Nimeamua kuachana na siasa rasmi. CHADEMA walinihatarishia ajira yangu ya umma ila leo wameunga juhudi

Kweli mkuu. Wakiambiwa wasiogope, wamwage damu, hawajitokezi. Chama kitaendeleaje na kutawala
Wengi ni mashabiki maandazi hawajapitia madhila ya kwenda jela kisa chama, mdee na bulaya walivunjwa Hadi mikono then wanapata nafasi mashabiki wanawaambia wasiende eti bungeni, halafu chama kikikosa ruzuku hawatachangia au kikipotea miongoni mwa watanzania watakuja kulaumu. Siasa za awamu hii Bora kuwa smart kuzifanya kulingana na mtawala
 
Nyie humu mnabomoana mnatukanana
Mnanuniana wenzenu wanaunga mkono juhudi
Hebu tuishi tujuavyo tuachane na hawa Wanasiasa teh teh teh

Ova
 
Njaa ni kitu kibaya sana kwa wanasiasa wa kiafrika, chama kama chama kimekuwa na msimamo kuwa hao wabunge hakiwatambui, ila ni wao tu, ndio njaa zao, na hata chama kiwafute uanachama kwa siasa za sasa haitakuwa na maana kwani bado serikali itaendelea kuwatambua tu! Siasa za ki afrika ni ngumu sana!
Lakini wananchi tutakuwa tumejua ukweli kuwa hizo ni njama za Ndugai
 
Baada ya kukosa nafasi ya kupiga kura 28/10/2020 niliumia sana kutomchagua mpinzani Mhe. Tundu Lissu.

Ila kwa yaliyotokea leo nadhani hata ule uchungu umeisha woteee.

1. Viti maaalumu wamepewa.
2. Tundu yupo Ubelgiji anakula soseji.
3. Maalimu Seif soon atakubali kuwa makamu wa raisi.

Kwahili naomba nijivue.

Yaliyotokea kwa Lowassa nilijipa moyo na kumuona msaliti nikaendelea kukomaa na CHADEMA.

Nilihatarisha utumishi wangu wa umma mara mbili kisa CHADEMA.

Ila kwa yaliyotokea leo DUUH SIASA BASI.

Muda wangu bora nipoteze kushabikia Liverpool na Yanga.
Na bila kusahau kutafuta hela.

Nimekuwa mwanachama wa CHADEMA tokea 2010 ila kwa mliyofanya leo CHADEMA duh

I'm DONE.

#YNWA
That makes the two of us, mimi nimekua mwanachama wa Chadema tokea mwaka 2009.
 
Back
Top Bottom