Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 38,070
- 57,721
Huko nyuma nilikuwa kwenye mahusiano na mdada mtu mzima, kutokana na uzuri wake pamoja na ujuaji wake, mahusiano yalijaa migogoro mingi; hali iliyopelekea ata mtoto aliyezaliwa kuhisi ana wababa zaidi ya mmoja.
Amekuwa akinitafuta katika nyakati zote ngumu anazopitia, kuanzia kwenye kujifungua, misiba ya ndugu, na kuumwa kwa mtoto n.k; nami nilikuwa mwepesi wa kutekeleza.
Ilifikia hali mpaka kumuuliza huyu mtoto ni wa kwangu kweli, yeye akawa ananiaminisha ni wa kwangu.
Ilikuwa ili anipatie huduma ya tendo la ndoa lazima nimtumie salio atakalo ona lina mfaa, ndio aweze kuja.
Mbaya zaidi miezi miwili iliyopita, ndio ilikuwa mwisho wa mawasiliano yetu; nilimtumia salio pamoja na nauli na kuahidi angekuja kunitembelea, mbaya zaidi hakufika na ku-block namba zangu.
Ikabidi nifanye maamuzi magumu ya kuvunja mahusiano na mawasiliano ili maisha mengine yaendelee.
Jana amekuja kunitafuta kwa njia ya simu na kunijulisha amevunjika mguu, anahitaji msaada wa hali na mali ili kukaa sawa.
Sasa najiuliza, hii huruma ya kusaidia watu wasio na shukrani ni sahihi.
Kwangu binafsi nimeamua kukaa pembeni ata kwenye hii changamoto anayopitia, kwa sababu si sahihi mtu akutafute kwenye shida tu.
Wakuu, ungekuwa wewe ungefanya maamuzi yapi?