bobby dolat
Senior Member
- May 18, 2015
- 167
- 264
Nawasalimu,
Haiwezekani baba mkwe kusema nimkopeshe hela halafu harudishi, karibia mwaka mzima sasa, mimi sina pesa za kuchezea
Haiwezi kuvuka 2 month kabla ya kupiga simu na kudai nimpe laki moja au mbili atarudisha kwamba anategemea kupata siku fulani, cha ajabu nikimtumia kwa m-pesa anapiga kimya hadi shida nyingine anaibuka tena kuwa nimuazime hela bila kutaja deni la nyuma, sasa nimechoka.
Nimemwambia mwanae tumeishia kugombana eti nisimnyanyasie baba yake kwa vijisenti vichache wakati mdogo wangu anakuja kila mara nampa pesa, vijisenti vichache? Wakati inakaribia millioni moja tangu mwaka uanze?
Nifanyeje kuhusu huyu mzee? Maana nimechoka, inafikia hatua hata nikisema sina atadai "kwa hiyo nikusubirie lini!!
Nonsense