Nimeamua kuoa baa medi

Nilifikiri tuko wachache tuliooa maeneo hayo, kumbe tuko wengi tu. Karibu Kiritimba, nyama ni ile ile ila mapishi ndio yanaweza kupishana kidogo.
 
Huyo nae pia ni mwanamke kama sisi,kama pengine anaweza kua na uelewa na uvumilivu kuliko wengine, kuuza baa niajira kama ajira nyengine sema akizidisha mambo mengine hapo ndio inakua mbaya,sasa kama unaona anafaa kila la kheir mwenyezi mungu akujalie kheir msikilizane mpendane na mpate watoto wema.....
 
Na hapo na yeye ana kazi..pengine mshahara mkubwa kuliko wewe. Pesa yake huioni hata siku moja. Hadi wazazi wake unawahudumia wewe.

Pesa yote inaenda kwenye vipodozi na kuvaa na kujiremba kila kinguo anachokiona anataka awe nacho, hawa watu bwana kazi kweli kweli
 
Endelea kufanya ziara mkuu.Ipo siku utaambulia wa kwako pengine yuko Twiga queens anapiga kabumbu au yu uwanja wa fisi.Mke popote bana.Waliosoma hawaoleki wanapenda mashindano.
 
Si unaona sasa!
Kwa mwanamke ambaye alikua mhudumu wa baa...ukimuoa halafu kila mwezi unampa laki 2 kama matumizi ya nyumbani, nakwambia itatosha na chenji inabaki. Mwaka wa kwanza mnanunua kiwanja, mwaka wa pili kupanga baaasi.

Uzuri wa hawa huwa wanakuwa na mapenzi ya dhati akisema anakupenda ni kweli anakupenda kwa dhati.
 
Wazo lako zuri sana, si baa medi tu ukitaka kuishi maisha mazuri ya ndoa mpe zari unayemuoa iwe ni surprise ya maisha ambayo hakutegemea kuishi kabisa, na tabia yake kama ni nzuri kidogo umelamba bingo sio kupalamia mwanamke mnaoana tu mnaanza kuchanga matumizi ndani ataona wapi tofauti yako wewe na yeye. hapo dharau mwanzo wisho.
 
Mkuu unamaanisha nilitakiwa kuwa provider wa kila kitu hata kama na yeye ana kazi!?
 
Barmaid ni mwanamke kama wanawake wengine, na hiyo ni kazi kama kazi nyingine. Leo unaweza kumkuta anafanya kazi ya bar kesho ukamkuta yuko saloon, au anauza duka. Sio vizuri kuwachukulia wafanya kazi wa bar kama watu wa hali ya chini katika maisha. Aidha, wengine wanafanya kazi hiyo wakati wakitafuta kazi nyingine kama ambavyo watu wengine wanabadilisha kazi. Kama ungekuwa unafikiria kuoa changudoa, ningekushuri uache kwa sababu yule tayari ameishingia kwenye kazi ambayo haina maadili.

Mkuu kama umpenda, wewe vuta kitu weka ndani ufurahie maisha. Nina mifano ambao wameoa kama hivyo uanvyofikiria wanakaa raha mstarehe. Ila uwe makini, sio siku manahitilafiana unaanza........ooo kwanza wewe unanitsha nini,.....umesaha nilikokutoa.........
 
Asante sana.
Watu wengi huwa wanawadharau sana watu hawa, lakini mimi nina experience nzuri sana ya viumbe hawa. Ni tofauti na watu wanavyofikiria.
 
Ishu sio mtu anafanya shughuli gani (baamedi...mwalimu..n.k) ila ni tabia binafsi na vile alivyo ndivyo vinavyomfanya awe mke mzuri au mbaya.
big up lizzy
 
Wanaume wengi wa sasa wanaangalia kazi na usomi wa mwanamke, ametoka katika familia gani n.k unakuta mtu ukikutana nae baada ya salamu tu anaanza unafanya kazi wapi kha! ndio mkome mke mwema anatoka kwa Mungu haijalishi anafanya kazi, msomi au hafanyi kazi unaweza ukamuoa na kumfungulia hata biashara ya genge kwa kuanzia na baadae mambo yakawa mazuri tu
 
Back
Top Bottom