Nimefanikiwa kuingia Gamboshi - True Story

Nimefanikiwa kuingia Gamboshi - True Story

mkuu acha chai bana wewe.....gamboshi ni kijiji kipo katikati ya mkoa wa shinganya na simiyu, ukipita njia ya shinyaga kuja bariadi utakutana na hicho kijiji, ni kijiji kama kijiji vingine acha kutupikia chai sahizi na jua kali lote hili.
Amini usiamini, ukienda kawaida tu huwezi kuona chochote. Lakini mimi kwa macho yangu haya mawili nimeshuhudia kabisa. Kama unabisha tufanye utaratibu tuende na wewe ukajionee.
 
Kila mwanasiasa mmoja uliemkuta huko ukimtaja hapa nakuwekea dau nono tu
 
Jamaa mmoja kwenye miaka ya 2005 alikuwa anasimula Pale RFA kwenye kipindi cha sitosahau siku ya kwanza anapelekwa gamboshi anadai alikutana na treni ya Umeme, viwanja vya ndege vya kisasa,

Nikajisemea kimoyo kumbe tupo vizuri, kuna haja ya kuwashirikisha hawa jamaa wa gamboshi kuelekea Tanzania ya viwanda
Huyo alikua anauza kitabu[emoji23][emoji23][emoji23]
Si nikanunua,Chumvi nyingi kweli kweli

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kila mwanasiasa mmoja uliemkuta huko ukimtaja hapa nakuwekea dau nono tu
Ninaweza kuwataja hapa. Ila unajuwa hiyo ni privacy ya mtu. Na kwa kuongezea matajiri wengu tu niliwaona na wengine wamo humu JF. Wengine watajaribu kupindisha mada yangu. Na wakiendelea kupindisha nitawataja.
 
Ninaweza kuwataja hapa. Ila unajuwa hiyo ni privacy ya mtu. Na kwa kuongezea matajiri wengu tu niliwaona na wengine wamo humu JF. Wengine watajaribu kupindisha mada yangu. Na wakiendelea kupindisha nitawataja.
Bila kuwataja, for me you are talking rubbish
 
Kuna kijiji kimoja kinatoa sana ndizi, misukule ndio inapakia, laiv bila chenga, nilienda huko na fuso, tulipofanikiwa kufikisha mzigo gairo na gari lao nikawaachia na kazi basi, sikukikariri jina kile kijiji ndio ilikuwa mara yangu ya kwenda na ya mwisho
 
SIMIYU INAPAKANA NA MKOA WA GEITA WENYE ILE WLAYA YA JAMAA AU?
Hapana, mkoa wa Simiyu unapakana na mkoa wa Mwanza, Shinyanga, Mara na Manyara kama sikosei. Na huo mkoa wa Geita, unapakana na Mwanza, Shinyanga na Kagera. Hivyo Simiyu na Geita, ziko mbali sana
 
Hapana, mkoa wa Simiyu unapakana na mkoa wa Mwanza, Shinyanga, Mara na Manyara kama sikosei. Na huo mkoa wa Geita, unapakana na Mwanza, Shinyanga na Kagera. Hivyo Simiyu na Geita, ziko mbali sana
ASANTE MKUU ILA SHINYANGA MNATISHA, SUMBAWANGA NA TANGA WANASUBIRI!!????
 
Gamboshi is real.
Ndungu zangu wanajamvi, wiki iliyopita nilikuwa katika safari zangu za kila siku za tafiti. Moja ya tafiti ambazo nimejikita nazo ni tafiti za kitamaduni na mali kale.
Kwanza nianze kwa kusema hivi uchawi upo, kila nchi inautumia kwa namna yake.
Nilitembelea katika kijiji kimoja huko mkoani shinyanga nikakutana na mzee anayejulikana kwa jina la Madeleke. Lengo langu ni kutaka kujua na kujifunza namna ya jamii za kale walivyoishi.

Tuliongea mambo mengi na alinifundisha vitu kadha wa kadha ikiwamo namna ya kufanya uchawi. Nikamwambi mzee nasikia habari za kuhusu gamboshi hivi kweli suala lipo.
Mzee aliniambia suala hilo lipo na yeye ni mmoja wa members wa gamboshi. Akaniahidi atanipeleka.
Tulifanya maandalizi kwa muda wa siku 6 kisha tukafunga safari kuelekea mkoani Simiyu.
Kusema kweli safari yetu ilikuwa ya ajabu sana, maana tulisafiri usiku wa manane. Usafiri uliotumika ni wa wanyama mithili ya fisi ila wao wapo juu kidogo.
Mida ya kama saa 8 za usiku niliona taa zikiwaka mbele yetu. Ni taa za kila namna.
Ndugu yangu, tuliingia kwenye lango lililo chini ya mlima na kukutana na watu wa kila aina. Walikuwepo wazungu, warabu, wachina na sisi waafrika.
Mzee kaniambia hapa ndio gamboshi.
Kulikuwa na chakula, vinywaji. Watu walikuwa wakisherehekea.
Wanawake wazuri wazuri walikuwepo. Na kuna wengine wasanii na wanasiasa wakubwa niliwaona. Niliwaona wachungaji kadhaa wanaohubiri wakijumuika.

Kweli uchawi upo na Gamboshi ipo.
Ninatarajia kwenda huko tena mwezi wa tano. Mzee ameniahidi ataenda kunitambulisha na mimi niwe member.
Ninayo mengi sana niliyojifunza. Watu wa gamboshi ni wakarimu na wanaupendo.
Kama kuna mtu yupo tayari aweze kuni PM tupange safari twende pamoja.

Asanteni.
PUNGUZA BHANGI MBICHI, NA MATATIZO YA NJAA NI KUWAZA UASI ILI UPATE SHIBE KWA NAMNA YOYOTE NA MATATIZO YA SHIBE NI KUFANYA UASI ILI UPUNGUZE SHIBE, ACHANA NA MAJANI MABICHI.
 
Back
Top Bottom