Nimeamua kuoa baa medi

Ina maana baamedi sio mwanamke?Ungekua umepata mmoja kati ya hao unaowaponda ungekuj kutuambia hapa?
 
Acha unyanyasaji. Baamedi ni sawa na wanawakd wengine, ana tabia sawa na wanawake wengine. Ana uwezo sawa na wanawake wengine.

Napenda tu kukushauri uwe makini unapoamua kumchagua. Usimchague kutokana na kazi yake. Usije ukarudi jamvini tena na kuanza kulia.
 
Omba Mungu akupe mke mzuri, mambo ya kazi gani anafanya hayana maana sana. Kazi ni kazi tu alimradi ni ya halali.
 
Mkuu isijekuwa ni wewe uliyevuta BAAMEDI, unataka kutushawishi na sisi tufuate mkumbo!
Acha bana Tunamshukuru Mola, wakwetu wametulia.
 
Ishu sio mtu anafanya shughuli gani (baamedi...mwalimu..n.k) ila ni tabia binafsi na vile alivyo ndivyo vinavyomfanya awe mke mzuri au mbaya.
Unaweza na wewe ukafuata mkumbo na kuchagua shughuli ya mtu badala ya mtu uturudie hapa ukilia!!

Omba Mungu ufanikiwe mwanamke atakaekufaa kama mke na rafiki bila kujali shughuli anayofanya!!
well said!
 
ni mwanamke kama wanawake wengine mengine ni tabia ya mtu binafsi kila la heri

Safi chauro. Lakini tafiti zinaonesha kuwa hawa wana nidhamu na huwa wanatulia sana katika ndoa tofauti na masistaduu ambao huwa wanapenda maisha ya juu hata kama hawana uwezo wa kufikia huko.
 
Kama umeamua kuoa mfanyakazi wa baa fanya hivyo wewe kama wewe.Sio eti kwa sababu fulani nae alifanya hivyo.Kwa kukusaida tu ni kwamba,mtu kufanya kazi baa sio kipimo cha uhovyo ama umalaya ama kutumika sana SI KWELI!Endelea na mchakato mkuu.Kama bahati iko upande wako basi utapata mke bora kabisa.
 
Back
Top Bottom