Nimeamua kuwatetea Lowassa, Chenge na Rostam

Nipo Kagoda Agriculture na Caspian construction & Caspian Mining.

Now you are coming to the My POINT, Ukipunguza Jazba na Ukiacha Kujibu Based on Emmotional. Kimsingi Uko Upande wangu
 
1. Ni Lini Lowasa, Chenge na Rostam walituhumiwa kwa ufisadi
2. Ni Wapi Lowasa, Chenge na Rostam walituhumiwa Kwa Ufisadi
3. Ni Nani aliyewatuhumu Lowasa, Rostam na Chenge kwa Ufisadi wao
4. Ni Vipi Lowasa, Rostam na Chenge waliingia BOT na kukwapua Mabilioni ya Shilingi.
5. Ni kwa vipi Kujiuzulu kwa Hao watatu kutaleta Nafuu kwa maisha ya Watanzania

I salute your 1-5 questions but I would not go to the extent of standing by RACHEL just because I don't have answerz to 1-5. I think we have two issues here, allegations against RACHEL (for which answers to q1-5 will shed light on) and the fact that allegations levelled against RACHEL have more to do with the nation than CCM. CCM uses RACHEL to try to save face but downplays RACHEL impact on the nation. For the latter, they don't enjoy my sympathy, no matter what!!
 
Kwa kipindi cha miezi miwili sasa imepita Tangu Chama Cha Mapinduzi ( CCM) kutangaza ilichokiita Kujivua Gamba kwa Lengo Si la kuboresha Maisha ya Watanzania bali KUKINUSURU Chama Cha Mapindizi ( Sijui nani kawadanganya kuwa wananchi watalia na kuomboleza siku wakisikia CCM imekufa ).

Moja kati ya Mikakati yao ni kuwaomba ( Wenyewe wanadai kuwataka, lakini huwezi kumtaka mtu ajiuzulu halafu unakaa naye Kikao cha Kumuomba ajiuzulu) wale wote wanatuhumiwa kwa ufisadi uliokichafua Chama Cha Mapinduzi Machoni mwa Watanzania. Lakini CCM hao hao hakuna Mahali wamesema kwamba

1. Ni Lini Lowasa, Chenge na Rostam walituhumiwa kwa ufisadi
2. Ni Wapi Lowasa, Chenge na Rostam walituhumiwa Kwa Ufisadi
3. Ni Nani aliyewatuhumu Lowasa, Rostam na Chenge kwa Ufisadi wao
4. Ni Vipi Lowasa, Rostam na Chenge waliingia BOT na kukwapua Mabilioni ya Shilingi.
5. Ni kwa vipi Kujiuzulu kwa Hao watatu kutaleta Nafuu kwa maisha ya Watanzania

Mpaka hapo CCM itakapotoa majibu kwa Maswali hayo Mepesi Nitaendelea kuwatetea Lowasa, Rostam na Chenge

Asanteni

Namna uliyotumia kujieleza kwamba UNAWATETEA ndio inayokufanya na itakayokufanya usieleweke kwa wengi. Umeuliza maswali mepesi, basi ulipaswa utoe na utetezi mwepesi ulio sawa na maswali yako. Hujatoa utetezi wowote zaidi ya kuuliza tu maswali.

Isitoshe fahamu kwamba hao watu wanatuhumiwa na WANANCHI walio wengi, bila hivyo hata CCM wasinge vurugana kama sasa. Mi nakujibu

- Lowassa anatuhuma za kuingiza nchi hasara kubwa kwa kuruhusu kuingia mkataba na kampuni feki ya kufua umeme wakati akiwa Waziri Mkuu. Na ufisadi unaanzia hapo, mtu wa ngazi ya Waziri Mkuu wa nchi kukosa watu makini wa kuchunguza tu suala dogo la uwepo wa kampuni au la sio kitu kidogo. Na hapa ndio panaanza kuleta harufu ya ufisadi kwamba either yumo ktk mpango wa kupata fedha za hiyo kampuni feki, au yeye ni mmoja wa waanzilishi.

Utetezi wake ni kukataa tu kwamba hausiki. Mara ooh, tatizo ni uwaziri mkuu. Huu utetezi hauendani na tuhuma zenyewe. Ni utetezi mwepesi sana, kama vile kukana mahakamani kwamba hujahusika kuiba (kwa lengo la kupata dhamana) wakati ulionekana wazi wazi unaiba.
Na fahamu kwamba kuongoza umma ni dhamana kubwa sana, ukiboronga kwenye maeneo nyeti ambayo yanagharimu pesa nyingi za walipa kodi walalahoi, wananchi hawawezi kukuamini tena. Achia ngazi, usilazimishe uaminike hata kama unajua kuchapa kazi namna gani.

Lowassa huyu huyu anatuhuma kutoka hadi kwa Hayati Mwalimu Nyerere. Aliwahi kuulizwa "Kijana mdogo kama wewe umetoa wapi utajiri mkubwa huo ulionao, halafu unataka uongozi wa nchi?? Hufai kabisa"

Chenge anatuhuma za ufisadi kwenye rada, tuhuma ambazo zimeigharimu BAE kuilipa Tanzania mamilioni ya paundi. Na kama vile haitoshi, Uingereza wenyewe walishasema wazi Chenge bado hajasafishika. Vilevile huyu huyu Chenge hajasema zile pesa alizoweka benki kule karibu na visiwa vya Uingereza (zaidi ya Bilioni 1 za Tanzania) kazipataje, anaishia kusema tu "Ni vijisent)

Nakushangaa unaulizia mpaka Rostam Aziz. Hata mtoto wa darasa la tatu anaweza kukwambia sifa za Rostam. Yeye ndio anasemwa kama mfanikishaji namba 1 wa mkataba na kampuni feki niliyoeleza hapo juu kwa Lowassa. Anahusishwa hadi kwenye Kagoda.

Ngoja sasa nikueleze kujiuzuru kwao kunavyoweza kuleta unafuu wa maisha kwa mtanzania
- Kutatoa nafasi kwa uchunguzi wa kina kufanyika dhidi ya tuhuma zinazowakabili. Uchunguzi utakuwa huru, tofauti na wanapokuwa kwenye nyazifa zao. Hizi tuhuma zinaweza kuja kuzaa matunda ukipatikana ushahidi wa kutosha kuwaburuza mahakamani, na hatimaye Richmond wasilipwe na pengine wapigwe faini kubwa kama ilivyowatokea BAE. Hizo pesa haziwezi kuwaletea unafuu wa maisha wananchi???

- Kuondoka kwao kwenye nyadhifa zao (pengine wakiondolewa na walioshiriki nao kwenye ufisadi) kutatoa nafasi kwa watanzania wengine kushika hizo nafasi, ambao watatumia nasafi hizo kuwaletea wananchi wenzao unafuu wa maisha, sambamba na unafuu wa maisha yao binafsi

- Pia utakuwa mwanzo wa kuondolewa kwa mafisadi kwenye sehemu zingine, na hatimaye tukapata watu wazalendo wa kweli wa kutuletea maendeleo ya kweli
 
Kama huna thread ya maana ya kushare na watu basi soma za wenzako, sio lazima uanzishe thread. mambo mengine ni kuja kujidharirisha tu hapa jamvini, by the way leo ni jumapili unaweza kwenda kupata kitimoto yako siku ikawa imekwenda. na nadhani leo hamna cha maana hapa jamvini kumejaa stori za kusadikika tu, mara mwingine kajifanya yeye ndio Edward Lowasa basi ili mradi ni vituko na porojo tupu. ni bora nisign out. endeleeni na porojo zenu wenyewe.

matola!!! matola!!!! matola!!!!! unatamani ccm inusurike! imekabwa na fupa (rachel) wewe hujatambua kuwa adui wa watanzania(watanganyika) anajimaliza kwa silaha zake, unatakiwa kuwasaidia watoweke kwenye uso wa dunia. CHENGE WANYUNYIZIE KAMA BUNGENI WATANYWEA hatimaye mtadondoka nao.
 
Wanaoshabikia na Kubeza Division Zero 310,826 nawashangaa!
Kwani Lengo la Community School nikutaka kumpa mwananchi nafasi ya kupata Elimu ya watoto na Kusimamia Shule zenyewe!Lowasa(Waziri Mkuu Mtendaji) alihamasisha zijengwe zikajengwa!Baadae akaondoka Serikalini Shule zikadumaa na Wananchi tukakalala!
Pamoja na Porojo zote Lowasa ndio alikuwa waziri Mkuu anayefaa kwa aina ya watu wa Tanzania!
Akisimamia jambo analifuatilia kwa nguvu zote hadi linafanikiwa!Na nasema bila woga enzi zake nilianza kuona serikali inayofanya Kazi!
Mipango mingi ilidorora alipo ondoka!Hakuna wa Kuhamasisha Ujenzi wa Hosteli za Shule na Nyumba za Walimu wamebaki wa Kuangalia Matokeo!
Ngoyai Olaigwanani Mkuu asibezwe!
Kama Kujivua Gamba alionyesha mfano Akaamua Kuachia Ngazi!
 
Anayesema Ngoyai Alifukuzwa Na Mwl Nyerere AICC hana Data!Wakati ngoyai yupo AICC Mzee Ruksa ndio alikuwa Madarakani nyererere alishang'atuka! Alikuwa AICC miaka ya mwisho ya 80!Wakati wa Awamu Muhula wa 2 Ya Mzee Ruksa Ndio Lowasa Kikapanda na Kuwa Waziri
Nakumbuka kipindi hicho nilikuwa Ilboru Sekondary
 
Hata mimi namtetea Lowassa, hasa kwa sababu Kamati ya Mwakyembe haikutoa yote yaliyopaswa kujulikana kwa Umma. Kama na JK anahusika walipaswa kutueleza, otherwise nasema Lowassa alitolewa kafara
 
Kwa kipindi cha miezi miwili sasa imepita Tangu Chama Cha Mapinduzi ( CCM) kutangaza ilichokiita Kujivua Gamba kwa Lengo Si la kuboresha Maisha ya Watanzania bali KUKINUSURU Chama Cha Mapindizi ( Sijui nani kawadanganya kuwa wananchi watalia na kuomboleza siku wakisikia CCM imekufa ).

Moja kati ya Mikakati yao ni kuwaomba ( Wenyewe wanadai kuwataka, lakini huwezi kumtaka mtu ajiuzulu halafu unakaa naye Kikao cha Kumuomba ajiuzulu) wale wote wanatuhumiwa kwa ufisadi uliokichafua Chama Cha Mapinduzi Machoni mwa Watanzania. Lakini CCM hao hao hakuna Mahali wamesema kwamba

1. Ni Lini Lowasa, Chenge na Rostam walituhumiwa kwa ufisadi
2. Ni Wapi Lowasa, Chenge na Rostam walituhumiwa Kwa Ufisadi
3. Ni Nani aliyewatuhumu Lowasa, Rostam na Chenge kwa Ufisadi wao
4. Ni Vipi Lowasa, Rostam na Chenge waliingia BOT na kukwapua Mabilioni ya Shilingi.
5. Ni kwa vipi Kujiuzulu kwa Hao watatu kutaleta Nafuu kwa maisha ya Watanzania

Mpaka hapo CCM itakapotoa majibu kwa Maswali hayo Mepesi Nitaendelea kuwatetea Lowasa, Rostam na Chenge

Asanteni

And then you go out there telling people that you have nade a spirited defence for the three musketeers? Shame on you! In politics, perception can stick and bear tangible results. Lakini nikwambie jambo moja tu. Inahitaji akili ya mwendawazimu (sina hakika kama wewe ni mmoja wao) kuamka na kudhani kwamba unaweza kuja na hizo taarabu zako kuhusiana na mapacha hawa watatu. Nyie ndiyo mnaodhani kufumania ndiyo ushahidi pekee wa spouse kukosa uaminifu. Kwa taarifa yako ushahidi wa vitendo vya ubadhirifu au wizi wa hawa mabwege wako siyo lazima uwe ni hukumu ya mahakama kwa sababu sisi tunachofanya siyo kuwahukumu kwenda jela. Hizo porojo zake waambie wasio na akili timamu lakini wenye akili timamu wote (hata mama yangu ambaye hajui kusoma) wanajua kwamba hawa ni madui wa ustawi wa watanzania na uache kutuchosha kwa hoja zako za kitoto!
 
Kwanza nianze kwa kukupongeza kwa mawazo mazuri haya....Labda nichangie kwa kuwakumbusha maelezo ya mwenyekiti wa chama cha magamba alipotuhumiwa kuwanadi watuhumiwa hawa hawa wa ufisadi wakati wa kampeni...Alijitetea kwa kusema...Nimewanadi kwa sababu kamati kuu ya CCM iliazimia wagombee nafasi hizo kwa sababu kilichopo mbele yao ni tuhuma tu za ufisadi na hakuna aliyethibitika kuwa na hatia...sasa leo hii wanawabembeleza kujiuzulu.? nini hiki? 1. Mtu anayethibitika kufanya ufisadi,au wizi wa mali ya umma,habembelezwi kujiuzulu bali hushinikizwa ama hulazimika kujiuzulu tena mara moja!! sio aendelee kuiba mpaka siku 90 zikiiisha ndio ajiuzulu... 2.Kama hawa watu walinadiwa eti kwa sababu kilichokuwa mbele yao ilikuwa ni tuhuma tu,leo hii mnavyowataka kujiuzulu ni kwa sababu gani? tuhuma au imeshathibitika? na kama imeshathibitika ni kwa vipi? 3. CCM wameshakunywa sumu ya kuutoa uhai wao wanafikiri kujiuzulu kwa hawa wa3 ndio pona yao..wako wrong sana..wakishajiuzulu itakuwa ni kuthibitishia umma wa watanzania kwamba ni kweli wamehusika na ufisadi..na hapo pressure nyingine kubwa mno itazaliwa toka kwa vyama vya upinzani na wanaharakati,ya kwamba kama kweli wamekubali kuhusika na ufisadi basi itabidi wafikishwe mahakamani na kuhukumiwa..maana Taifa limefika pabaya kwa ufisadi mkubwa walioutekeleza...Nimalizie kwa kusema mkuu Albedo mimi naungana nawe Kuwa support akina Lowassa,mpaka CCM watakapothibitisha ufisadi walioufanya na kuwafikisha mahakamani na kuwahukumu..bila hivyo sishoboki na sinema yao hii ya KUVUA GAMBA
 
Mimi nawashauri Lowassa, Chenge & Rostam wasife peke yao. Ni bora wamlipue na huyu jamaa ambaye haeleweki, JMK. Kwa nini awatose wao peke yao wakati hizo hela walizitumia kwa maslahi yao wote. Huu ni uanfiki wa watanzania, ati jk anaangushwa na mafisadi, watendaji wake. Huu ni uongo semeni JMK na serikali yake wamewaangusha watanzania.

RACHEL komaa mfe naye huyo jama anataka kuwatosa baharini shukeni naye mfe wote. Ala!
Muda wa kumlipua ni sasa wakishatoswa watamlipulia wapi itaonekana ni revenge tu au hasira za kutimuliwa, na kama hawawezi kumlipua sasa hivi na wakae kimya hata wakitoswa hakuna wa kuwahurumia
 
Du so msekwa ndo katumwa kuwabembeleza atari ila ndo kuelekea kwenye mapinduz ya kwel
 
Kwa kipindi cha miezi miwili sasa imepita Tangu Chama Cha Mapinduzi ( CCM) kutangaza ilichokiita Kujivua Gamba kwa Lengo Si la kuboresha Maisha ya Watanzania bali KUKINUSURU Chama Cha Mapindizi ( Sijui nani kawadanganya kuwa wananchi watalia na kuomboleza siku wakisikia CCM imekufa ).

Moja kati ya Mikakati yao ni kuwaomba ( Wenyewe wanadai kuwataka, lakini huwezi kumtaka mtu ajiuzulu halafu unakaa naye Kikao cha Kumuomba ajiuzulu) wale wote wanatuhumiwa kwa ufisadi uliokichafua Chama Cha Mapinduzi Machoni mwa Watanzania. Lakini CCM hao hao hakuna Mahali wamesema kwamba

1. Ni Lini Lowasa, Chenge na Rostam walituhumiwa kwa ufisadi
2. Ni Wapi Lowasa, Chenge na Rostam walituhumiwa Kwa Ufisadi
3. Ni Nani aliyewatuhumu Lowasa, Rostam na Chenge kwa Ufisadi wao
4. Ni Vipi Lowasa, Rostam na Chenge waliingia BOT na kukwapua Mabilioni ya Shilingi.
5. Ni kwa vipi Kujiuzulu kwa Hao watatu kutaleta Nafuu kwa maisha ya Watanzania

Mpaka hapo CCM itakapotoa majibu kwa Maswali hayo Mepesi Nitaendelea kuwatetea Lowasa, Rostam na Chenge

Asanteni

Hivi waziri mkuu anapoingilia mamlaka ya watendaji wake wa chini, kama alivyofanya Lowassa
kumshinikiza Waziri wa Nishati na Madini kuipa mkataba Richmond wakati akijua kabisa kuwa
ni kampuni ya kitapeli unaionaje hiyo?
 
Ha ha ha Ambaye sasa hivi ni Mbunge siyo
 
And then you go out there telling people that you have nade a spirited defence for the three musketeers? Shame on you! In politics, perception can stick and bear tangible results. Lakini nikwambie jambo moja tu. Inahitaji akili ya mwendawazimu (sina hakika kama wewe ni mmoja wao) kuamka na kudhani kwamba unaweza kuja na hizo taarabu zako kuhusiana na mapacha hawa watatu. Nyie ndiyo mnaodhani kufumania ndiyo ushahidi pekee wa spouse kukosa uaminifu. Kwa taarifa yako ushahidi wa vitendo vya ubadhirifu au wizi wa hawa mabwege wako siyo lazima uwe ni hukumu ya mahakama kwa sababu sisi tunachofanya siyo kuwahukumu kwenda jela. Hizo porojo zake waambie wasio na akili timamu lakini wenye akili timamu wote (hata mama yangu ambaye hajui kusoma) wanajua kwamba hawa ni madui wa ustawi wa watanzania na uache kutuchosha kwa hoja zako za kitoto!

Mkuu So far CCM haijasema ni nini Edward, Andrew na Rostam wameiba, wamefisadi, Wamehujumu. kauli ya CCM ambayo bado inasimama ( Undesputed) ni

1. Ajali ya Kisiasa
2. Rostam ni Jembe
3. Chenge ni Safi n.

Ni kauli Ambazo zilitolewa na Mwenyekiti wa CCM ambaye leo nii Nimejitokeza Kumuunga Mkono na Kusema kwamba Edward, Rostam na Andrew hawana Makosa.

Na kwa sababu jawana makosa basi tunaendelea KUNEGOTIATE nao wapumzike halafu TUTANGAZE tumewatimua kwani Watapoteza nini? Si Wataendelea kula kuku tu
 
Which System?
Unajuwa jana wakati unaanzisha hii thread kwa sababu ilikuwa ni jumapili basi nikajuwa umeshlamba viroba au valouer zimekulevya, sasa na leo jumatatu umeamka na topic hii hii, yaani kwamba umezamilia! sina hamu.
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom