Sikia nikwambie kitu kizuri rafiki.....! Maisha tunayoishi wanadamu sisi wenyewe ndio tunaamua yaweje, either yawe yenye furaha,upendo,amani, afya na raha mustarehe. Au yawe yenye huzuni,kutojiamini,mfadhaiko,upweke na maumivu.
Sasa wewe kwa kutokujua umejikuta umechagua upande wa mabaya, yawezekana unalipa mabaya uliyoyafanya nyuma sasa law of karma inakuadhibu.
Lakini habari njema ni kwamba unaweza kuirudisha furaha, amani, upendo, kujiamini kuliko potea. Unafanyaje sasa? Twende taratibu hahahaha....
Ni hivi ubongo wa binadamu umegawanyika katika sehemu kuu 2....! Conscious mind na subconscious mind.
Sasa huyu bwana conscious mind yeye ni kama captain wa meli yeye ndio anaona kilicho mbele na ndio anampa taarifa na muongozo injinia aliyoko ndani, ambaye ni subconscious mind...! Sasa endapo captain atamwambia injinia kata kulia hata kama Kuna barafu yeye atafuata hivyo hivyo....! Kila unachokiona, kila unachofikiri, kila unachoamini, kila unachotamka kinachukulia na conscious mind kinapelekwa kwa subconscious mind, ambaye ndio analeta matokeo sasa
Subconscious mind yako ina uwezo mkubwa sana, ina uwezo wa kukupatia chochote kile unachokita endapo utaiomba kwa unyenyekevu na kuiamini...! Kinachokuponza wewe umekua mtu wa kujiwazia mabaya tu, hivyo unachowaza ndio hicho subconscious inakuletea.....!
Sasa kuanzia leo anza kufanya yafuatayo na utakua mtu kama wengine utakua ni mwenye furaha kuliko.....! Andika kwenye karatasi yafuatayo
1.subconsious mind yangu inajua kila kitu, ina uwezo usio na mwisho wala kifani imenifanya kuwa ni mwenye furaha,
2.mimi ni mwenye amani ya moyo.
3.mimi najiamini sana.
4.mimi ni mwenye upendo na ninapendwa na kila mtu.
5.mimi na furahia sana kuishi katika hii dunia iliyo nzuri na baraka tele. Tamka maneno hayo kila siku kabla ya kulala na baada tu ya kuamka asubuhi, kwa unyenyekevu na uiaminishe subconscious mind yako kuwa hayo uyasemayo ni kweli. Nakuhakikishia baada ya siku 21-40 ukitamka maneno hayo kwa utaratibu niliokwambia utakua mtu mwingine kabisa...!
Na kamwe usijiwazie mabaya hata kidogo maana yatakutokea kweli, always think positive....! Ni ujinga kuamini kitu kinachokudhuru.....
Amini amini amini nakwambia nawe utaponyeka.... hakuna aliyezaliwa aje kuteseka, wote tumezaliwa Kuja kufurahia maisha. Ila Kuna watu wanashindwa kufahamu uwezo mkubwa walionao ndani yao, mwisho wake wanaishia kupata shida na taabu kama mtoa thread. Subconscious mind yako ina majibu yoote yanayokusumbua ila tu wengi hawajui jinsi ya kutumia uwezo huo, wenzetu wazungu siri hizi walizijua mapema ndio maana shida shida hizi wao haziwapati.....!
Nikutakie kila la kheri