Nimechoka

Nimechoka

Habari zenu: Tangu niolewe huu ni mwaka wa tatu lakini kuna kitu kinanitatiza huyu mwanaume mara nyingi huwa anapigiwa simu na namba mpya tofauti tofauti nikijaribu kuzipiga wanapokea wadada ukimuuliza anakwambia alikosea namba je hiyo namba yake huwa inakosewa na wadada tuu? Kingine wadada wa ofisini kwao kila siku usiku wanamtakia usiku mwema mara awaalike kwenye mitoko huwa tunaenda nae lakini nahisi huwa wananisanifu kwa nini awe na urafiki na wadada tuu?

akili kumkichwa hapo mamie, unaeza kutwa unaibiwa kiaina siunajua mjini tena hapa
 
U Better be harted by truth rather than being conforted by lies..akili kichwan mwako..pole mwaya
 
Kuwa mvumilivu utamnasa iposiku ukimwakia saahizi utakuwa huna nguvu ya uhakika kukuchenga ni rahisi sana
 
Acha kumtisha mwenzio kwani akienda huko umesikia anaiacha hukohuko mchana ya wenzio jioni yako...aaalaaaah
 
...its wrong numbers na marafika wa kazini full stop..! Unless uje na some evidance kuliko kuja na hisia bila ushahidi...
 
Sema na Moyo wako, Je Unampenda Mumeo na Kumheshimu????????

Anamatatizo Mengine zaidi ya hilo la simu na urafiki na wadada????????

Vinakuthiri wewe kwa kiasi gani?????

Vinaukweli kwa kiasi gani???????

Kisha chukua Hatua
 
Hayatuhusu. Haya ni mambo yenu binafsi wewe na huyo mumeo. JF sio mahala pa kuleta mambo yenu!! Peleka kwa wakwe. Ukiona anaendelea, mtose, tafuta bwana mwingine!!

Wewe kila siku mtu akipost jukwaa hili HAYATUHUSU!! WEWE ni MSEMAJI WETU? Domo kama c.h.o.o! Kama hutaki tambaa!! Acha watu wenye issues zao washare na wanajamvi!
 
Habari zenu: Tangu niolewe huu ni mwaka wa tatu lakini kuna kitu kinanitatiza huyu mwanaume mara nyingi huwa anapigiwa simu na namba mpya tofauti tofauti nikijaribu kuzipiga wanapokea wadada ukimuuliza anakwambia alikosea namba je hiyo namba yake huwa inakosewa na wadada tuu? Kingine wadada wa ofisini kwao kila siku usiku wanamtakia usiku mwema mara awaalike kwenye mitoko huwa tunaenda nae lakini nahisi huwa wananisanifu kwa nini awe na urafiki na wadada tuu?

Pole sana. Mimi nimeoa na labda niseme mke wangu anaweza kuwa na experience kama yako.

Simu yangu niliyokuwa naitumia ujanani ndio nimeifanya ya nyumbani. Hii simu wrong numbers zishapigwa sana na wadada, tukipiga back mtu anasema wrong number. Mke wangu haimtatizi.

Ofisini kusema ukweli ni sehemu ya pili ya maisha. Message za usiku si nzuri sana especially kutoka kwa kina dada. Sasa nalichofanya mimi na mke wangu ni kuhakikisha madada wa ofisini ambao tunashare kazi wanakuwa marafiki wa wife. Sio urafiki wa karibu saaana ila wanaweza kuchat na hata message ikitumwa haina tatizo.

Weekends tukitoka mara nyingine hao madada wa ofisini wanapendekeza twende wapi, namchukua wife tunaenda na huko ni full furaha.

Mimi nadhani kuna kiji element cha kutokumwamini mume wako kinakunyemelea. Kipotezee. Jiweke urafiki na hao wadada wa ofisini kwake, ukitoka kuwa positive. MTU anayefanya UZINZI ataumbuka tu siku moja.
 
...its wrong numbers na marafika wa kazini full stop..! Unless uje na some evidance kuliko kuja na hisia bila ushahidi...

nilishawahi kukuta meseji za mdada zinazohusu mapenzi mara arudi saa 6 za usiku
 
Wewe kila siku mtu akipost jukwaa hili HAYATUHUSU!! WEWE ni MSEMAJI WETU? Domo kama c.h.o.o! Kama hutaki tambaa!! Acha watu wenye issues zao washare na wanajamvi!

si ndo hapo afadhali umenisaidia kumwambia mijitu mingine bwana
 
mi sikumfosi nikimwambia naenda nyumbani ananiahidi kunifanyia mambo mabaya kuna siku tuligombana nikaondoka ile nafika tu stendi nikakamatwa na police wakanipeleka kituoni nilikaa kama masaa mawili hivi akaniijia sasa mi simuelewi ameshanifanyia vituko vingi vinatia hasira sasa hii ni ndoa au nikutekwa?

Afu jamaa ni mtekaji pia,hahahaha,ndoa hizi
Ingekua ni busara zaidi kama ungelifikisha ili jambo kwa wazazi wake
 
Mh jamani jamani....pole ndo niwezayo kukupa! Ila mueleze tu ukweli..communicate with your husband.
 
Back
Top Bottom