Nimeamua kumpuuza Tundu Lisu

Nimeamua kumpuuza Tundu Lisu

Status
Not open for further replies.
Tuanze kwa AMANI..

Bwana huyu ameshazoea kuwa kituko "A laughing doll" kwa watu hivyo mara nyingi anapotoa kauli zake "hafikirii" uthabiti na matokeo ya kauli hizo.

Hivi karibuni katika mahojiano yake ktk vyombo vya habari amenukuliwa akimkashifu Mhe Rais, Dkt John Pombe Magufuli kuwa ni mtu anayefanya kazi zake kwa kutaka "headlines" kwenye vyombo vya habari..

Lakini hakuishia hapo, akaeleza kuwa Mhe Magufuli ni mtu asiyefuata Sheria na kanuni za Utawala bora..akitaja kuwa hatua zinazochukuliwa "kusafisha" Serikali na Wezi Serikali ni kinyume na Sheria.

Ni Mpuuzi pekee, anayeweza kusema kuwa kufukuza wezi, wala Rushwa na wahujumu uchumi waliotengeneza mitandao ya wizi serikalini ni Kwenda kinyume na utawala bora...na kisha akadai kuwa CHAMA CHAKE, kinaendelea na mapambano dhidi ya rushwa na wezi Serikalini.

Sioni haya, wala sitaomba radhi, nitasema hili popote pale na SITAFUTA KAULI kuwa kwa upofu wa fikra alionao Mhe TUNDU ktk hili yeye ni JIPU miongoni mwa majipu yanayosumbua nchi hii.

Kwa kuwa mimi siungi mkono na nimejitenga mbali na UPUUZI nasimama kumkemea TUNDU kama vile Injili ya Bwana inavyoelekeza wema kukemea UOVU.

Nawatakia Ijumaa njema.

Wenu.

JULIANA.
Hao chadema hawana aibu tangu watuambie msafi waliyemsema ni fisadi niliwaona watu wa ovyo sana
 
Lissu ni mgonjwa wangu-Kigwangalla.
 
Inawezekana haujaijua "..DOLA.." hakuna mwanadamu katika ulimwengu huu aliye chini ya dola yeyote akaitetemesha dola hiyo...unless otherwise Dola iamue kumpuuza. chezea kila kitu katika maisha lakini usijaribu kuchezea Dola. Wapo waliojaribu, ebu fanya ulizio.

At least nina address kama Mbunge, ila sioni wewe unaongea kama nani..? Kapuku mmoja anayetumia ID fake JF unataka kuninyooshea kidole...unaanzaje..?
Ubunge upi? Huo wa ganda la ndizi? Kweli binadamu wana akili za ajabu Mno!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom