Habari zenu wana jamvi,
Leo nimeamua kuvunja ukimya, nasema ukweli jamani ndugu zangu YESU ni mtamu, acheni nilewe huyu YESU mie. Yeye ni jana leo na hata mileleeee mwanzo na mwisho.
Hakuna kama yeye chini ya jua na kwingine kokote. Ni huyu Yesu aliyenipa elimu baada ya kufeli kwa mara ya kwanza form 4 na kukata tamaa kabisa, ni huyu Yesu, alinionesha njia hadi leo nina CV ya ukweli.
Ni yeye huyu aliyenipa kazi kwa muda mfupi tu baada ya kuhitimu masomo bila ujanja wowote ila kwa MAOMBI tu, ni yeye huyu aliyesimama na mimi pale kazini kupingana nao wale wote walionionyesha chuki na kunitengenezea mazingira ya mimi kufukuzwa kutokana na wivu wa elimu,.
Ni huyu YESU aliyempigania baba yangu kwa miaka 17 sasa akipita katik ajaribu lile.Ni huyu aliyenipa uzima hadi sasa naishi. Any way natamani na wewe umjue huyu MWANAUME ambaye;-
1. Sio msaliti
2. Mwaminifu 100%
3. Rafiki wa kweli nyakati zote
4. Mtimiza ahadi
5. Aliyeyashika maisha yako mkononi mwake
6. nk;
Jamani ndugu zangu tumwamini Yesu, dunia imeshatuchoka na hivyo inataka kututema tu, sasa sijui itakutema wapi, ni wakati wetu vijana tuamke na KUMPOKEA YESU AWE BWANA NA MWOKOZI WETU. AMEEN.
GOD BE WITH YOU