Nimeamua kumpuuza Tundu Lisu

Nimeamua kumpuuza Tundu Lisu

Status
Not open for further replies.
Ni vyema ukajifunza kutofautisha siasa chafu na kusema KWELI. Mpuuzi sio tusi bali ni sifa ila ni sifa mbaya ambayo mtu mzima aliyetimia sawasawa kichwani hapaswi kuwa nayo.

Nikieleza kuwa Lissu ni mpuuzi, simtukani bali naelezea moja ya sifa zake kubwa anayojitanabaisha nayo kwa watu.

Kwani ukiacha hizo personal attack umeambiwa ndiyo mwisho wa kibarua chako CCM? Kwa utu uzima ulio nao ina maana hukuwahi kujifunza hekima ama kupima matamshi yako kwa kuzingatia kujulikana kwako kijamii?
 
(Hii ni thread yangu niliyoileta hapa JF tarehe 15 January 2016, kwa bahati mbaya sana mods wakaiondoa...sikutaarifiwa juu ya sababu zao za kufanya hivyo ila naamini yeyote aliyefanya hivyo aliteleza kibinadamu kama inavyotokea kwa wengine. Nimeileta tena leo hili niwajaze maarifa wanajamvi )

TUNDU ANTIPAS LISSU - Mpuuzi niliyeamua kumpuuza.

Tuanze kwa AMANI..

Bwana huyu ameshazoea kuwa kituko "A laughing doll" kwa watu hivyo mara nyingi anapotoa kauli zake "hafikirii" uthabiti na matokeo ya kauli hizo.

Hivi karibuni katika mahojiano yake ktk vyombo vya habari amenukuliwa akimkashifu Mhe Rais, Dkt John Pombe Magufuli kuwa ni mtu anayefanya kazi zake kwa kutaka "headlines" kwenye vyombo vya habari..

Lakini hakuishia hapo, akaeleza kuwa Mhe Magufuli ni mtu asiyefuata Sheria na kanuni za Utawala bora..akitaja kuwa hatua zinazochukuliwa "kusafisha" Serikali na Wezi Serikali ni kinyume na Sheria.

Ni Mpuuzi pekee, anayeweza kusema kuwa kufukuza wezi, wala Rushwa na wahujumu uchumi waliotengeneza mitandao ya wizi serikalini ni Kwenda kinyume na utawala bora...na kisha akadai kuwa CHAMA CHAKE, kinaendelea na mapambano dhidi ya rushwa na wezi Serikalini.

Sioni haya, wala sitaomba radhi, nitasema hili popote pale na SITAFUTA KAULI kuwa kwa ujinga na upofu wa fikra alionao Mhe TUNDU ktk hili yeye ni JIPU miongoni mwa majipu yanayosumbua nchi hii.

Kwa kuwa mimi siungi mkono na nimejitenga mbali na UPUUZI nasimama kumkemea TUNDU kama vile Injili ya Bwana inavyoelekeza wema kukemea UOVU.

Nawatakia Ijumaa njema.

Wenu.

JULIANA.

Hata wewe ni mpuuzi ambaye umeacha shughuli zako huko ccm kutwa kucha unazungumzia Chadema na viongozi wake. Tunakudharau sana.
 
eti magufuli anapambana na ufisadi,ufisadi upi??? mafisadi wakubwa nchi hii wa kwanza ni Mka.pa na Ki.kwetesasa fisadi gani ambao anapambano nao
 
Only if mods wasingeliuondoa uzi huu kwa mara ya kwanza nisingelilazimika kuandika tena leo hii. Nilimpuuza hapo mwanza na nampuuza hata sasa.
Nadhani neno Kupuuza halimaanishi Ignoring tena.Kwangu niliamini kupuuza ni kutojihusisha na mtu/kitu fulani kwa namna yeyote ile..Ningefurahi ungenipa tafsiri sahihi ya neno hili.Kubali tu "Kumpuuza" literally . Sometimes even a negative publicity can be a good publicity.
 
Lissu peke yake anatetemesha Dola ya Magufuli. Je, wangekuwa angalau watatu ingekuwaje. Eti mbunge wa 'Vitu Maalum' naye anaweza kumpuuza Lissu, maajabu!
Inawezekana haujaijua "..DOLA.." hakuna mwanadamu katika ulimwengu huu aliye chini ya dola yeyote akaitetemesha dola hiyo...unless otherwise Dola iamue kumpuuza. chezea kila kitu katika maisha lakini usijaribu kuchezea Dola. Wapo waliojaribu, ebu fanya ulizio.

At least nina address kama Mbunge, ila sioni wewe unaongea kama nani..? Kapuku mmoja anayetumia ID fake JF unataka kuninyooshea kidole...unaanzaje..?
 
La kwanza,
Natoa shukrani zangu kwa wananchi wa Songwe walionichagua kuwa mwakilishi wao bungeni.

La pili,
Siasa sio Ukigeugeu, leo useme Lowassa fisadi kesho useme ni mtetezi wa wanyonge. Ni wapuuzi pekee ndio wanaweza kufanya siasa za ukigeugeu
Sijui kama una kumbukumbu ulipokuwa CDM ulikuwa unasema nini juu ya CCM.
Na ulipohamia CCM sasa unasema nini juu ya CDM. Wanasiasa ni vigeugeu.
 
Ni vyema ukajifunza kutofautisha siasa chafu na kusema KWELI. Mpuuzi sio tusi bali ni sifa ila ni sifa mbaya ambayo mtu mzima aliyetimia sawasawa kichwani hapaswi kuwa nayo.

Nikieleza kuwa Lissu ni mpuuzi, simtukani bali naelezea moja ya sifa zake kubwa anayojitanabaisha nayo kwa watu.

Na mimi hapo juu nimesema ukweli kwa kuelezea sifa za wanasiasa(hasa walio madarakani) kwa kufanya siasa chafu...Hawataki kfuata utaratibu walioapa kuulinda na kuusimamia ,wanaongoza kwa utashi wao..

Waliosaidiwa kuingia madarakani wamegeuka wapiga zumari kwa kupaka rangi mapambio yanayo imbwa na wakubwa wao bila ya kujali ni sahihi au la...Tuache unafiki hapa...

Nchi imejaa vigeugeu mpaka tumekwama ,hatu hubiriwi tena Tanzania ya viwanda ..Hatuna vipaumbele leo mnashika hili kesho mnashika jengine..

Maajabu ya Elimu bure ,na sasa tunachangishwa kwa lazima pesa ya kununulia madawati..Miaka 50 kipaumbele cha Elimu ni madawati...
 
Hivi na wewe ni mmoja ya watunga sheria wa nchi hii? Andiko hili linasaidia vipi watu wa Songwe? Matatizo yenu yanasababishwa na Lissu?
 
kama umeshapata viti maalumu unahangaika nini tena au unataka unaibu waziri? huna reasoning ya maana ni kujikomba au kuonesha unalipa hisani? Tanzania kwa wanasiasa wa aina yako tuna long way to go!
 
Nadhani neno Kupuuza halimaanishi Ignoring tena.Kwangu niliamini kupuuza ni kutojihusisha na mtu/kitu fulani kwa namna yeyote ile..Ningefurahi ungenipa tafsiri sahihi ya neno hili.Kubali tu "Kumpuuza" literally . Sometimes even a negative publicity can be a good publicity.

Halafu ni msomi wa level ya Phd
 
Watu wanaotumia muda mwingi kuweweseka bila kujali kukaa chini na kutathmini matumizi ya pesa wanazopewa na Wafadhili wao km zimetumika halali ama la eti nao wanataka dola. Nidhamu ya matumizi ya fedha tu hamna vipi kuendesha dola. Kwa nini Dadayetu mpendwa asiungane na Mkapa kuona tatizo walilonalo wa upande huo na kuwapa ushauri wa bureeee? Tumieni muda hata kidogo kutathmini mwenendo wa pande zenu.
 
La kwanza,
Natoa shukrani zangu kwa wananchi wa Songwe walionichagua kuwa mwakilishi wao bungeni.

La pili,
Siasa sio Ukigeugeu, leo useme Lowassa fisadi kesho useme ni mtetezi wa wanyonge. Ni wapuuzi pekee ndio wanaweza kufanya siasa za ukigeugeu

Juliana,
Should we learn anything from you? if yes...what is it
 
Ni vyema ukajifunza kutofautisha siasa chafu na kusema KWELI. Mpuuzi sio tusi bali ni sifa ila ni sifa mbaya ambayo mtu mzima aliyetimia sawasawa kichwani hapaswi kuwa nayo.

Nikieleza kuwa Lissu ni mpuuzi, simtukani bali naelezea moja ya sifa zake kubwa anayojitanabaisha nayo kwa watu.
Umesema umechaguliwa na watu wa Jimbo gani hivi? Ni usemi kuwa ukikuta mahali anayetawala ana chongo basi amini wanaotawaliwa ni vipofu.
 
(Hii ni thread yangu niliyoileta hapa JF tarehe 15 January 2016, kwa bahati mbaya sana mods wakaiondoa...sikutaarifiwa juu ya sababu zao za kufanya hivyo ila naamini yeyote aliyefanya hivyo aliteleza kibinadamu kama inavyotokea kwa wengine. Nimeileta tena leo hili niwajaze maarifa wanajamvi )

TUNDU ANTIPAS LISSU - Mpuuzi niliyeamua kumpuuza.

Tuanze kwa AMANI..

Bwana huyu ameshazoea kuwa kituko "A laughing doll" kwa watu hivyo mara nyingi anapotoa kauli zake "hafikirii" uthabiti na matokeo ya kauli hizo.

Hivi karibuni katika mahojiano yake ktk vyombo vya habari amenukuliwa akimkashifu Mhe Rais, Dkt John Pombe Magufuli kuwa ni mtu anayefanya kazi zake kwa kutaka "headlines" kwenye vyombo vya habari..

Lakini hakuishia hapo, akaeleza kuwa Mhe Magufuli ni mtu asiyefuata Sheria na kanuni za Utawala bora..akitaja kuwa hatua zinazochukuliwa "kusafisha" Serikali na Wezi Serikali ni kinyume na Sheria.

Ni Mpuuzi pekee, anayeweza kusema kuwa kufukuza wezi, wala Rushwa na wahujumu uchumi waliotengeneza mitandao ya wizi serikalini ni Kwenda kinyume na utawala bora...na kisha akadai kuwa CHAMA CHAKE, kinaendelea na mapambano dhidi ya rushwa na wezi Serikalini.

Sioni haya, wala sitaomba radhi, nitasema hili popote pale na SITAFUTA KAULI kuwa kwa ujinga na upofu wa fikra alionao Mhe TUNDU ktk hili yeye ni JIPU miongoni mwa majipu yanayosumbua nchi hii.

Kwa kuwa mimi siungi mkono na nimejitenga mbali na UPUUZI nasimama kumkemea TUNDU kama vile Injili ya Bwana inavyoelekeza wema kukemea UOVU.

Nawatakia Ijumaa njema.

Wenu.

JULIANA.
Aliyepuuzwa hatajwi tajwi wala kuzungumziwa!!

Umempuuza MTU then unamuanzishia Uzi?

Unatia kinyaa sana wewe!!
 
Tokea amsafishe Lowasa, hatuna imani nae tena.

Lisu ni mkuu Wa wanafiki Tanzania
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom