Nimeanza kufuga kwa mara ya kwanza

araway

araway

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2007
Messages
519
Points
225
araway

araway

JF-Expert Member
Joined Sep 26, 2007
519 225
nimeanza kufuga kwa mara ya kwanza kuku wa kienyeji! kwa kuanza nimenunua kuku 9 kati ya hao jogoo ni moja ambaye namwona bado ndama . nina siku ya tatu tangia nianze na leo nimeamka nimeona kuku mmoja anapinda mgongo na anakuwa kazubaazubaa sasa sijui kama ndio kideri kimeanza! naomba mdaqu mwenye uzoefu na hawa wadudu anishauri ni dawa gani naweza kuwapa ili kunusuru hawa jamaa!101_0521.JPG
101_0520.JPG
 
Maundumula

Maundumula

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2010
Messages
7,048
Points
1,225
Maundumula

Maundumula

JF-Expert Member
Joined Nov 4, 2010
7,048 1,225
Pole kaka, siku ya tatu tu wanapinda mgongo?

Ngoja waje wataalam watakusaidia
 
Mandingo

Mandingo

JF-Expert Member
Joined
Sep 22, 2011
Messages
3,871
Points
2,000
Mandingo

Mandingo

JF-Expert Member
Joined Sep 22, 2011
3,871 2,000
Mkuu huja nitendea haki kwa hako kajogoo!umekapa madem wengi ila si saiz yake kabisa hebu tafuta mwanaume wa kweli!.....
.....Halafu ume wafuga kiswaz sana yaani msosi ume mwaga chini!maji kwenye vikopo duuh huyu eti ndio ata wafikia kina Interchick!!!
 
M

Malila

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2007
Messages
4,527
Points
2,000
M

Malila

JF-Expert Member
Joined Dec 22, 2007
4,527 2,000
Mkuu huja nitendea haki kwa hako kajogoo!umekapa madem wengi ila si saiz yake kabisa hebu tafuta mwanaume wa kweli!.....
.....Halafu ume wafuga kiswaz sana yaani msosi ume mwaga chini!maji kwenye vikopo duuh huyu eti ndio ata wafikia kina Interchick!!!

Kwanza nikupongeze kwa kuthubutu kuanza.

Pili sikubaliani na mtoa mchango hapo pekundu, ni lazima uwe na mahali pa kuanzia ktk safari yo yote, umeanza vizuri na umefanya vizuri zaidi kujitokeza ili kupata michango ya wenzako. usirudi nyuma hata kidogo, kesho utakuwa na ujasiri wa kuwafundisha wanao/wenzako namna ya kuanza cho chote hata kama una fedha kiduchu,cha msingi kwako ni kusimamia vision yako.
 
C

ChiefmTz

JF-Expert Member
Joined
Apr 15, 2008
Messages
2,722
Points
2,000
C

ChiefmTz

JF-Expert Member
Joined Apr 15, 2008
2,722 2,000
Uko mkoa gani? Mie nina majogoo ya ukweli
 
L

Luiz

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2011
Messages
342
Points
0
Age
29
L

Luiz

JF-Expert Member
Joined May 23, 2011
342 0
araway kama upo hapa nitafute kwenye namba hii 0764860293 ninakauzoefu kidogo na ufugaji wa kuku wa kienyeji kwa ugonjwa wa kideli kuna dawa inaitwa FLUBAN kuna kitu naona umekosea jitaidi nitafute nikuele vizur.
 
Last edited by a moderator:
CHASHA FARMING

CHASHA FARMING

Verified Member
Joined
Jun 4, 2011
Messages
6,431
Points
2,000
CHASHA FARMING

CHASHA FARMING

Verified Member
Joined Jun 4, 2011
6,431 2,000
nimeanza kufuga kwa mara ya kwanza kuku wa kienyeji! kwa kuanza nimenunua kuku 9 kati ya hao jogoo ni moja ambaye namwona bado ndama . nina siku ya tatu tangia nianze na leo nimeamka nimeona kuku mmoja anapinda mgongo na anakuwa kazubaazubaa sasa sijui kama ndio kideri kimeanza! naomba mdaqu mwenye uzoefu na hawa wadudu anishauri ni dawa gani naweza kuwapa ili kunusuru hawa jamaa!View attachment 72018
View attachment 72019
Mkuu Hongera Sana, Usiikatishwe Tamaa, Yule Mkenya Mwenye Kampuni ya Kuku Kubwa kuliko zote Kenya nzima alianza na kuku kama hawa,

Na siku Itakuwa hiviSo mkuu hakuna kukata tamaa,
 
bishoke

bishoke

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2010
Messages
276
Points
0
bishoke

bishoke

JF-Expert Member
Joined Jan 12, 2010
276 0
nimeanza kufuga kwa mara ya kwanza kuku wa kienyeji! kwa kuanza nimenunua kuku 9 kati ya hao jogoo ni moja ambaye namwona bado ndama . nina siku ya tatu tangia nianze na leo nimeamka nimeona kuku mmoja anapinda mgongo na anakuwa kazubaazubaa sasa sijui kama ndio kideri kimeanza! naomba mdaqu mwenye uzoefu na hawa wadudu anishauri ni dawa gani naweza kuwapa ili kunusuru hawa jamaa!View attachment 72018
View attachment 72019
Hongera sana kwa kuthubutu kuanzisha mradi wa kuku wa kienyeji. Idadi uliyoanza nayo nadhani ni nzuri ila unahitaji jogoo mwenye uwezo mzuri wa kupanda. Mimi siyo daktari wa mifugo lakini ni mfugaji wa kuku kideli ni rahisi sana kuki kinga kwa chanjo ya kideli and newcastle lakini wakisha anza kusinzia ni nadra kufanya lolote. Nimesoma kitabu fulani cha shirika linaitwa KIMKUMAKA wanashauri kutumia muarobaini kutibu kideli. Jaribu kutwanga muarobaini loweka kwenye maji na chija machicha kisha wapatie wanywe. Kwakuwa ni chungu, siku ya kuwapa muarobaini hakikisha siku hiyo unawapa chakula bila maji na wapatie maji ya muarobaini baada ya kuwa wamepata kiu sana.

Wape wote dawa hata wale ambao hawajaanza kusinzia. Ukijaribu chanjo ya kideli sasa hivi usije shangaa wakafa wote. wakisha pona wapatie chanjo ya kideli walao mara 3 au 4 kwa mwaka, utafurahia mifugo yako. Pia usisahau dawa ya monyoo. Hongera sana na kila la kheri.
 
platozoom

platozoom

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2012
Messages
8,136
Points
2,000
platozoom

platozoom

JF-Expert Member
Joined Jan 24, 2012
8,136 2,000

MAELEZO MAZURI: K wa kuongezea

Mkuu umewachanja chanjo ya kideri? unawapa chakula chenye mchanganyiko wa calcium kama dagaa? na kama hujawachanja usiwachanje kabisa ..............jaribu kuwapa antibiotic (zipo vets) ama wape mchanganyiko wa majani ya alovera kwenye maji na wanywe kwa siku saba ndipo uwape chanjo ya kideri.

Seriously ukizubaa kuku wote watakufa!! Kideri si mchezo...........na chanjo yenyewe kila baada ya miezi mitatu (wanapozaliwa, halafu mara mbili, baada ya hapo unauza (huwezi kukaa na kuku kwa zaidi ya miezi sita sio ng'ombe!!
Seriously jogoo ni muhimu sana awe na afya njema, mwenye umbo kubwa, na kidole cha nyuma kiwe kidogo........asiwe mgonjwa na mbegu ya mchanganyiko au chotara........Ukifanya hivyo atapiga kazi balaa .......hadi mitetea 10!!
 
L

Luiz

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2011
Messages
342
Points
0
Age
29
L

Luiz

JF-Expert Member
Joined May 23, 2011
342 0
mwanzo mgumu uckate tamaa ulichokosea kingine usimwage chakula chini ni rahisi sana kupata magonjwa tafuta vyombo vya kulia ni vya bati vinauzwa kwenye masoko ya kawaida hakikisha sehemu wanaporia ni pakavu .
 
Dafo

Dafo

Member
Joined
Aug 1, 2012
Messages
70
Points
95
Dafo

Dafo

Member
Joined Aug 1, 2012
70 95
hongera mkuu kwa kuanza kufuga,ni mwanzo mzuri mana umethubutu kufanya kwa vitendo.pindi uonapo kuku ameanza kuonyesha dalili kama hizo na nyingine ambazo sio za kawaida kama anayokua siku zote.ni vyema na inashauriwa haraka sana umtenge na kumuweka peke yake ili kama ni ugonjwa asiambukize wengine.pili jitahidi uende kwenye duka la dawa za mifugo au mtaalam na umuelezee dalili zote alizonazo kuku.
Tatu jitahidi kuboresha hayo mazingira angalau chakula uwawekee kwenye vyombo hii itasaidia kupunguza upotevu wa chakula usiokuwa wa lazima na pia utapunguza uwezekano wa kupata maambukizi hasa kwa kuku wanakaa eneo moja.kila la heri mkuu
 
araway

araway

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2007
Messages
519
Points
225
araway

araway

JF-Expert Member
Joined Sep 26, 2007
519 225
araway kama upo hapa nitafute kwenye namba hii 0764860293 ninakauzoefu kidogo na ufugaji wa kuku wa kienyeji kwa ugonjwa wa kideli kuna dawa inaitwa FLUBAN kuna kitu naona umekosea jitaidi nitafute nikuele vizur.

mkuu nashukuru sana kwa ushauri nilichelewa kuingia hapa naona muda umeenda natumaini kesho kukutafuta. kwa sasa nilienda kwa maduka ya mifugo wakanipa dawa inaitwa VETOXY-20 ninaichanganya na maji na kwasiku zote mbili sijawapa maji ya kawaida zaidi ya mchanganyiko wa hii dawa.
 
araway

araway

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2007
Messages
519
Points
225
araway

araway

JF-Expert Member
Joined Sep 26, 2007
519 225
Hongera sana kwa kuthubutu kuanzisha mradi wa kuku wa kienyeji. Idadi uliyoanza nayo nadhani ni nzuri ila unahitaji jogoo mwenye uwezo mzuri wa kupanda. Mimi siyo daktari wa mifugo lakini ni mfugaji wa kuku kideli ni rahisi sana kuki kinga kwa chanjo ya kideli and newcastle lakini wakisha anza kusinzia ni nadra kufanya lolote. Nimesoma kitabu fulani cha shirika linaitwa KIMKUMAKA wanashauri kutumia muarobaini kutibu kideli. Jaribu kutwanga muarobaini loweka kwenye maji na chija machicha kisha wapatie wanywe. Kwakuwa ni chungu, siku ya kuwapa muarobaini hakikisha siku hiyo unawapa chakula bila maji na wapatie maji ya muarobaini baada ya kuwa wamepata kiu sana.

Wape wote dawa hata wale ambao hawajaanza kusinzia. Ukijaribu chanjo ya kideli sasa hivi usije shangaa wakafa wote. wakisha pona wapatie chanjo ya kideli walao mara 3 au 4 kwa mwaka, utafurahia mifugo yako. Pia usisahau dawa ya monyoo. Hongera sana na kila la kheri.
nashukuru mkuu! nimewapa dawa inaitwa vetoxy-20 kwa siku mbili na naendelea kuwapa kwa wiki hii nzima nimeambiwa inatibu kideri na magonjwa mengine yanayo wasumbua kuku sasa nawasikilizia lakini kuna mmoja naona anasinzia sinzia
 
araway

araway

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2007
Messages
519
Points
225
araway

araway

JF-Expert Member
Joined Sep 26, 2007
519 225
mwanzo mgumu uckate tamaa ulichokosea kingine usimwage chakula chini ni rahisi sana kupata magonjwa tafuta vyombo vya kulia ni vya bati vinauzwa kwenye masoko ya kawaida hakikisha sehemu wanaporia ni pakavu .
ni kweli mkuu hapo ndio kwanza nilikuwa nimetoka kuwanunua na hata banda nilikuwa sijaandaa lakini nashukuru nimefanikiwa kupata banda leo na nategemea kununua vifaa vya kulia chakula, kuhusu jogoo bado natafuta mbegu nzuri zaidi na huku nilipo wanapatikana majogoo ya kuchi tatizo raia wagumu sana kuuza mbegu lakini bado nawasaka.
 
funzadume

funzadume

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2010
Messages
8,453
Points
2,000
funzadume

funzadume

JF-Expert Member
Joined Jan 28, 2010
8,453 2,000
safi sana kuku wanalipa kama ukiwafuga vizuri cha muhimu tafuta duka la madawa ya mifugo ambao wanatoa na ushauri na dawa pia usiwe bahili kuwalisha na kuwatibu
 
N

Nguto

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2011
Messages
2,798
Points
2,000
N

Nguto

JF-Expert Member
Joined Apr 11, 2011
2,798 2,000
Ukitaka kuku hao wakupe faida wafuge kisasa na uwape chanjo zote. Waenclose kwenye chumba usiwafuge kienyeji kama picha yako inavyoonyesha. Kwenye mtandao kuna taarifa nzuri tu. Andika "Indigenous chicken" halafu google na utajifunza mwenyewe jinsi ya kutnza kuku wa kienyeji. Mpeleke huyo uku kwa daktari wa mifugo ili ujue kwa nini anapinda mgongo.
nimeanza kufuga kwa mara ya kwanza kuku wa kienyeji! kwa kuanza nimenunua kuku 9 kati ya hao jogoo ni moja ambaye namwona bado ndama . nina siku ya tatu tangia nianze na leo nimeamka nimeona kuku mmoja anapinda mgongo na anakuwa kazubaazubaa sasa sijui kama ndio kideri kimeanza! naomba mdaqu mwenye uzoefu na hawa wadudu anishauri ni dawa gani naweza kuwapa ili kunusuru hawa jamaa!View attachment 72018
View attachment 72019
 
M

Mzee Mukaruka

JF-Expert Member
Joined
Jun 18, 2012
Messages
448
Points
250
M

Mzee Mukaruka

JF-Expert Member
Joined Jun 18, 2012
448 250
Mbona umewafunga kwenye machuma! Ili iweje na huyo jogoo atazalisha vipi chini ya ulinzi huo? Wape uhuru watembeetembee kwani hili pia ni zoezi tosha kwa afya zao mkuu!
 
THE BIG SHOW

THE BIG SHOW

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2012
Messages
13,992
Points
2,000
THE BIG SHOW

THE BIG SHOW

JF-Expert Member
Joined Feb 28, 2012
13,992 2,000
kila la heri,na ni mwanzo mzuuri tuh

kwa maisha haya ya sasa hatuwez ishi bila ujasiriamali

hongera sana
 
Forum statistics

Threads 1,283,903
Members 493,869
Posts 30,805,569
Top