Nimechimba kisima kwa 5.8mil nasambaza maji mtaa mzima; Nashangaa miradi ya Serikali huwa inakwama wapi

wewe kweli pwagu!!! unaulizia unit kwenye Lita 20? anyway! Lita 1000 sawa na unit moja, kwahiyo ndoo itakuwa sawa 0.02unit
Safi sana mkuu komaa tu na akija boya yoyote mtoe nduki tu......kuna Mijitu humu inaleta siasa sjui upime Maji blahblah tu

Ova
 
habari wapendwa!!
Mimi kwa gharama ya 5.8 mil nilichimba kisima na nimepata maji mengi mno, kiasi kwamba nimeamua kusambaza mtaani kwangu! kwa bei ya 1500@unit.
Nashangaa sana miradi ya serikali inatumia mabilioni ya pesa lakini maji hayatoki kwa visingizio lukuki!
nimetafakali kwa kina hawa wataalam wetu wanakosea wapi sijapata majibu!
naombeni mwenye majibu anisaidie tafadhari!

updates:

Kuna watu wananitumia message Inbox kwamba nifute huu Uzi; Naomba kutoa jibu la pamoja hapa kwamba huu uzi sifuti, na lengo la uzii huu ni kujadili ili kupata suruhisho, kama Mimi nimetumia 5.8mil tu, na nimeweza kusaidia karibu mtaa mzima, Kwa nini serikali isichimbe visima vidogo vidogo vingi kama vya kwangu kila mtaa? kama Mimi nimetumia 5.8mil nimepata maji ya kutosha hao watndaji wasomi inakuwaje wanachimba visima kwa bei ya mabillioni na havina maji?
Wasomi mnatakiwa mbadilike, Sheria kandamizi ziondolewe, Huko vijijini watu wanakunywa maji ya visima na hayajapimwa,
Wanaoirudisha nyuma nchi ni wasomi wasiojali Maisha ya watanzania wanataka nini!
Maji ni huduma mhimu, Unaponikataza nisigawe maji unataka watu waoge na kunywa tope?
Huu Uzi sifuti, Na atakaye jitia kuja kwangu sijui figisufigisu nasema kabisa Ole wao! Wasinijaribu, Nitakachowafanya Hiiiiiiiiiiiiii. Yaani nimekaa na ukame miaka nenda miaka rudi Leo nimechimba kisima changu MTU aje anizingue!? Nimegawa maji mtaa mzima kwasababu nimechoka kuombwa ombwa!

View attachment 774933
mchanganuo!
1. Motor ya maji 2HP nilinunua kwa laki 7
2. sim tank mbili 1.2 mil
3. kuchimba kisima na pump 3.1mil
4. vifaa vingine na ufundi laki 8
We watafute na utawapata. .
 
Ngoja niiforward kwa commissioner gerneral wa tra a raise invoice akuletee. Unataka kushindana na dawasco?
 
Hawezi kujitapa hivi Na kufanya wahandisi wa maji ni kitu!

Hajuh Sheria za kusambaz maji safi!.
Kwanza sijuh kama ana kibali toka kwa bonde!..

Hatukatai kuchimba kisima!
Wachimbieni wekeni taratibu zenu.....
Mngechimba nyie mradi huo mngesema mmetumia bln1

Ova
 
Sijaona kibali hapo kutoka ofisi ya bonde mkuu na nina imani upo mjini ulipaswa kufanya hivyo kabla ya kuchimba kisima alafu unaiponda serikali angalia wasije wakakuundia zengwe kwa kukuambia umechimba maji bila kibali hivyo unaiba rasilimali za Taifa wakati huo huo unaletewa na wataalamu wa "water quality" kuona kama ulifanya "water quality assessment" wakati unachimba na baada ya kuweka pump (nchi ya visasi hii kwa sasa)
 
Lakini mkuu mi nakushauri ukae kimya tu. We fanya yako tena acha sifa usianze kuishangaa sirikali.
Kuna NEMC,TFDA. Maji unayo sambaza kwa raia wengine ni lazima ya pimwe. Na mamlaka ikija hapo na mashariti yao Wallah unaweza ukawasusia hicho kisima.
Stay cool Bra.
 
Back
Top Bottom