Tetesi: Nimeamini Mhe. Mbowe sasa amekwama

Egnecious

JF-Expert Member
Jul 8, 2015
875
960
NIMEAMINI MHE. MBOWE SASA AMEKWAMA.
21 Sept.

Nimesikitishwa sana kumuona kiongozi wa chama kikuu cha upinzani Freeman Mbowe akilalama kuiponda serikali na kuilaumu kufuatia ajali ya MV Nyerere.

Niwe mkweli sikutarajia kuona Mbowe amefikia hatua hii. Sikutarajia kuona Mbowe ameamua kuwa mwanasiasa anayeokoteza hoja na kubwabwaja uongo kwa kiwango hiki.

Juzi kaitisha mkutano na waandishi wa habari kaongea uongo mtupu kuhusu uchaguzi mdogo uliofanyika tarehe 16 Sept, 2018. Jana Mkurugenzi wa Uchaguzi Dk. Kihamia amemjibu na kumtaka aombe radhi kwa uongo alioutangaza ndani ya siku saba ama sivyo athibitishe madai yake.

Leo kaibuka tena na uongo na uchochezi kuhusu ajali ya Mv Nyerere iliyopinduka na kuzama ziwa Victoria. Najua atakapotakiwa kuthibitisha uongo wake atapiga chaka tena kama alivyopiga chaka kuhusu uongo wake juu ya uchaguzi mdogo wa majuzi.

Watanzania wapo kwenye majonzi, hii ni ajali imechukua roho za ndugu zetu, hapa sio mahali pa kufanyia siasa. Tena siasa zenyewe za kusema uongo.

Ukisikia kufilisika kisiasa ndio huku, kiongozi mkuu unaacha kujenga hoja za haja, unapiga porojo za uongo halafu watu makini kwenye chama chako wakiamua kuhama chama unasema wananunuliwa. Mtu mwenye akili timamu hawezi kukaa mahali panaomdhalilisha na panaomharibia sifa na dhamira yake kwa Taifa. Mahali palipojaa usanii.

Kwanza, Mbowe anasema Mbunge wa Ukerewe aliwahi kutahadharisha kuhusu ubovu wa MV Ukerewe lakini Serikali ilipuuzia ndio maana kumetokea ajali. SIO KWELI HATA KIDOGO. Hata kabla ya Mbunge wa Ukerewe hajasema Bungeni Serikali ya awamu ya tano ilishaanza mchakato wa kukarabati kivuko hicho na ilikuwa tayari imetenga fedha za kukikarabati. Katikati ya Mwezi Julai 2018 ukarabati ulikamilika kwa gharama ya shilingi milioni 191 zilizohusisha ununuzi wa injini mbili na maboresho mengine. Sote tuliona kwenye vyombo vya habari wananchi wa kisiwa cha Ukara wakishangilia na kuishukuru Serikali kwa kukitengeneza kivuko hicho ambacho baada ya ukarabati kilikuwa na uwezo wa kusafiri kwa dakika 45 kati ya Ukara na Bugorora tofauti na awali kilipokuwa kinatumia masaa 2 hadi 3. Mbowe kadanganya.

Pili, Mbowe anasema serikali haitilii maanani usalama wa majini. Ni muongo wa kupigiwa mfano, Serikali imefanya juhudi kubwa kununua boti za doria na kuongeza uwezo wa jeshi la zimamoti na uokoaji kwa ajili ya kuimarisha shughuli za uokoaji na waliopo katika maziwa wanaona kilichofanyika kupitia majeshi yetu.

Niliposikia maneno haya ya Mbowe harakaharaka nikaangalia bajeti ya Zimamoto na uokoaji ambayo imepitishwa katika Bunge la Bajeti lililopita ambalo Mbowe aliwaambia Wabunge wake wasusie na kutoka nje. Nikaona baada ya ukame wa miaka mingi kwa mara ya kwanza serikali ya awamu ya tano imetoa fedha nyingi kiasi cha shilingi Bilioni 5 za kununulia magari ya zimamoto na uokoaji, imetoa shilingi milioni 500 kwa ajili ya kununulia vifaa vya uokoaji majini na inatarajia kupata mkopo nafuu kutoka Austria wa Euro milioni 5 sawa na zaidi ya shilingi bilioni 14.5 kwa ajili ya kupata vifaa zaidi na vya kisasa vya uokoaji.

Sasa kwa maoni yangu serikali ya awamu ya tano imeonesha dhahiri sio tu nia ya kuimarisha usalama wa majini bali pia kuimarisha usafiri wenyewe.

Mbowe ameshasahau kuwa ni juzi tu Rais Magufuli amezindua ujenzi wa meli mpya katika ziwa Victoria. Amesahau kuwa Serikali ya Awamu ya Tano tayari imekarabati meli 5 kati ya meli zote 14 zilizokuwa zimesimama kutoa huduma kutokana na ubovu kwa miaka mingi tena nyingine zimesimama tangu miaka 10 iliyopita.

Mbowe amesahau kuwa Serikali ya Awamu ya Tano ya Rais Magufuli imekamilisha ujenzi wa MV Njombe na MV Ruvuma katika ziwa Nyasa ambazo sasa zimeleta suluhisho na usalama wa usafiri kwa wananchi. Inasikitisha sana.

Tatu, hoja zingine za Mbowe mniwie radhi zinaonekana za kipuuzi kabisa, eti anaponda kwa nini salamu za Rais zimetolewa na Msigwa. Yaani kajitoa ufahamu kuwa Msigwa ni Msemaji wa Rais na anachosema ndicho alichosema Rais.

Halafu anasahau kwamba Rais Magufuli sio level yake, maana namuona anasema CHADEMA inamtaka Rais Magufuli atangaze maombolezo ya Kitaifa. Tangu lini Serikali ikafanya kazi kwa maelekezo ya CHADEMA?

Mbowe kaendelea kuokoteza hoja, mara hooo kusitisha zoezi kwa sababu ya giza ilikuwa ni makosa, yeye Mbowe anajua kilichokuwa kinatokea eneo la tukio? Anataka kusema watu wote waliokuwa wakiendelea na uokoaji pale hawana akili isipokuwa yeye aliyekuwa Dar es Salaam kwenye mkutano wa waandishi wa habari?

Halafu ajali za kuzama vivuko ama meli zimetokea Tanzania tu? Huko kwingine zinakotokea watu huwa hawapotezi maisha? Upuuzi mtupu.

Mbowe anadai kila mwezi kuna watu 20 hadi 30 wanakufa kwa kuzama majini kapata wapi takwimu hizi, nani kathibitisha vifo hivyo. Yaani wafe watu 20 hadi 30 nchini halafu ajue Mbowe tu? Hata Rais awe hajui wala vyombo vya habari havijui wala wananchi waliopo maeneo ya usafiri wa maji hawajui?

Au ndio ule ule utamaduni wa Mbowe na genge lake wa kuwatangazia Watanzania kuwa watu wameua kwa mamia na miili inaokotwa kwenye ufukwe wa bahari lakini akiulizwa mamia waliofiwa wapo wapi hakuna anachoonesha, usanii mtupu.

Mbowe anataka viongozi wawajibike kwa matukio haya ya ajali. Mimi ningemuelewa zaidi kama yeye angeonesha mfano wa kuwajibika kuendesha siasa zisizo na tija na ambazo zinasababisha watu kufa akiwemo Akwelina Akwilini, Daudi Mwangosi, Chacha Wangwe na juzi tu msadizi wake.

Ningeelewa zaidi kama Mbowe angeonesha mfano wa kuwajibika kwa kuachia madaraka ya uenyekiti kutokana na anguko la chama chake linalotokana na kuhama kwa wabunge, madiwani na maelfu ya wanachama. Lengo si kuonesha umewajibika kama kiongozi mwenye dhamana? Aanze yeye ili tujue kuwa anaongoza kwa mifano.

Kwa kweli namshangaa sana Mbowe na kwa mwendo huu anatengeneza anguko lake kubwa sana kisiasa. Na kwa kuwa amekikumbatia chama chake cha CHADEMA anguko hili halitakuwa la Mbowe pekee yake litakuwa anguko pia la chama chake.

Nawasihi Watanzania tuwe makini na siasa za kichochezi za watu wa aina ya Mbowe. Bahati nzuri serikali imekaa vizuri sana kuwadhibiti wanasiasa wachochezi akiwemo yeye Mbowe. Naanza kuwaamini wanaosema kuwa sasa hivi Mbowe anajitoa ufahamu ili kutafuta huruma ya wananchi hasa wakati huu ambapo anakabiliwa na kesi mbaya ambayo kwa tunaojua mwenendo wa kisheria pale hataweza kuchomoka, kifungo kinamhusu vizuri sana.

Ifike mahali Watanzania tuongee lugha moja na tuachane na propaganda za kutuchelewesha. Kama anavyosema Rais Magufuli tumechelewa mno, sasa imetosha tuchape kazi tujenge nchi yetu.

Mwisho natoa pole kwa wote waliofikwa na msiba wa kuondokewa na jamaa zao katika ajali ya Mv Nyerere, pole kwa majeruhi wote na nawaombea mpone haraka.

Siku njema

Bw. Mpoki Ambonisye
Uyole, Mbeya
 
Tuache siasa kwenye jambo hili.
Watu wamefiwa watu wanaomboleza.
Inauma sana.
Acheni masihara.
Naamini kabisa ndugu yako wa karibu angekuwa kafa kwenye hii ajali usiangendika hizi mambo humu.
Tuacheni tuomboleze. Siasa za kipuuzi tupa kule.
 
Pumba tupu

Kwanza mmiliki wa kivuko ni nani? Kingekuwa cha mtu binafsi sasa hivi unajua angekua wapi?

Pili usalama wa majini maana yake ni nini? Kazi za mamala za usafiri majini ni zipi? Ilikuaje ikaruhusu kivuko kinachopaswa kubeba watu 100 wapande watu 200+? Je uzembe wa nani?

Kununua injini mpya haifanya kivuko kuwa salama, je maboya yapo yalikuwepo ya kutosha?

Hakuna jinsi unaitoa hiyo lawama kwa serikali maana ndio mmiliki, ndio msimamizi wa usalama na ndio mwendesha kivuko.

Sijui uongo wa Mbowe upo wapi? Kuna wakati unapaswa kutafakari badala ya kutoa majimaji na mapovu kama mtu mwenye kifafa.
 
Mtoa hoja ulitaka kusema nini? Siku nyingine kama unataka kuonyesha uongo wa mtu, weka tu jedwali linaloonyesha uongo na unaweka na ukweli juu ya jambo unalolizungumzia. Lakini kwa uliyoyasema ni nafuu ya Mbowe kuliko wewe. Mbowe melalama ameeleweka lakini wewe umeropoka tena kwa maandishi! Chunga sana, maandishi haya yatadumu kukushuhudia.
 
kinachoniumiza zaidi ni pale viongozi wetu wanapotumia shida zetu kama platform ya kick kama wanashindwa kuwa hata sehemu ya utatuzi wa shida zetu basi wawe hata sehemu ya waombolezaji badala yake ni fursa kwao kuendelea kuwa mbele ya cameramen damn it! RIP nduguzangu #Damuyangu #MitaChacheTuKutokaUfukweni
Yule mtoto anaemsubiri baba yake amletee zawadi kutoka mnadani,mama anaesubiri mumewe amletee mboga kwa ajili ya chakula chausiku na yule baba anaemsubiri mkewe arudi nyumbani aandae mlo wa familia hataelewa ni nani hakutenda wajibu wake daah! watoto wa shule walioenda gulioni kufata daftari na peni kwa ajili ya shule jumatatu ndo mwisho wao hawataweza tena kuimaliza robo ya mwisho ya muhula wa mwaka..........
 
Pumba tupu

Kwanza mmiliki wa kivuko ni nani? Kingekuwa cha mtu binafsi sasa hivi unajua angekua wapi?

Pili usalama wa majini maana yake ni nini? Kazi za mamala za usafiri majini ni zipi? Ilikuaje ikaruhusu kivuko kinachopaswa kubeba watu 100 wapande watu 200+? Je uzembe wa nani?

Kununua injini mpya haifanya kivuko kuwa salama, je maboya yapo yalikuwepo ya kutosha?

Hakuna jinsi unaitoa hiyo lawama kwa serikali maana ndio mmiliki, ndio msimamizi wa usalama na ndio mwendesha kivuko.

Sijui uongo wa Mbowe upo wapi? Kuna wakati unapaswa kutafakari badala ya kutoa majimaji na mapovu kama mtu mwenye kifafa.
Nimepeda ulivyomjibu
 
Mkumbushe huyo msemaji wa selikari kuwa hadi mda anatoa taarifa watu zaidi ya mia walikuwa wamepatina wamekufa tayari.. sasa hizo taarifa za watu 75 waziri wake amezitoa wapi?? MBONA kama hakuna ukweli wa taarifa zake hadi kwenye Majanga.
Screenshot_2018-09-21-16-49-33.jpg
 
Mleta mada yupo sahihi kabisa ila tatizo vijana wa Leo wa Chadema hawana tena tafakuri ya mambo muhimu kwa Taifa letu.

Mbowe amechanganyikiwa kwa sasa anahitaji kuwa na washauri makini sana. Chama kinapukutika kwa kukosa kiongozi . Mbaya zaidi hana mtu anayeamini kuwa ataweza kuvaa viatu vyake vya kutumia chama kama Saccos yao binafsi.

Kwa hekima na busara na maarifa makubwa Mbowe alipaswa kutoa salam za Rambirambi na kutoa wito kwa Wanachama na viongozi wote wa Chama waliopo eneo la tukio kujitokeza kwa wingi na kusaidia kufanya kazi ya uokoaji kwa kushirikiana na watanzania wengine waliopo eneo hilo.

Suala la kulaumiana lingekua baadae huko Bungeni na sio sasa.
Kuna mambo hayafai kabisa kuyatumia kama kiki ya kisiasa.

Tena kwa busara zaidi angeweza kuwa wakwanza kufika kwenye eneo la tukio kutoa mawazo yake na kushauriana na mkuu wa mkoa ili kujenga imani na kuonyesha utu kwa vitendo.

Sasa Kiongozi mkuu tena dikteta kama Mbowe anapoanza kwa kutoa maneno ya lawama na kejeli basi linakua ni suala la wote walioko chini yake wataanza kutoa matamko na maneno ya kijinga hali itakayozidi kuwafanya waone kuwa anageuza msiba huu mkubwa kuwa suala lake la kujijenga kisiasa bila kujali maumivu na huzuni waliyo nayo wale waliopoteza ndugu zao.

Kidemokrasia Mbowe hastahili kuendelea kukalia kiti cha uongozi hata kwa dakika moja mbele. Hana hoja zaidi ya vioja.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom