Nimeamua kusitisha matumizi kwa aliyekuwa mke wangu, kisheria nina makosa?

sambasha

JF-Expert Member
Dec 14, 2015
264
248
Habar zenu wakuu.

Miaka7 iliyopita nlikua na mwanamke tuliishi nae na tukapata watoto wawilii lakini ndani ya uhusiano huu pia tulienda kwa shehe tukafunga ndoa ili tupate cheti kwasababu hyu bibie ni mwalimu na alikua anataka apate uhamisho ahamie mjini kwani alikua akifundisha nje ya mjini.

Hapo ndani maisha yetu mwanamke alikua mkorofi mnoooo mlevi na pia usaliti ndani yake. Sasa kwasababu kule anapoishi ndo kulikua na biashara zangu nikawa naishi kwake nayeye akija mjini anafikia kwangu alizidisha ukorofi hdi akanifukuza kwake nikaondoka nikaendelea na biashara zangu nikanunua gari mbili huku nahudumia watoto.

Hatimae namimi nikaoa kwani mimi ni muislamu na nmepata mtoto mwingine hpo ndo mwalimu akaanza kunisumbua nimuandikie talaka. Wakati huo huo siruhusiwi tena kuwaona wanangu naninalipa ada na pia hela ya matumizi kila wiki. Baada ya kunizuia nimekata huduma zote.

Jee kisheria hapo nina makosa asanteni wakuu naomba ushauri wenu. Natanguliza shukrani
 
Chakufanya omba msaada kisheria ikiwezekana kabsa lea watoto wako chini ya sheria.....

Utakuja kujuta kama utapotezea suala la watoto..

Ushauri wa bure nenda hata ustawi wa jamii kabsa.
 
WATOTO NI HAZINA KUBWA KWA FAMILIA...Jaribu kuukwepesha ugomvi wako wewe na mkeo ili usiwadhuru watoto..Suluhisheni matatizo yenu yaishe.. Mahitaji ya watoto wape kama kawaida kwa sababu ni jukumu lako ukiwa kama Baba mzazi...Usiikimbie Damu yako mkuu
 
Kuacha kuhudumia watoto wako ni kosa kidini na hata Sheria za nchi,matatizo yenu yasiwasababishie watoto kukosa haki zao za msingi
 
Watoto hawana makosa hata usithubutu kuwasitishia ada, wape malezi yote tena ikiwezekana zidisha upendo kwao mara mbili ili wasiathirike kisaikologia kisa ugomvi wako na mkeo. Kisheria ni kosa sana hata kidini ni kosa pia na hata usingekuwa na dini pia kimadili ni kosa.
 
Wakuu sina tatizo katika mahusiano wala sina haja na aliyekuwa mke wangu tatizo ni kwamba nazuiwa kuonanana na watoto wangu hilo tuu ndo tunapishana. Wanangu nawapenda sana shahidi mungu.
 
Sheria ya ndoa ya mwaka 1971, imeweka matakwa kwa mwanaume yeyote kumhudumia mtoto wake ama akiwa katika himaya yake au ya mtu yoyote kwa kumpa mahitaji muhimu kama chakula, mavazi na elimu...

Wajibu wa mwanamke katika kuchangia matunzo ya mtoto kisheria ni pale baba amefariki, haifahamiki anaishi wapi ama baba hana uwezo wa kumtunza.

Ni haki ya mtoto kupata mahitaji muhimu katika maisha yake kwa mujibu wa sheria ya mtoto ya mwaka 2009.

Kitendo cha kupuuzia kumhudumia mtoto Ili hali unauwezo wa kufanya ni kosa la jinai pamoja na kutotoa chochote kwaajili ya mahitaji yake muhimu kama ilivyoanishwa katika kifungu cha 166 na 167 cha kanuni za adhabu.

Suala la yeye kukuzuia kumuona mtoto fahamu sheria inasema hivi

Kisheria, wazazi wanapotengana ama kuachana, mtoto ana haki zifutazo.

1.Kulelewa ama kuhudumiwa pamoja na kupata elimu kama ile aliyopata awali kabla ya wazazi kutengana ama kuachana.

2.Haki ya kuishi na mzazi( baba au mama) ambaye kwa mtazamo wa mahakama aweza kumhudumia kwa maslahi bora ya mtoto.

3.Mtoto ana haki ya kumtembelea na kuishi na mzazi wake wakati wowote anapohitaji, isipokuwa kama tu, itaingilia masomo ama mafunzo yake.

Sheria pia imeweka dhanio (presumption) ya kwamba kwa kuzingatia maslahi bora ya mtoto, kama ni mwenye umri chini ya miaka saba awe na mama yake ingawa dhana hii yaweza pingwa (rebuttabal presumption). Hiyo ni kwa mujibu wa kifungu cha 26(1) cha Sheria ya Mtoto mwaka 2009. Maelezo yako na mtazamo wa kisheria ni kwamba anachokifanya mzazi mwenzako ni kinyume na sheria na kinamnyima haki mtoto na kufanya wewe kushindwa kutekeleza wajibu wako kisheria
 
Kaombe msaada wa kisheria, watoto wako wanahitaji waishi kwa kupata mahitaji yao ya kila siku ili waweze kufikia malengo yao
 
Asante sana mkuu kwa ufafanuzi mzuri. Sasa nifanyeje mkuu
 
Kwa ufafanuzi wako sheria inanibana kwa kutokutoa matumizi na pia inambana na mzazi mwenzangu kwa kunizuia kuona watoto
 
Usithubutu kuwatelekeza wanao unaweza kuja kujuta baadaye. Endelea kuwahudumia kwenye kila kitu ambacho ulikuwa unawahudumia, tafuta msaada wa kisheria ili haki yako ya kuwaona wanao iendelee kuwepo.

Habar zenu wakuu.

Miaka7 iliyopita nlikua na mwanamke tuliishi nae na tukapata watoto wawilii lakini ndani ya uhusiano huu pia tulienda kwa shehe tukafunga ndoa ili tupate cheti kwasababu hyu bibie ni mwalimu na alikua anataka apate uhamisho ahamie mjini kwani alikua akifundisha nje ya mjini.

Hapo ndani maisha yetu mwanamke alikua mkorofi mnoooo mlevi na pia usaliti ndani yake. Sasa kwasababu kule anapoishi ndo kulikua na biashara zangu nikawa naishi kwake nayeye akija mjini anafikia kwangu alizidisha ukorofi hdi akanifukuza kwake nikaondoka nikaendelea na biashara zangu nikanunua gari mbili huku nahudumia watoto.

Hatimae namimi nikaoa kwani mimi ni muislamu na nmepata mtoto mwingine hpo ndo mwalimu akaanza kunisumbua nimuandikie talaka. Wakati huo huo siruhusiwi tena kuwaona wanangu naninalipa ada na pia hela ya matumizi kila wiki. Baada ya kunizuia nimekata huduma zote.

Jee kisheria hapo nina makosa asanteni wakuu naomba ushauri wenu. Natanguliza shukrani
 
Mtoa mada naomba nikuulize swali nje ya ulichokiuliza. Hivi baada ya kuoa mke wa pili huyo hana mapungufu?
 
Mapungufu yapo ya kibinadamu ila sii kama yale ya usaliti na dharau ubabe wa waziwazi.
 
Back
Top Bottom