President of China
JF-Expert Member
- Dec 6, 2018
- 31,772
- 89,799
Gamboshi is real.
Ndungu zangu wanajamvi, wiki iliyopita nilikuwa katika safari zangu za kila siku za tafiti. Moja ya tafiti ambazo nimejikita nazo ni tafiti za kitamaduni na mali kale.
Kwanza nianze kwa kusema hivi uchawi upo, kila nchi inautumia kwa namna yake.
Nilitembelea katika kijiji kimoja huko mkoani shinyanga nikakutana na mzee anayejulikana kwa jina la Madeleke. Lengo langu ni kutaka kujua na kujifunza namna ya jamii za kale walivyoishi.
Tuliongea mambo mengi na alinifundisha vitu kadha wa kadha ikiwamo namna ya kufanya uchawi. Nikamwambi mzee nasikia habari za kuhusu gamboshi hivi kweli suala lipo.
Mzee aliniambia suala hilo lipo na yeye ni mmoja wa members wa gamboshi. Akaniahidi atanipeleka.
Tulifanya maandalizi kwa muda wa siku 6 kisha tukafunga safari kuelekea mkoani Simiyu.
Kusema kweli safari yetu ilikuwa ya ajabu sana, maana tulisafiri usiku wa manane. Usafiri uliotumika ni wa wanyama mithili ya fisi ila wao wapo juu kidogo.
Mida ya kama saa 8 za usiku niliona taa zikiwaka mbele yetu. Ni taa za kila namna.
Ndugu yangu, tuliingia kwenye lango lililo chini ya mlima na kukutana na watu wa kila aina. Walikuwepo wazungu, warabu, wachina na sisi waafrika.
Mzee kaniambia hapa ndio gamboshi.
Kulikuwa na chakula, vinywaji. Watu walikuwa wakisherehekea.
Wanawake wazuri wazuri walikuwepo. Na kuna wengine wasanii na wanasiasa wakubwa niliwaona. Niliwaona wachungaji kadhaa wanaohubiri wakijumuika.
Kweli uchawi upo na Gamboshi ipo.
Ninatarajia kwenda huko tena mwezi wa tano. Mzee ameniahidi ataenda kunitambulisha na mimi niwe member.
Ninayo mengi sana niliyojifunza. Watu wa gamboshi ni wakarimu na wanaupendo.
Kama kuna mtu yupo tayari aweze kuni PM tupange safari twende pamoja.
Asanteni.