kwa kifupi mimi naona ni kama chama kitakachokuja kuisumbua sana CCM baadae
Nawasilisha✌