Makosa makubwa ya mswada wa TISS. Sehemu ya 2

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,987
20,271
MAKOSA MAKUBWA YA MSWADA WA TISS.

SEHEMU YA 2.

Baada ya kuona makosa ya vifungu vya 5 na 16 namna vinavyopingana, na mapendekezo niliyoweka ili kuboresha mswada huu wa sheria ya Usalama wa Taifa Tanzania.

Sasa naomba leo tuchambue vifungu vingine ambavyo vina utata vikichwa vipite kama vilivyo itakuwa hatari kwa nchi. Mswada unasema, Kufuatia mabadiliko ya jumla yanayoweka usimamizi wa Idara chini ya Rais, inapendekezwa vifungu vya 11, 15, 18, 19(3) virekebishwe ili kuondoa mamlaka ya usimamizi wa Waziri wa Mambo ya Nje, Katibu Mkuu Kiongozi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika masuala mbalimbali yanayohusu usimamizi wa intelijensia na usalama.

Marekebisho haya ni hatari, Afrika na dunia ya leo y utandawazi ukimwacha mtu mmoja aamue na kudhibiti Sekta nyeti kama ya Ujasusi pekee yake ni hatari kwake binafsi na ni hatari kwa taifa. Hii ni room inayoweza kuipa TISS kumpindua Rais, hasa ikizingatiwa kuna kifungu cha 16 kinachoficha utambulisho wa Afisa wa TISS. Pili, afisa huyu ana kinga ya kisheria ya kutoshitakiwa kijinai kwamjibu wa kifungu cha 19 cha mswada huuhuu. Huu ni mtego mbaya kwa nafasi ya Rais, Vyombo hivi vinaongozwa na watu ambao wanatoka katika jamii zetu hizihizi na wanahisia hizihizi za kutaka madaraka. Sasa Rais anabebeshwa pekee yake uamuzi na udhibiti wa ida, ni hatari, iko siku tutapata Rais ambae sio Samia, atatumia meno haya kuangamiza taifa.

Mapendekezo yangu, vifungu vya 11, 15, 18, 19(3) virekebishwe Mamlaka yote ya TISS yawe chini ya Rais, lakini atasaidiwa/atashauriwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Waziri wa Katiba na Sheria na Waziri wa Mashauri ya Kigeni. Kwasababu ya hoja zifuatazo, Mswada huu haujawa katika mtazamo wa kiuchumi kama tulivyokuwa tukishauri, badala yake mabadiliko yanalenga udola zaidi. Hivyo Waziri wa Fedha na Mipango ataingia katika usimamizi wa Idara kama sehemu ya Sera mpa ya TISS ya kuongoza njia za uchumi wa nchi katika mtandao wa kifedha na uwekezaji, Ikizingatiwa tayari kuna kitengo cha Ujasusi wa kiuchumi kilichoundwa mwaka juzi pale Bank, Miradi ya uwekezaji wa ndani na nje yote ikiwemo sera ya uwekezaji na fedha viwe chini ya Waziri kwa mwamvuli wa TISS.

Waziri wa Sheria na Katiba anaingia kwaajili ya usimamizi wa sheria na katiba wakati wote wa uendeshaji na Oparesheni za TISS, atakuwa pia mshauri wa Rais katika mambo ya sheria na katiba. Waziri wa Mambo ya nje anaingia kwaajili ya maswala yote ya kijasusi nje ya mipaka ya nchi, na hasa katika diplomasia ya kimataifa na uwekezaji wa kigeni.

Hapo vifungu hivi vya mamlaka ya usimamizi wa TISS chini ya Rais vitakuwa vimetumia. NB: huko nyuma Mawaziri tajwa waliokuwa wanatambuliwa na sheria iliyopo walikuwa wapo kama kivuli tu, Kila kitu cha TISS iliamliwa na Rais, hata mswada huu umesema wazi kuwa wanarasmisha ule utaratibu wa awali ambao haukuwa rasmi. Kama Rais anamchagua Waziri Mkuu kwakushauriana na Makamu wa Rais, iweje jambo nyeti kama TISS Rais anapewa mamlaka ya pekee yake? Tukatae hili kwa nguvu zote!

Sehemu nyingine yenye utata ambayo inahitaji ifanyiwe marekebisho ya laazima ni kifungu cha 19 cha Mswaada huu kinachotoa kinga ya kijinai kwa maafisa wote wanapofanya uhalifu wawapo kazini. Hiki kifungu kina hatari nyingi sana, Lakini kuwa zaidi kina hatari kwa Umma, madhara ya utekaji wa raia na mauaji ya raia kwa miaka mitano iliyopita shutuma zote zilielekezwa kwa Idara ya Usalama wa Taifa kupitia genge lililoitwa watu wasiojulikana. Uhatari wa pili unahusu Mamlaka ya Rais kuwa hatarini ikiwa taasisi nzima maafisa wote wana kinga ya kijinai inatoa room ya kumpindua Rais kwa mwamvuli wa kinga hii. Ninafahamu, Mswada huu wa sheria ya Usalama wa Taifa ulianza kutungwa kipindi cha Magufuli 2019, nilidokezwa, Ulitungwa kwakuangalia mazingira ya wakati ule, na ulilenga dhana ya umagufulication, Rais Samia kaja kufanya maboresho kidogo tu, Rais Samia stuka, unabebeshwa dude hatari kwa usalama wako na wa nchi kwa ujumla. Rekebisheni

Duniani kote maafisa na wakuu wa idara nyeti kama ya Ujasusi huwa hawapewi kinga hata chembe, ili iwe rahisi kuwadhibiti kisheria pale wanapovuka mipaka yao ya kazi. Ndio maana unaweza kuona Mkurugenzi wa CIA au Mosad anafika mbele ya mahakamu kujibu tuhuma kadhaa zilizotokea katika utendaji wao. Ni juzi tu maafisa wa shirika la Ujasusi la Urusi walifikishwa katika mahakama moja mjini Moscow kwa makosa kadhaa ya usaliti katika vita huko Ukraine.

Mapendekezo yangu, Kinga kwa maofisa wa TISS iondolewe, badala yake kingi iwekwe kwenye kazi/Oparesheni na taarifa tu. Afisa kama mtu ashitakiwe tu kwamjibu wa taratibu za kijeshi kwakuwa tayari sheria kifungu cha kwanza kabisa kimeitambua TISS kama jeshi hivyo utaratibu wa kinidhamu wa Mahakama za kijeshi utumike kama kawaida.

Ikiwa kuna ulazima ambapo Kimsingi unajionyesha ni wa kisiasa zaidi kama ule aliopewa Spika, Jaji Mkuu nk, Basi kinga apewe Miurugenzi wa Usalama pekee na sio maafisa wote katika idara.

Kwa leo tuishie vifungu hivi... Tutaendelea wakati ujao

Na Yericko Nyerere
 
Mhe Yeriko naomba nami niweke tofauli langu kwenye hili jambo la kuwekeana KINGA,

Kwa kurejea Jurisprudence ya Common Laws, Commonwealth precedents, Mkataba wa Haki za Binadamu wa 1948 na Katiba ya Tanzania ibara ya 13 kila mtu anahesabiwa hana HATIA hadi hapo Mahakama itakapothibitisha kinyume chake (preumption of innocence), kwa msingi huu sasa kitendo cha kuweka kinga/immunity ya kutokushitakiwa kwa watendaji wa idara au ofisi yeyote ni kwenda kinyume na mikataba ya Kimataifa, kinyume kabisa cha maamuzi ya Mahakama za Juu Precedents nk

Kwa mfano, ukimwekea Kinga Ofisa ili asihojiwe au asishitakiwe popote maana yake, ile presumption of innocence inakuwa haina maana tena na anaweza hata kutenda makosa makubwa ya kuigharimu Nchi huku akijua kuwa kamwe hawezi kushitakiwa, Ikitokea Military mutiny kama majaribio yaliyofeli kama ya 1963 au 1983/7 halafu hao watu wamepewa KINGA ya kutokushitakiwa itakuwaje?

Pili, kitendo cha kumwekea mtu immunity against prosecution kinaondoa Uwajibikaji-accountability na badala yake huzalisha upendeleo, inefficiency, lack of result based outputs na hatimaye ni anarchy au chaos. Wafalme walioitawala ULAYA hadi karne ya 17 wote walikuwa na immunity na haikuwezekana kuwashitaki kwa jambo lolote hadi ilipotokea Mapinduzi ya mfalme wa Uingereza -Glorious revolution of 1658 na mapinduzi ya Ufaransa ya 1789-Napoleon Bonapatre Revolution ambayo yote yalisababishwa na kukosekaa kwa accountability kwenye uendeshaji wa Nchi na matumizi ya KODI.

USA ilipata Uhuru wake kutoka UK mwaka 1776 baada ya BUnge la UK kupitisha sheria ya kutoza Kodi kwa masettlers wa US waliokuwa na mashamba makubwa ambapo jamaa walisema No Taxation without Representation, ndipo mwanzo wa REPUBLIC yente nguvu huku duniani iliyoleta maboresho makubwa kwenye doctrine of SEPARATION OF POWERS. Hii yote ilikuwa ni namna ya kuleta uwajibikaji na kuuondoa mambo ya Kinga kinga kwa wafalme. Mwaka 2023 Rais wa US alishitakiwa kwa makosa ya JINAI,

Mei 2023 aliyekuwa Waziri Mkuu wa Afaghastan Imran Kann alishamatwa na kupelekwa MAHAKAMANI na kwa Makosa ya Rushwa aliyoyatenda akiwa PM ,

Aliyekuwa Rais wa Brazil Lula Da Silva ambaye aliyeshinda uchaguzi juzi juzi, alishitakiwa baada ya kumaliza muda wake wa Urais na akapatikana na hatia, akatumikia adhabu yake na akaja kugombea.
Rais msaafu wa USA Donald Trump badoa ana Kesi za Jinai kwenye mahakama za New york kwa makosa aliyoyatenda kiwa Rais,

Kwa msingi huo huo wa falsafa ya SHERIA, itakuwa ni kurudi na Nyuma kama Nchi yetu ambayo ni mwanachama wa Commonwealth, inayotumia Precedents za mahakama mbali mbali kuendelea kuweka kinga kwa watendaji wa serikali wakati kuna HOJA za kuuondoa Kinga kwa Rais kwenye Katiba ili kuongeza uwajibikaji na matumizi ya Ofisi za umma.

Kwa hiyo nikiwa miongoni mwa Watanzania wachache wenye ufaulu mzuri kwenye Somo la Constitutional Law and Legal Systems of East Africa, natofautiana na hoja hii ya kuwawekea watumishi wa Umma kinga, ni muhimu kutokuweka kinga ili kila mtu awajibike kwa matendo yake binafsi aliyotenda kinyume na maslahi ya Umma, itakuwa ni makosa kurudi nyuma miaka ya 1658, 1789,Huu ni wakati wa kwenda mbele sio kurudi nyuma.
Fīat jūstitia ruat cælum ="Let justice be done though the heavens fall."
The maxim signifies the belief that justice must be realized regardless of consequences.
 
YERIKO NYERERE tumeshakuzoea siku zote ww hunaga jema lolote linalofanyika kwenye hili taifa hutafuta dosari Ili uonekane una akili nyingi kuliko wenzako.

Binafsi NAUNGA MKONO MAPENDEKEZO YOTE yaliyoletwa na TISS juu ya mabadiliko nyie wapinga Kila kitu tumewachoka.

Huu mswaada naamin haujaandaliwa na mtu MMOJA Leo hii ww Mmoja na naamin hao watu waliouandaa wameona mbali acha tuwape muda siyo Kuwapinga Pinga tu.

Harafu KUPINGA Huwa ni rahisi kuliko kuanzisha hoja ya kupingwa.
 
MAKOSA MAKUBWA YA MSWADA WA TISS.

SEHEMU YA 2.

Baada ya kuona makosa ya vifungu vya 5 na 16 namna vinavyopingana, na mapendekezo niliyoweka ili kuboresha mswada huu wa sheria ya Usalama wa Taifa Tanzania.

Sasa naomba leo tuchambue vifungu vingine ambavyo vina utata vikichwa vipite kama vilivyo itakuwa hatari kwa nchi. Mswada unasema, Kufuatia mabadiliko ya jumla yanayoweka usimamizi wa Idara chini ya Rais, inapendekezwa vifungu vya 11, 15, 18, 19(3) virekebishwe ili kuondoa mamlaka ya usimamizi wa Waziri wa Mambo ya Nje, Katibu Mkuu Kiongozi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika masuala mbalimbali yanayohusu usimamizi wa intelijensia na usalama.

Marekebisho haya ni hatari, Afrika na dunia ya leo y utandawazi ukimwacha mtu mmoja aamue na kudhibiti Sekta nyeti kama ya Ujasusi pekee yake ni hatari kwake binafsi na ni hatari kwa taifa. Hii ni room inayoweza kuipa TISS kumpindua Rais, hasa ikizingatiwa kuna kifungu cha 16 kinachoficha utambulisho wa Afisa wa TISS. Pili, afisa huyu ana kinga ya kisheria ya kutoshitakiwa kijinai kwamjibu wa kifungu cha 19 cha mswada huuhuu. Huu ni mtego mbaya kwa nafasi ya Rais, Vyombo hivi vinaongozwa na watu ambao wanatoka katika jamii zetu hizihizi na wanahisia hizihizi za kutaka madaraka. Sasa Rais anabebeshwa pekee yake uamuzi na udhibiti wa ida, ni hatari, iko siku tutapata Rais ambae sio Samia, atatumia meno haya kuangamiza taifa.

Mapendekezo yangu, vifungu vya 11, 15, 18, 19(3) virekebishwe Mamlaka yote ya TISS yawe chini ya Rais, lakini atasaidiwa/atashauriwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Waziri wa Katiba na Sheria na Waziri wa Mashauri ya Kigeni. Kwasababu ya hoja zifuatazo, Mswada huu haujawa katika mtazamo wa kiuchumi kama tulivyokuwa tukishauri, badala yake mabadiliko yanalenga udola zaidi. Hivyo Waziri wa Fedha na Mipango ataingia katika usimamizi wa Idara kama sehemu ya Sera mpa ya TISS ya kuongoza njia za uchumi wa nchi katika mtandao wa kifedha na uwekezaji, Ikizingatiwa tayari kuna kitengo cha Ujasusi wa kiuchumi kilichoundwa mwaka juzi pale Bank, Miradi ya uwekezaji wa ndani na nje yote ikiwemo sera ya uwekezaji na fedha viwe chini ya Waziri kwa mwamvuli wa TISS.

Waziri wa Sheria na Katiba anaingia kwaajili ya usimamizi wa sheria na katiba wakati wote wa uendeshaji na Oparesheni za TISS, atakuwa pia mshauri wa Rais katika mambo ya sheria na katiba. Waziri wa Mambo ya nje anaingia kwaajili ya maswala yote ya kijasusi nje ya mipaka ya nchi, na hasa katika diplomasia ya kimataifa na uwekezaji wa kigeni.

Hapo vifungu hivi vya mamlaka ya usimamizi wa TISS chini ya Rais vitakuwa vimetumia. NB: huko nyuma Mawaziri tajwa waliokuwa wanatambuliwa na sheria iliyopo walikuwa wapo kama kivuli tu, Kila kitu cha TISS iliamliwa na Rais, hata mswada huu umesema wazi kuwa wanarasmisha ule utaratibu wa awali ambao haukuwa rasmi. Kama Rais anamchagua Waziri Mkuu kwakushauriana na Makamu wa Rais, iweje jambo nyeti kama TISS Rais anapewa mamlaka ya pekee yake? Tukatae hili kwa nguvu zote!

Sehemu nyingine yenye utata ambayo inahitaji ifanyiwe marekebisho ya laazima ni kifungu cha 19 cha Mswaada huu kinachotoa kinga ya kijinai kwa maafisa wote wanapofanya uhalifu wawapo kazini. Hiki kifungu kina hatari nyingi sana, Lakini kuwa zaidi kina hatari kwa Umma, madhara ya utekaji wa raia na mauaji ya raia kwa miaka mitano iliyopita shutuma zote zilielekezwa kwa Idara ya Usalama wa Taifa kupitia genge lililoitwa watu wasiojulikana. Uhatari wa pili unahusu Mamlaka ya Rais kuwa hatarini ikiwa taasisi nzima maafisa wote wana kinga ya kijina inatoa room ya kumpindua Rais kwa mwamvuli wa kinga hii.

Mswada = Muswada. Halafu Tanzania tuna Wizara ya Mambo ya Nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki. Hiyo Wizara ya mashauri ya kigeni ni yako binafsi.
 
Jamaa unakuaga kama fyatu hivi, wewe ndio ulikuwa unasifia kweli haya mabadiliko, baada ya kuona wengi wanayaponda ndio umegeuka
 
Vipi yale mabadliko ya Ujasusi wa kiuchumi na kidola yamo?
 
Uhatari wa pili unahusu Mamlaka ya Rais kuwa hatarini ikiwa taasisi nzima maafisa wote wana kinga ya kijina inatoa room ya kumpindua Rais kwa mwamvuli wa kinga hii.
Hii hapana, katika kupindua wanakula kiapo cha utii lkn wanapindua. Hivyo kupindua rais itakuja hata wakiwa hawana kinga maana kupindiua kuna MOTIVE KUBWA NDANI YA MIOYO YA WATU na si viapo au KINGA AU nini sijui
 
YERIKO NYERERE tumeshakuzoea siku zote ww hunaga jema lolote linalofanyika kwenye hili taifa hutafuta dosari Ili uonekane una akili nyingi kuliko wenzako.

Binafsi NAUNGA MKONO MAPENDEKEZO YOTE yaliyoletwa na TISS juu ya mabadiliko nyie wapinga Kila kitu tumewachoka.

Huu mswaada naamin haujaandaliwa na mtu MMOJA Leo hii ww Mmoja na naamin hao watu waliouandaa wameona mbali acha tuwape muda siyo Kuwapinga Pinga tu.

Harafu KUPINGA Huwa ni rahisi kuliko kuanzisha hoja ya kupingwa.
Hutaki hata kushughulisha fuvu lako ndugu umekomaza na mapambio tu?
 
Una akili ndogo sana kama funza, Wapi na lini nilisifu muswada huu?

Mabadiliko tunayoyapigania ya idara ya usalama sio haya ya kujipa kinga
Elewa kwanza hiyo Kinga inatumika katika mazingira Gani.

Ndio maana nikaandika omba consultation kwanza.
 
Mhe Yeriko naomba nami niweke tofauli langu kwenye hili jambo la kuwekeana KINGA,

Kwa kurejea Jurisprudence ya Common Laws, Commonwealth precedents, Mkataba wa Haki za Binadamu wa 1948 na Katiba ya Tanzania ibara ya 13 kila mtu anahesabiwa hana HATIA hadi hapo Mahakama itakapothibitisha kinyume chake (preumption of innocence), kwa msingi huu sasa kitendo cha kuweka kinga/immunity ya kutokushitakiwa kwa watendaji wa idara au ofisi yeyote ni kwenda kinyume na mikataba ya Kimataifa, kinyume kabisa cha maamuzi ya Mahakama za Juu Precedents nk

Kwa mfano, ukimwekea Kinga Ofisa ili asihojiwe au asishitakiwe popote maana yake, ile presumption of innocence inakuwa haina maana tena na anaweza hata kutenda makosa makubwa ya kuigharimu Nchi huku akijua kuwa kamwe hawezi kushitakiwa, Ikitokea Military mutiny kama majaribio yaliyofeli kama ya 1963 au 1983/7 halafu hao watu wamepewa KINGA ya kutokushitakiwa itakuwaje?

Pili, kitendo cha kumwekea mtu immunity against prosecution kinaondoa Uwajibikaji-accountability na badala yake huzalisha upendeleo, inefficiency, lack of result based outputs na hatimaye ni anarchy au chaos. Wafalme walioitawala ULAYA hadi karne ya 17 wote walikuwa na immunity na haikuwezekana kuwashitaki kwa jambo lolote hadi ilipotokea Mapinduzi ya mfalme wa Uingereza -Glorious revolution of 1658 na mapinduzi ya Ufaransa ya 1789-Napoleon Bonapatre Revolution ambayo yote yalisababishwa na kukosekaa kwa accountability kwenye uendeshaji wa Nchi na matumizi ya KODI.

USA ilipata Uhuru wake kutoka UK mwaka 1776 baada ya BUnge la UK kupitisha sheria ya kutoza Kodi kwa masettlers wa US waliokuwa na mashamba makubwa ambapo jamaa walisema No Taxation without Representation, ndipo mwanzo wa REPUBLIC yente nguvu huku duniani iliyoleta maboresho makubwa kwenye doctrine of SEPARATION OF POWERS. Hii yote ilikuwa ni namna ya kuleta uwajibikaji na kuuondoa mambo ya Kinga kinga kwa wafalme. Mwaka 2023 Rais wa US alishitakiwa kwa makosa ya JINAI,

Mei 2023 aliyekuwa Waziri Mkuu wa Afaghastan Imran Kann alishamatwa na kupelekwa MAHAKAMANI na kwa Makosa ya Rushwa aliyoyatenda akiwa PM ,

Aliyekuwa Rais wa Brazil Lula Da Silva ambaye aliyeshinda uchaguzi juzi juzi, alishitakiwa baada ya kumaliza muda wake wa Urais na akapatikana na hatia, akatumikia adhabu yake na akaja kugombea.
Rais msaafu wa USA Donald Trump badoa ana Kesi za Jinai kwenye mahakama za New york kwa makosa aliyoyatenda kiwa Rais,

Kwa msingi huo huo wa falsafa ya SHERIA, itakuwa ni kurudi na Nyuma kama Nchi yetu ambayo ni mwanachama wa Commonwealth, inayotumia Precedents za mahakama mbali mbali kuendelea kuweka kinga kwa watendaji wa serikali wakati kuna HOJA za kuuondoa Kinga kwa Rais kwenye Katiba ili kuongeza uwajibikaji na matumizi ya Ofisi za umma.

Kwa hiyo nikiwa miongoni mwa Watanzania wachache wenye ufaulu mzuri kwenye Somo la Constitutional Law and Legal Systems of East Africa, natofautiana na hoja hii ya kuwawekea watumishi wa Umma kinga, ni muhimu kutokuweka kinga ili kila mtu awajibike kwa matendo yake binafsi aliyotenda kinyume na maslahi ya Umma, itakuwa ni makosa kurudi nyuma miaka ya 1658, 1789,Huu ni wakati wa kwenda mbele sio kurudi nyuma.
Fīat jūstitia ruat cælum ="Let justice be done though the heavens fall."
The maxim signifies the belief that justice must be realized regardless of consequences.
Asante Mkuu
 
Back
Top Bottom