Mimi ni mkristo pia sikuulizi kwa nia mbaya.
Wewe unasema Yesu amefanya baada ya kuhitimu umepata kazi, Sasa kwahiyo watu ambao wanamwamini kama wewe(wengi ninaowafaham) wamehitimu na hametafuta kazi kama wewe hawajapata, kwahiyo je, wao ndo vipi? au huyo Yesu mbaguzi kakusaidia wewe upate kazi halafu wao hawana kazi kawaacha?
Na kingine umepata kazi kama unavyosema ikitokea umefutwa kazi utasema Yesu amekusababisha ufutwe au kitu gani(kwasabu si unasema yesu ndo kakufanya upate kazi?)??
Naomba unifafanulie hapo nikuelewe vizuri kabisa.!
Maswali mazuri sana, nimependa - ila natamani ningekuwa nakuelezea ana kwa ana ingefaa sana maana kuna vitu vingine ni vyema kuvielezea live. Ok nitajaribu kuweka kwa ufupi ili usichoke sana. -
Kwanza kwa haya maswali napata kuhisi kwamba wewe ni mchanga sana ktk masuala ya imani au labda ni muislamu tu, ila si ishu sana.
1. Tambua kwamba niliokoka tangu form 1 na nimekua mtumishi wa Bwana tangu hapo kupitia CASFETA, hivyo nilipomaliza form 4 mara ya kwanza nilifeli na wengine wengi walifaulu. Je hapo Yesu alinisahau? - jibu ni hapana ila alitaka ajitukuze kupitia mimi, nililia nikamwambia Yesu nimekutumikia kipindi chote cha masomo, y this? nilikata tamaa sana, nikarudia mitihani huku YESU nikimuomba kwa hali ya juu aniwezeshe> -
MAOMBI
2. Yesu sio mbaguzi na wala si kwamba hao unaowafahamu Yesu amewaacha NO, -
Isaya 43:26 inasema "Unikumbushe na tuhojiane eleza mambo yako upate kupewa haki yako" - MAOMBI, wapendwa wengi hawaombi, hawafungi, wakiambiwa njoo kuna mkesha tumuombe Mungu mtu haji, lakini ktk harusi hadi sa 9 usiku anaenda.- MAOMBI MAOMBI MAOMBI hili ndio tatizo, na hapa ndipo shetani ametushika sana, TUNAPASWA KUAMUA KUKAA KTK MAOMBI, - SIJISIFU, NILIAMUA KWA DHATI KUOMBA MUNGU, na ndio maana ameonekana,
Naamka usiku saa 9 hadi kumi naomba, usingizi ninao lakini nasema hapana YESU amesema nijaribuni muone - nikadhamilia kumjaribu, Nafunga peke yangu, nyumbani wanaleta kuku na vitu vingine vizuri, nafsi inashawishika kufungulia lakini nasema hapana hadi nimalize maombi jioni.
Kuomba ni mzigo mzito, wengi wanomba wakiwa wamekaa chini matokeo yake ni kusinzia tu, Niliamua kuomba kwa kusimama hadi leo nina uwezo wa kusimama hadi masaa 4 naomba tu huku natembea, na maneno hayajirudii, - MAOMBI MAOMBI, na KUJITAHIDI KUIKIMBIA DHAMBI + MAOMBI TUTASHINDA.
3. Hata ikitokea nimefukuzwa kazi sasa hivi, YESU bado ni wangu tu, hiyo ni sehemu ya majaribu ya kupimwa imani yangu, sitaaacha kamwe.
Nb: Ningekuwa na wewe ana kwa ana ingependeza sana