Nimeamua Kulima kwa mara ya Pili kilimo cha mahindi

Wafungue mipaka ya Soko la nje, hali imeshatengamaa itakuwa ni hasara kwa wakulima na wafanyabiashara wa Kitanzania.
 
Kama utakua tayari kuniuzia mahindi na majani yake yakifikisha miezi 3niko tayari kununua wa heka Mimi nayavuna na kusaga kwa ajili ya Chakula cha ngombe huna haja ya kusubiri miezi 6mpaka yakauke Mimi nahitaji yakiwa mabichi kwa ajili ya silage
 
Mkuu nitakuja PM tuone kama tuwaweza kufanya biashara. Mana nami ni mkulima wa mahindi pia.

Kama utakua tayari kuniuzia mahindi na majani yake yakifikisha miezi 3niko tayari kununua wa heka Mimi nayavuna na kusaga kwa ajili ya Chakula cha ngombe huna haja ya kusubiri miezi 6mpaka yakauke Mimi nahitaji yakiwa mabichi kwa ajili ya silage
Kama utakua tayari kuniuzia mahindi na majani yake yakifikisha miezi 3niko tayari kununua wa heka Mimi nayavuna na kusaga kwa ajili ya Chakula cha ngombe huna haja ya kusubiri miezi 6mpaka yakauke Mimi nahitaji yakiwa mabichi kwa ajili ya silage
 
Nachokushauri ndugu yangu usiwe sana optimistic hasa kwenye masuala ya bei.. mfano kwa sasa gunia ni 35,000/= tena na japo serikali imeruhusu mahindi kuuzwa nje lakini bado wakenya wamegoma kununua yetu wananunua ya Zambia.. ila hoepful by March next year things will be different and maize demand itakuwa kubwa tofauti na sasa.

Yangu nimeamua kuhifadhi tu kwa dawa nisubiri.. Siku zote wanasema "Farming looks mighty easy when your plow is a pencil and you're a thousand miles from the corn field." hizo hesabu utaona mamilioni kwenye daftari hapo, ila in real life situation ujiandae kisaikolojia hasa kwa hiki kilimo chetu cha kutegemea mvua.

Ningekushauri fanya hivi;
1. Uzuri unalima turiani hapo, na shamba lako ni kubwa.. Nenda pale Tanfeed International kwa Profesa Kekule, huwa kiwanda chake cha kusaga chakula cha kuku anatumia yale mahindi ya njano.. na mara ya mwisho kuongea nae alisema ananunua kilo moja si chini ya shilingi 600.. This was last year when i met him.. sasa unaweza kuingia mkataba nae angalau ukawa na uhakika na soko kabla hata ya kuingia shambani.. si lazma ulime mahindi yote ya njano lakini at least you have that assurance.

2. Kama wewe si mtaalamu wa kilimo basi hapo halmashauri kuna mabwana shamba wamekalia tu mabenchi, nenda onana na crops officer akupe mtaalamu ambae atakuwa consultant wako..uzuri wa kutumia mtaalamu wa eneo husika ni kwamba wamekaa hapo wanaielewa ardhi vizuri, mbolea zipi zinarespond vizuri, mbegu gani nzuri, visumbufu gani vya mazao hasa wadudu na magonjwa na general agronomic practice utakayokupa matokeo chanya kwa kuwa kila agro ecological zone zinatofautiana.. Kwa hiiyo uwe na mtu wako mmoja wa kukupa ushauri.. hata kama una utaalamu, fanya hivyo utajikuta unajifunza kitu.. usiogope vigharama vidogo vidogo kama nauli yake, posho au tips..you are investing and you dont wanna take any risks..Make use of these experts. Pia uzuri mwingine ukimtumia mtaalamu yeye atajivunia kuwa ana mkulima wake wa mfano anaemsimamia, so pia ni credit kwake na hii inaweza kufungua hata opportunities nyingine kwako zinazokuja kwenye idara ya kilimo wilayani kwa ajili ya wakulima wa hayo maeneo.

3. Ni vizuri ukafanya diversification.. wanasema a farmer can not put all his eggs in one basket, kwa hiyo uamue may be kufanya mono cropping au intercropping, na kama utaamua ni mahindi tu usipande mbegu ya aina moja.. In case ya shida yoyote na kwa uwekezaji mkubwa hivyo unaweza kupoteza kila kitu ukajikuta unatembea ukiongea mwenyewe barabarani. kwa hiyo diversify, pia unaweza kutupia mikunde katikati au any other crop ambayo in the process itakuondolea weeds pressure na kurutubisha udongo wako

4. Tafuta njia za kukusaidia kufanya operations mbalimbali kwa wepesi.. mfano kwenye palizi unaweza kutumia herbicides, kuliko kutegemea watu, . hii itasaidia kukuwezesha kumaliza mapema kwani ili kupata tija, hutakiwi mazao yako yawe na visumbufu kama wadudu na magugu..ukitegemea watu hadi wamalize itachukua muda sana na mtasumbuana sana

5. Mwisho MUHIMU WEWE MWENYEWE KUWEPO SHAMBANI WAKATI WA HATUA MUHIMU. MFANO KUPANDA, KUWEKA MBOLEA, NA KUVUNA. USIJE UKAWAAMINI WATU UKATEGEMEA SIMU.. Kanunue mbegu uhakikishe imeishia shambani, mbolea hakikisha imewekwa yote kwa vipimo sahihi kuvuna pia usipoenda unapigwa. Angalau palizi unaweza kurelax kidogo mradi utaenda kukagua. Watu hasa vibarua hawaaminiki kabisa hasa kwa hizo hatua nilizokuambia

Nimeamua kushare experience yangu, i hope utaokota mawili matatu yatakayokusaidia.. Goodluck na usisahau kutupa mrejesho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…