Wengi hudhania kuwa ndoa ni unganiko tu la wenzi wawili na kufanyika mwili mmoja, lakini husahau kuwa pia ni unganiko la familia mbili na ndio maana huambatana na chagizo la sherehe(harusi) na nderemo. Uliyekuwa unamuita
mama watu8 baada ya ndoa jinale hubadilika na kuwa
mama. vivyo hivyo kwa baba na ndugu wengine kila mmoja kwa nafasi yake.
Hivyo basi kama wewe ni mwanamke au mwanaume wa Kiafrika kuna mambo ya kuzingatia kabla ya kujihusisha na mahusiano yapelekeayo ndoa.
1. Kabila
2. Imani za dini
3. Tabia
4. Kipato
5. Mengineyo
Hiyo ni baadhi tu ya mitazamo tofauti ambayo ipo kwenye familia zetu za Kiafrika, ingawa si kila familia hutilia mkazo lakini zipo kaya ambazo hadi sasa zimekuwa waumini wa dhana hizo.
Mifano ipo mingi na mingine ipo wazi sana na tumekuwa tukiishuhudia kila iitwapo leo. Mathalani si haba kukutana na malalamiko ya mtu wa dini fulani kukutana na kikwazo cha kuoa au kuozwa kwa kuwa tu kuna utofauti wa imani.
Eleine kitu cha muhimu kwako kutambua sasa ni kuwa, heri umepata nafasi ya kuelezwa kwa uwazi kuwa mtu wa kabila lako hatakiwi katika familia ya mchumba wako, kuliko vimbwanga ambavyo ungekutana navyo pindi ungeolewa.
Binafsi ninaweza kusema huyo jamaa amekuwa mstaarabu kukueleza kwa kuwa anakujali, la sivyo angekuwa ni mtu mwingine angelazimisha lakini ndoa yako ingekuwa chungu kutokana na mashinikizo hasi ya mama mkwe.
Piga moyo konde mapenzi hayajaanza leo wala jana, yapo tokea kipindi cha Adam na Hawa.