Nimeamini Tigo wizi

Miunda

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
530
182
Jana nimeweka 10,000 ili ninunue 10 gb Internet. Cha kushangaza baada ya kujiunga nikapata ujumbe salio halitoshi, nikajaribu kutaka kujua kiasi gani kimebaki *102*01# naambiwa sina salio.

Suali najiuliza zimeenda wapi? Akili yangu ikanijibu kuwa labda ni kosa la mtandao, pengine tayari ninayo 10GB.

Baada ya sekunde chache nikapata ujumbe kuwa nishatumia 500sh. Nikasema hata shilingi hizi ziko wapi? Nikiangalia salio naambiwa sina.

Nikawasiliana na customer service, nikaambiwa 10Gb Nnazo na nishatumia kadhaa, sawa, baada ya muda naona Sipati huduma ya Internet, nikapiga simu tena kuomba msaada, nikawa fahamisha customer service, Mara akaikata simu, nikapiga kwa mara ya tatu, dada muongeaji nilipo jaribu kumwomba kutaka kujua salio langu, akaanza kunipangia muda na sekunde nilio tumia shilingi 10,000.

Nikamwambia ataa sikubaliani, kwa sababu kila Time naangalia salio naambiwa Sina, na nilipo jiunga Nimeambiwa salio halitoshi, zilikwenda wapi? Inamaanisha kuwa salio nilikuwa nalo ila mulitumia laghai nisiweze kuona zikatike kama umeme in 45 minutes?

Hakutaka tena kuni saidia kurudishiwa salio langu na kutaka mie niende tawi la Tigo, wakati ni usiku.

Huu ndio wizi wa Tigo wamekataa kunipatia haki yangu
 
Kwa kuongezea customer service ameniambia nimejiunga na hadithi Sijui nilikatwa 150 shilingi, wakati sikujiunga kabisa, pia hata SMS sikupata za kukatwa huko
 
Pole aisee. Hata mimi nimeachana na huo mtandao kwa mambo kama hayo.
Nilikuwa nime sign mkataba ambao naweka 30000/= kwa mwezi napata muda wa maongezi dakika 33kwa siku kwa mwezi mzima ambao najua siumalizi kwa huo mwezi kwa matumizi yangu ninavyoyajua. Nimefanya hivo kwa kama mwaka mzima hivi. Kuanzia November last year zikawa zinaisha kabla ya wiki. Nikiangalia salio hawanioneshi. Nikaenda pale makumbusho yule officer akaandika email kwa hao sijui ndio technical department au watu gani..!? Lakini sikupata suluhisho wala ufafanuzi wa kinachoendelea. Nishachoka nao. Hapa ninaendelea kuiweka online kwasababu najua naweza kutafutwa kwa line hiyo na baadhi ya watu. Lakini natumia mtandao mwingine kabisa.
 
Nedna ofisini kwao upate maelezo mazuri,pole sana mkuu
Office ni wanatoa maelezo tu, hawana msaada wowote wa kukusaidia zaidi watakuambia tutatuma email, Hizo gharama za kufika ofisini na kurudi sio ndogo, nilio wasiliana nao ndio wa kunipatia uvumbuzi kwa sababu wanaona kila kitu kwenye system.

Nilicho gundua kuwa customer service hawana uwezo wa kutoa huduma, nimetembea nchi mbalimbali, na huko kwa wenzetu Unapo kuwa na tatizo kama hili, customer service muda huo huo huwasiliana na manager, ndani ya dakika 10 unapewa maamuzi ambayo kama mteja unaridhika.
 
Nimenunua bundle la internet la 2,000/= then la 1,000/= kwa tigo pesa, ela yangu wakachukua na bundle sikupewa. Nikiwapigia wananiambia tunashughulikia subiri, siku ya 3 hii hamna kitu, ndio washaniibia hapo, wizi mtupu
 
Back
Top Bottom