Nimechoka kukopwa hela na baba mkwe kila mara

Nimechoka kukopwa hela na baba mkwe kila mara

Mkuu katika kitu unachotakiwa kuwa nacho makini
ni kuweka mawasiliano ya karibu na mama mkwe au baba
mkwe , hawa wengi ni watupa mawe kinoma. Kama vipi siku
nyingine unajifanya mtandao unasumbua au simu yako imejiblock
hivyo huwezi tuma hela.

heeheheheheeee nimecheka sana....nao ni ushauri mzuri
 
Si atapiga kwa kutumia no. Ya binti yake, hebu nipe niongee na mumeo hapo

akipiga kwa namba ya binti yake ajifanye sauti imekauka anaumwa kikohozi kwaiyo hawezi kuongea,,hiyo ndo dawa maana hakuna namna
 
akipiga kwa namba ya binti yake ajifanye sauti imekauka anaumwa kikohozi kwaiyo hawezi kuongea,,hiyo ndo dawa maana hakuna namna

Hahaha jamaa atabaniwa papuchi na mkewe mpk atamtumia hela mkwe
 
Achana na mwanae tu sasa maana hakuna namna jombaa. Ulifuga mwenyewe maradhi.
 
Kwanza makosa uliyafanya mwanzo mkuu kwa kumzoesha kumkopesha. OK ushalipia mahari? Kaa na wife wako mweleze hali harisi na kiasi ambacho ushampatia baba mkwe, kama ni mwelewa na anakujari atakupatia jibu unalotegemea. Ukiona kaegemea kwa mzazi wake hapo hamna namna tena zaidi ya kuongeza mke wa pili maana muda wowote atakuacha na hautapata sapoti yoyote kwa mkwe.
 
hehehe "kwa hiyo nikusubirie lini"
mkuu jitose umwambie ukweli, msemo "truth shall set you free" hua uko sahihi 100%, mwambie mzee siwezi kukupa pesa period. Yeye hakujali sioni sababu ya wewe kuchukulia easy kiasi hicho ungekua mtu mwenye pesa ndefu hapo sawa, ila kama unalaumu kumpa milioni kwa mwaka moja inaonyesha kabisa haupo kwenye hali nzuri kiuchumi, mpe makavu tu, hawezi kukuchukia, akikuchukia basi yeye ni mtu mbaya na si wa kua karibu naye kabisa.

Ukimpa makavu hatorudia tena na utaishi kwa amani kabisa bila yeye kukupa mawazo. Muda mwingine hawa wazazi wanatakiwa wawekwe kwenye mstari wajue nafasi yao, wewe ukifulia hutoenda kwake kuomba msaada.
 
Nawasalimu,

Haiwezekani baba mkwe kusema nimkopeshe hela halafu harudishi, karibia mwaka mzima sasa, mimi sina pesa za kuchezea

Haiwezi kuvuka 2 month kabla ya kupiga simu na kudai nimpe laki moja au mbili atarudisha kwamba anategemea kupata siku fulani, cha ajabu nikimtumia kwa m-pesa anapiga kimya hadi shida nyingine anaibuka tena kuwa nimuazime hela bila kutaja deni la nyuma, sasa nimechoka.

Nimemwambia mwanae tumeishia kugombana eti nisimnyanyasie baba yake kwa vijisenti vichache wakati mdogo wangu anakuja kila mara nampa pesa, vijisenti vichache? Wakati inakaribia millioni moja tangu mwaka uanze?

Nifanyeje kuhusu huyu mzee? Maana nimechoka, inafikia hatua hata nikisema sina atadai "kwa hiyo nikusubirie lini!!

Nonsense
Huyo mke wako ni mwanachama wa CCM?? au anaundugu na yule mwanachama profesa au yule mwanasheria a.k.a nyoka anayerembua??
 
Kama mke wako anajua hilo jaribu kumwambia amwambie baba yake kuwa hali yako si nzuri kiuchumi ati, ILA ukiwa nazo usiache kumpa na ukimpa si lazima wife wako ajue.
 
Duuuhh, wakati mwingine onyesha wewe ni mtu wa aina gani. Ni vizuri watu wanaokuzunguka wakajua wewe ni mtu wa aina gani?
 
Nawasalimu,

Haiwezekani baba mkwe kusema nimkopeshe hela halafu harudishi, karibia mwaka mzima sasa, mimi sina pesa za kuchezea

Haiwezi kuvuka 2 month kabla ya kupiga simu na kudai nimpe laki moja au mbili atarudisha kwamba anategemea kupata siku fulani, cha ajabu nikimtumia kwa m-pesa anapiga kimya hadi shida nyingine anaibuka tena kuwa nimuazime hela bila kutaja deni la nyuma, sasa nimechoka.

Nimemwambia mwanae tumeishia kugombana eti nisimnyanyasie baba yake kwa vijisenti vichache wakati mdogo wangu anakuja kila mara nampa pesa, vijisenti vichache? Wakati inakaribia millioni moja tangu mwaka uanze?

Nifanyeje kuhusu huyu mzee? Maana nimechoka, inafikia hatua hata nikisema sina atadai "kwa hiyo nikusubirie lini!!

Nonsense

Kaka pole sana kwa kisanga hicho, ila tambua unapotoa pesa yeyote kwenda kwa mkwe usiwekee maanani kuwa ipo siku hizo pesa zitarudishwa kwani tambua hutoweza kudai hata kama utazihitaji, hivyo unavyo mpa hela mkwe wako uwe mambo mawili kurudishiwa au kutorudishiwa.
 
Ni ubaguzi huo, hivi angekuwa babako ungelalamika hivi?
 
Si nasikia huwa hamumalizi deni la mahali ili baba mkwe asione aibu kukueleza shida yake, kwa kuwa unadaiwa.
 
Duuuh!watu wengine matatizo mnajitakia wenyewe.
 
Eti "Kwa hiyo nikusubirie lini" mjibu baada ya miaka miwili mzee.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom