Nimeathirika

Nilifikili ni mimi tu, kumbe tuko wengi, basi kifo cha wengi ni harusi, haina haja ya kuhofia huu ugonjwa.
 
JF ni ugonjwa, mimi mwenyewe kazi haziendi vizuri kisa kubrowse kwenye JF na network ikizingua huwa nahamia kwenye simu.,basi sikilizia credit inavyokata...
 
Kwa kweli ni hatari
Ila wengi watapona kama dawa zifuatazo zitatolewa; especially hii itawatibu zaidi wale guests

- No guest log in , ku log in JF 5000 Tshs per each 20 minutes you are logged in

Hela hizi zitasaidia kuboresha wodi hii ya JF
 
Ndugu wana Jamii forums,
natangaza rasmi mbele ya kadamnasi hili kuwa mimi ni muathirika.
Nikiamka asubuhi sifanyi kitu kingine zaidi ya kuingia Jamii,
Kazi haziendi bila ka window ka jamii kuwa minimized mara maximazed.
akili yangu inawaza Jamii Forums.
Kweli mimi ni muathirika na hii kitu imemeza kabisa ufahamu wangu.
Je kuathirika huku ni kwangu mie tu au na wenzangu wapo?
hii ina maana employer wako analose money kwa kukulipa mshahara wakati kazi haiendi...
 
Yaani!!! Hata mimi nimo. Mimi JF ndio inanihabarisha yaani nimeifanya ndio magazeti. Kila asubuhi naanza nayo. Kazi kweli!!!!!!!!!!!
 
Oooh Kazi yangu ni sawa na bi mkubwa bt JF mke mdogo tayari keshaiweka ndoa yangu na bi mkubwa rehani,lakina nashukuru kwa kua nikitaka stess najiu majukwaa ya kuzipatia na nikitaka tulizo la akili najua ni jukwaa gani niingie so sitaki dawa so far ni mgonjwa nayejitambua!
 
ndugu wana jamii forums,
natangaza rasmi mbele ya kadamnasi hili kuwa mimi ni muathirika.
Nikiamka asubuhi sifanyi kitu kingine zaidi ya kuingia jamii,
kazi haziendi bila ka window ka jamii kuwa minimized mara maximazed.
Akili yangu inawaza jamii forums.
Kweli mimi ni muathirika na hii kitu imemeza kabisa ufahamu wangu.
Je kuathirika huku ni kwangu mie tu au na wenzangu wapo?

asee hata mimi! Im in love with this hadi shem anadhani nafanya ndivyo sivyo
 
Nilidhani ni mimi tu kumbe tuko wengi!!! Mi na2mia cm ya mkononi mara nyingi nikiwa off unakuta niko bz sana na cm mpaka nahisi nataka kupofuka macho. Kuhusu gharama huwa c2mii gharama kubwa. Mi na2mia mtandao wa voda huwa nanunua kifurushi cha 50mb@Tsh 2,000 ambayo ina2mika@ muda wa cku 30.
 
Hapa mi nina mtafaruku na gf wangu...kanuna tangu jana,leo baada ya chai, yupo kimya!!duh na mm nipo tena JF
 
Pole, sana kwa hilo tatizo, waathirika wa mitandao mpo wengi tu, wengine facebook, wengine twiter, poleni sana ila jaribuni kupunguza muda wa kuwaza hii mitandao, na kujaribu kutafuta vitu vingine vya kufanya zaidi
 
kaka pole sana.unapoendelea kuishi kwa matumaini nakushauri uogeze CD4 zako kwa kutembelea mtandao wa Fikrapevu
 
waathirika tupo wengi; waombolezaji (waajiri) ni lukuki; waumiao (dependants) kibao na waangamiao ni taifa zima ambalo uzalishaji unapungua kisa ushiriki wa JF. ingawa hivyo kuna faida nyingi zinapatikana kwa kuathirika na JF kubwa ikiwa ni kujadiliana kwa mapana na marefu mustakabali ya nchi na hatma ya uongozi wake
 
Back
Top Bottom