Nimeamua kuwatetea Lowassa, Chenge na Rostam

Nimeamua kuwatetea Lowassa, Chenge na Rostam

Namna uliyotumia kujieleza kwamba UNAWATETEA ndio inayokufanya na itakayokufanya usieleweke kwa wengi. Umeuliza maswali mepesi, basi ulipaswa utoe na utetezi mwepesi ulio sawa na maswali yako. Hujatoa utetezi wowote zaidi ya kuuliza tu maswali.

Isitoshe fahamu kwamba hao watu wanatuhumiwa na WANANCHI walio wengi, bila hivyo hata CCM wasinge vurugana kama sasa. Mi nakujibu

- Lowassa anatuhuma za kuingiza nchi hasara kubwa kwa kuruhusu kuingia mkataba na kampuni feki ya kufua umeme wakati akiwa Waziri Mkuu. Na ufisadi unaanzia hapo, mtu wa ngazi ya Waziri Mkuu wa nchi kukosa watu makini wa kuchunguza tu suala dogo la uwepo wa kampuni au la sio kitu kidogo. Na hapa ndio panaanza kuleta harufu ya ufisadi kwamba either yumo ktk mpango wa kupata fedha za hiyo kampuni feki, au yeye ni mmoja wa waanzilishi.

Utetezi wake ni kukataa tu kwamba hausiki. Mara ooh, tatizo ni uwaziri mkuu. Huu utetezi hauendani na tuhuma zenyewe. Ni utetezi mwepesi sana, kama vile kukana mahakamani kwamba hujahusika kuiba (kwa lengo la kupata dhamana) wakati ulionekana wazi wazi unaiba.
Na fahamu kwamba kuongoza umma ni dhamana kubwa sana, ukiboronga kwenye maeneo nyeti ambayo yanagharimu pesa nyingi za walipa kodi walalahoi, wananchi hawawezi kukuamini tena. Achia ngazi, usilazimishe uaminike hata kama unajua kuchapa kazi namna gani.

Lowassa huyu huyu anatuhuma kutoka hadi kwa Hayati Mwalimu Nyerere. Aliwahi kuulizwa "Kijana mdogo kama wewe umetoa wapi utajiri mkubwa huo ulionao, halafu unataka uongozi wa nchi?? Hufai kabisa"

Chenge anatuhuma za ufisadi kwenye rada, tuhuma ambazo zimeigharimu BAE kuilipa Tanzania mamilioni ya paundi. Na kama vile haitoshi, Uingereza wenyewe walishasema wazi Chenge bado hajasafishika. Vilevile huyu huyu Chenge hajasema zile pesa alizoweka benki kule karibu na visiwa vya Uingereza (zaidi ya Bilioni 1 za Tanzania) kazipataje, anaishia kusema tu "Ni vijisent)

Nakushangaa unaulizia mpaka Rostam Aziz. Hata mtoto wa darasa la tatu anaweza kukwambia sifa za Rostam. Yeye ndio anasemwa kama mfanikishaji namba 1 wa mkataba na kampuni feki niliyoeleza hapo juu kwa Lowassa. Anahusishwa hadi kwenye Kagoda.

Ngoja sasa nikueleze kujiuzuru kwao kunavyoweza kuleta unafuu wa maisha kwa mtanzania
- Kutatoa nafasi kwa uchunguzi wa kina kufanyika dhidi ya tuhuma zinazowakabili. Uchunguzi utakuwa huru, tofauti na wanapokuwa kwenye nyazifa zao. Hizi tuhuma zinaweza kuja kuzaa matunda ukipatikana ushahidi wa kutosha kuwaburuza mahakamani, na hatimaye Richmond wasilipwe na pengine wapigwe faini kubwa kama ilivyowatokea BAE. Hizo pesa haziwezi kuwaletea unafuu wa maisha wananchi???

- Kuondoka kwao kwenye nyadhifa zao (pengine wakiondolewa na walioshiriki nao kwenye ufisadi) kutatoa nafasi kwa watanzania wengine kushika hizo nafasi, ambao watatumia nasafi hizo kuwaletea wananchi wenzao unafuu wa maisha, sambamba na unafuu wa maisha yao binafsi

- Pia utakuwa mwanzo wa kuondolewa kwa mafisadi kwenye sehemu zingine, na hatimaye tukapata watu wazalendo wa kweli wa kutuletea maendeleo ya kweli

Mkuu wewe ni makini! Umeua kila kitu na huyo bwana aliyejipachika msalaba wa kuwa mtetezi sasa imedhihirika kwamba anawaharibia maana angalau watanzania walishaisahau hii hoja. Sasa kama ameamua kuzifufua chuki zilizopita ajue kwamba hiyo itakula kwa akina RACHEL. Yaani dhambi za hawa jamaa hata walio gerezani (Ukonga au Segerea) wanazifahamu sasa huyo mtetezi sijui alikuwa Guantanamo Bay!
 
Unajuwa jana wakati unaanzisha hii thread kwa sababu ilikuwa ni jumapili basi nikajuwa umeshlamba viroba au valouer zimekulevya, sasa na leo jumatatu umeamka na topic hii hii, yaani kwamba umezamilia! sina hamu.

Mkuu Matola as far as uko hapa and provided that you are not Fooled with the so called "Kujivua Gamba" and the most important ukiwa kama Greta Thinker basi utanielewa.

Ila kama

1. Wewe ni Shabiki wa Magamba basi itakuchukua Miaka Mingi kunielewa na Ikifikia Umenielewa Basi Ushakuwa Mzee
 
Mkuu Sikuelewi Hizi si Story kaka I'm for Real. I Stand for Edward, Andrew and Rostam

Wewe uko Upande Gani? Wa kujivua Gamba?

ni wachache sana watakuelewa, wengi wanajibu juujuu pasipo kuelewa kuwa hujawatetea kuwa wao sio mafisadi lakini unataka serikali inayowaita mafisadi ipambanue ufisadi wao na tija kwa watanzania baada ya wao kutoswa, HILO HALITAWEZEKANA MAANA RACHEL NI CCM NA CCM NI SERIKALI INAYOTAWALA=UFISADI WA RACHEL UNAJUMUISHA SERIKALI MOJA KWA MOJA BILA KUUMA MANENO, (asante kwa atakae nielewa)
 
Mkuu wewe ni makini! Umeua kila kitu na huyo bwana aliyejipachika msalaba wa kuwa mtetezi sasa imedhihirika kwamba anawaharibia maana angalau watanzania walishaisahau hii hoja. Sasa kama ameamua kuzifufua chuki zilizopita ajue kwamba hiyo itakula kwa akina RACHEL. Yaani dhambi za hawa jamaa hata walio gerezani (Ukonga au Segerea) wanazifahamu sasa huyo mtetezi sijui alikuwa Guantanamo Bay!

Ha ha ha Hawna Makosa Ndiyo Maana Kutwa Vikao vya Kuwabembeleza, Wewe Unampa MWIZ SIKU TISINI AJIHUKUMU ha ha haaaaaaaaa
 
Which System?

The government of Tanzania. Hivi unafikiriaje suala la watu ambao si siku nyingi zimepita
rais (wakati huo akiwa mgombea) aliwasifia kuwa ni wachapakazi hodari, leo hii tunaambiwa
kuwa ni magamba wanatakiwa wajivue. Lakini hapohapo bado wanashikilia nafasi nyeti ndani ya chama.
Hii maana yake ni nini?
 
Wanaoshabikia na Kubeza Division Zero 310,826 nawashangaa!
Kwani Lengo la Community School nikutaka kumpa mwananchi nafasi ya kupata Elimu ya watoto na Kusimamia Shule zenyewe!Lowasa(Waziri Mkuu Mtendaji) alihamasisha zijengwe zikajengwa!Baadae akaondoka Serikalini Shule zikadumaa na Wananchi tukakalala!
Pamoja na Porojo zote Lowasa ndio alikuwa waziri Mkuu anayefaa kwa aina ya watu wa Tanzania!
Akisimamia jambo analifuatilia kwa nguvu zote hadi linafanikiwa!Na nasema bila woga enzi zake nilianza kuona serikali inayofanya Kazi!
Mipango mingi ilidorora alipo ondoka!Hakuna wa Kuhamasisha Ujenzi wa Hosteli za Shule na Nyumba za Walimu wamebaki wa Kuangalia Matokeo!
Ngoyai Olaigwanani Mkuu asibezwe!
Kama Kujivua Gamba alionyesha mfano Akaamua Kuachia Ngazi!

Mbona hata zile shule za Monduli ambako yeye ni mbunge wake na mwenye dhamana na jukumu la usimamizi wake zimetoa matokeo mabovu ajabu! Tuache kumpamba asipostahili!
 
ni wachache sana watakuelewa, wengi wanajibu juujuu pasipo kuelewa kuwa hujawatetea kuwa wao sio mafisadi lakini unataka serikali inayowaita mafisadi ipambanue ufisadi wao na tija kwa watanzania baada ya wao kutoswa, HILO HALITAWEZEKANA MAANA RACHEL NI CCM NA CCM NI SERIKALI INAYOTAWALA=UFISADI WA RACHEL UNAJUMUISHA SERIKALI MOJA KWA MOJA BILA KUUMA MANENO, (asante kwa atakae nielewa)

Mkuu Umewatafunia sasa ni Jukumu lao Kumeza, sasa Umesema waziwazi na ambaye hataelewa basi ana matatizo

Watanielewa tu Taratibu
 
Kwa kipindi cha miezi miwili sasa imepita Tangu Chama Cha Mapinduzi ( CCM) kutangaza ilichokiita Kujivua Gamba kwa Lengo Si la kuboresha Maisha ya Watanzania bali KUKINUSURU Chama Cha Mapindizi ( Sijui nani kawadanganya kuwa wananchi watalia na kuomboleza siku wakisikia CCM imekufa ).

Moja kati ya Mikakati yao ni kuwaomba ( Wenyewe wanadai kuwataka, lakini huwezi kumtaka mtu ajiuzulu halafu unakaa naye Kikao cha Kumuomba ajiuzulu) wale wote wanatuhumiwa kwa ufisadi uliokichafua Chama Cha Mapinduzi Machoni mwa Watanzania. Lakini CCM hao hao hakuna Mahali wamesema kwamba

1. Ni Lini Lowasa, Chenge na Rostam walituhumiwa kwa ufisadi
2. Ni Wapi Lowasa, Chenge na Rostam walituhumiwa Kwa Ufisadi
3. Ni Nani aliyewatuhumu Lowasa, Rostam na Chenge kwa Ufisadi wao
4. Ni Vipi Lowasa, Rostam na Chenge waliingia BOT na kukwapua Mabilioni ya Shilingi.
5. Ni kwa vipi Kujiuzulu kwa Hao watatu kutaleta Nafuu kwa maisha ya Watanzania

Mpaka hapo CCM itakapotoa majibu kwa Maswali hayo Mepesi Nitaendelea kuwatetea Lowasa, Rostam na Chenge

Asanteni
mKUU Alberto mimi nakuuunga mkono 100% mwenyewe nawatetea kwa moyo woote tena bila unafiki na CDM hawa watu wakija wapokeeni, sioni tatizo kwao zaidi ya udhaifu wa JK tuu na serikali yake ya ccm, Kuondoka kwa hawa watu ndani ya ccm hakutapunguza hata kidogo ugumu makali ya maisha. ile yali ya ufisadi ndani ya ccm wameiruhusu wenyewe na hilo ndo tatizo kubwa kiasi kwamba imekuwa kufanya ufisadi ni SIFA, wakina ROSTAM wanaonewa tuu!
 
The government of Tanzania. Hivi unafikiriaje suala la watu ambao si siku nyingi zimepita
rais (wakati huo akiwa mgombea) aliwasifia kuwa ni wachapakazi hodari
, leo hii tunaambiwa
kuwa ni magamba wanatakiwa wajivue. Lakini hapohapo bado wanashikilia nafasi nyeti ndani ya chama.
Hii maana yake ni nini?

Ndiyo Maana nimeamua KUWATETEA hawa JAMAA kwa Maslahi ya Watanzania
 
Mkuu wewe ni makini! Umeua kila kitu na huyo bwana aliyejipachika msalaba wa kuwa mtetezi sasa imedhihirika kwamba anawaharibia maana angalau watanzania walishaisahau hii hoja. Sasa kama ameamua kuzifufua chuki zilizopita ajue kwamba hiyo itakula kwa akina RACHEL. Yaani dhambi za hawa jamaa hata walio gerezani (Ukonga au Segerea) wanazifahamu sasa huyo mtetezi sijui alikuwa Guantanamo Bay!
hizoo zooote zitabaki shutuma tuu kwani kwa sasa hata kesi mahakamani zipo???
ACHENI KUWACHAFUA WENZENU BANA!
 
hizoo zooote zitabaki shutuma tuu kwani kwa sasa hata kesi mahakamani zipo???
ACHENI KUWACHAFUA WENZENU BANA!

CCM Watu wa Ajabu sana WASHIRIKIANE KULA NYAMA ZA WATU HALAFU wanataka kuwazuga WANANCHI kwa KAFARA ya Edward, Andrew na Rostam
 
Kwa kipindi cha miezi miwili sasa imepita Tangu Chama Cha Mapinduzi ( CCM) kutangaza ilichokiita Kujivua Gamba kwa Lengo Si la kuboresha Maisha ya Watanzania bali KUKINUSURU Chama Cha Mapindizi ( Sijui nani kawadanganya kuwa wananchi watalia na kuomboleza siku wakisikia CCM imekufa ).

Moja kati ya Mikakati yao ni kuwaomba ( Wenyewe wanadai kuwataka, lakini huwezi kumtaka mtu ajiuzulu halafu unakaa naye Kikao cha Kumuomba ajiuzulu) wale wote wanatuhumiwa kwa ufisadi uliokichafua Chama Cha Mapinduzi Machoni mwa Watanzania. Lakini CCM hao hao hakuna Mahali wamesema kwamba

1. Ni Lini Lowasa, Chenge na Rostam walituhumiwa kwa ufisadi
2. Ni Wapi Lowasa, Chenge na Rostam walituhumiwa Kwa Ufisadi
3. Ni Nani aliyewatuhumu Lowasa, Rostam na Chenge kwa Ufisadi wao
4. Ni Vipi Lowasa, Rostam na Chenge waliingia BOT na kukwapua Mabilioni ya Shilingi.
5. Ni kwa vipi Kujiuzulu kwa Hao watatu kutaleta Nafuu kwa maisha ya Watanzania

Mpaka hapo CCM itakapotoa majibu kwa Maswali hayo Mepesi Nitaendelea kuwatetea Lowasa, Rostam na Chenge

Asanteni
Mi nipo upande wako, maana nimefikiri kwa muda mrefu, iweje wawatose hawa watu watatu kwa kisingizio cha kujivua gamba wakati kuna msururu wa mafisadi ndani ya ccm maana ukiwapanga kwa mstari wanafika Morogoro. Halafu kuwatosa kirahisi rahisi namna hiyo sio vizuri, BAADA YA KUWATOSA WAWAPELEKE NA MAHAKAMANI ili tujue mbivu na mbichi, watamtaja Chinga na JK kuwa walishirikiana nao kwenye huo UFISADI.
 
Albedo,
Endelea kuwatetea kwa nguvu zote. Ile mitambo iliowachafua sana ya Richmond kisha ikawa Dowans na sasa Symbion imewashwa na mgao umepungua.
 
Kwa kipindi cha miezi miwili sasa imepita Tangu Chama Cha Mapinduzi ( CCM) kutangaza ilichokiita Kujivua Gamba kwa Lengo Si la kuboresha Maisha ya Watanzania bali KUKINUSURU Chama Cha Mapindizi ( Sijui nani kawadanganya kuwa wananchi watalia na kuomboleza siku wakisikia CCM imekufa ).

Moja kati ya Mikakati yao ni kuwaomba ( Wenyewe wanadai kuwataka, lakini huwezi kumtaka mtu ajiuzulu halafu unakaa naye Kikao cha Kumuomba ajiuzulu) wale wote wanatuhumiwa kwa ufisadi uliokichafua Chama Cha Mapinduzi Machoni mwa Watanzania. Lakini CCM hao hao hakuna Mahali wamesema kwamba

1. Ni Lini Lowasa, Chenge na Rostam walituhumiwa kwa ufisadi
2. Ni Wapi Lowasa, Chenge na Rostam walituhumiwa Kwa Ufisadi
3. Ni Nani aliyewatuhumu Lowasa, Rostam na Chenge kwa Ufisadi wao
4. Ni Vipi Lowasa, Rostam na Chenge waliingia BOT na kukwapua Mabilioni ya Shilingi.
5. Ni kwa vipi Kujiuzulu kwa Hao watatu kutaleta Nafuu kwa maisha ya Watanzania

Mpaka hapo CCM itakapotoa majibu kwa Maswali hayo Mepesi Nitaendelea kuwatetea Lowasa, Rostam na Chenge

Asanteni
kweli mkuuuu watupe majibu
 
CCM Watu wa Ajabu sana WASHIRIKIANE KULA NYAMA ZA WATU HALAFU wanataka kuwazuga WANANCHI kwa KAFARA ya Edward, Andrew na Rostam
CCM wahuni kwanza ilitakiwa wadhibitishe uwizi na ufisadi wa hawa jamaa ndipo wawafukuze kwenye chama sasa wanataka kuwafukuza watu kwa maneno ya DR Slaa na magazeti tuuu! hiii siyo haki kabisa!
 
Albedo,
Endelea kuwatetea kwa nguvu zote. Ile mitambo iliowachafua sana ya Richmond kisha ikawa Dowans na sasa Symbion imewashwa na mgao umepungua.

Mkuu Baniani Mbaya ......
 
1. Ni Lini Lowasa, Chenge na Rostam walituhumiwa kwa ufisadi
2. Ni Wapi Lowasa, Chenge na Rostam walituhumiwa Kwa Ufisadi
3. Ni Nani aliyewatuhumu Lowasa, Rostam na Chenge kwa Ufisadi wao
4. Ni Vipi Lowasa, Rostam na Chenge waliingia BOT na kukwapua Mabilioni ya Shilingi.
5. Ni kwa vipi Kujiuzulu kwa Hao watatu kutaleta Nafuu kwa maisha ya Watanzania

Siwatetei ila naona tuhuma dhidi yao ni kuuficha uchafu wa walio wengi, sasa hawa wasiondoke ili tuyaone yaliyojificha sirini zaidi. wakikubali kuondoka haya majibu hayatapatikana kamwe na kwahio wezi wataongezeka.
 
albedo,
endelea kuwatetea kwa nguvu zote. Ile mitambo iliowachafua sana ya richmond kisha ikawa dowans na sasa symbion imewashwa na mgao umepungua.

hapa pia ni great thinkers tu ndo watakuelewa km wataunganisha na topic ya albedo.
 
[QUOTE=Albedo;2059010]''Kwa .......Tangu Chama Cha Mapinduzi ( CCM) kutangaza ilichokiita Kujivua Gamba ........''
''Mpaka hapo CCM itakapotoa majibu kwa Maswali hayo Mepesi Nitaendelea kuwatetea Lowasa, Rostam na Chenge
'Asanteni[/QUOTE]


Albe,
your thread is thought provoking.
Sijaona mahali CCM ilipo define huko ''kujivua gamba'' na ndio maana wengi wamekuja na tafsiri zao tofauti na wanakuwa sensitive unapotoa tamko kama hilo la kuwatetea.....taabu yetu iko kwa huyo kinyonga mkuu anayetaka kupendwa na wote na anayewaogopa waliomsukumiza kuvaa viatu vinavyompwaya (naambiwa kuna wakati - 2005- alionyesha kuogopa wakamshinikiza kwenda chukua fomu ya ugombea) na ndiye aliyekuja na hiyo vague concept ya kujivua gamba! Je na huyu naye unasemaje juu yake?

 
Back
Top Bottom