Natumai muwazima wa afya ,niko kwenye mahusiano na kaka mmoja ambaye alionyesha kunipenda na kunijali ,nilimwamini sana ila cha kushangaza kunasiku ametoka kwangu tukaagana vyema kua anaenda nyumbani .Baada ya muda nampigia cm nijue kama amefika salama ,haipokelewi nikajisemea atakua yuko bafuni .Mara muda cm yangu inaita kupokea cm imejipiga yuko na mwanamke wanasifiana vibaya mno kwa mambo waliyokwisha kuyafanya .wanaagiza vinywaji nikasikiliza baadae nikaona upuuzi nikakata cm ,nikapiga hajapokea ndani ya dakika tatu akapiga .Anadai nilikua bafuni nikamwambia sawa bafu lako wanapiga mziki na wanauza savana na henken ,nikakata cm nikashangaaa mtu anagonga nikamfungulia kuingia anasema lov umesikia vibaya nikamwambia sawa .leo kakosea msg ya tigopesa katuma kwangu tsh 20 na txt usinipigie nipo semina ntakucheki na tuko wote mi nikamjibu sawa .Anaanza sor nilikua namtumia mshikaji ananisumbua nikamuuliza na hii elfu ishirini ya nn ananiuliza ipi.oooh nimekutumia ya vocha daaah nimechoka namwacha leoleo niendelee tu kuwa single .