Nimeambiwa nirithi mke wa kakaangu

Nimeambiwa nirithi mke wa kakaangu

Yaani umekuja kutafuta majibu kwa swali ambalo tayari umesha jijibu...
Sasa... kwani unataka sisi tukushauri nini akati, tayari umesha fanya maamuzi...
Mshauri mkuu, anaweza badili maamuzi.
Pia waweza mpa moyo juu ya maamuzi yake
 
Umeuliza kwetu vipi, sisi ilikuwepo lakini ilishakufa zamani. Kama mnapendana na huyo shemeji yako na mila zenu zinaruhusu basi rithi. Wawezakuta uliishaanza kumsaidia kakaako akiwa bado hao.
 
Kila la kheri kaka wasikuvunje moyo kama anatabia njema msimpoteze kwenye mikono salama ya familia kubwa hujalinzisha ww wazee wenyewe ndio wamekupa baraka endeleaa usisahau kutupa mrejesho
 
Habari wana jamvi,

Jana ilikuwa arobaini ya kaka yangu. Kaka alifariki kwa ajali. Kaacha mke na mtoto mwenye miezi 7 wakiume. Walioana mwaka jana.

Mimi ndie nilie mfata broh na ni wa mwisho. Tunatofautiana miaka 3.

Mimi bado sijaoa, na wala sina mchumba zaidi ya mademu ambao sina malengo nao.

Sasa katika kikao cha wazee leo asubuhi, ndio likaja hilo wazo kwamba binti huyu ana mtoto wa miezi 7, hana kazi atakwenda wapi na ataishi wapi? Na pia familia yetu ilimpenda sana na haiko tayari kuja kushuhudia kuolewa na mtu mwingine baki.

Baba ana nyumba mbili Dsm bado alikuwa ajatukabidhi, moja itakuja kuwa yangu, nyingine angepewa kaka, lkn ndo mauti yashamkuta.

Na kiukweli sisi wachaga hatupendi kupoteza mtoto. Ndipo wazee wakaniita na kuniuliza kama nina mchumba, nikawajibu hapana.

Wakanieleza kwa taratibu za mila na desturi za zamani hali kama hii ikitokea ina bidi mdogo mtu arithi jukumu la kaka ili gurudumu liende mbele.

Nilipokuwa namwazia shemeji angu ambae ni mke wa kaka angu jinsi alivyo poa na bado anaita, nikaona sio mbaya kupokezana vijiti.

Kiukweli mimi na shemeji yangu tulikuwa tunaheshimiana sana, kila mara alikuwa anauliza nitaoa lini. Alikuwa kama rafiki yangu, japo sikuwahi waza jambo kama hili laweza kuja tokea.

Wazee wameamua kuwatafuta wa mama wa makamo wamweleze shemeji jambo hili waone msimamo wake.

Kwa upande wangu sina tatizo kabisa, kwani kwa tabia yake, ukarimu, upendo kwa marehemu kaka, namuona ni mke mwema ambae naweza ishi nae.

Nasubiria kikao cha Akina mama na shemeji juu ya maamuzi yake.

Vipi wadau, kwa huko kwenu huu utaratibu upo?
Kwa wewe binafsi unaichukuliaje?
Mkuu kama yuko mswano we kula tu !Usisahau kutupa mrejesho
 
Kila la kheri kaka wasikuvunje moyo kama anatabia njema msimpoteze kwenye mikono salama ya familia kubwa hujalinzisha ww wazee wenyewe ndio wamekupa baraka endeleaa usisahau kutupa mrejesho
Sawa mkuu, ngoja nisubiri majibu yake
 
Umeamua uamuzi sahihi huyo mtoto ni damu yako,chukua usukani endesha gurudumu.
 
Back
Top Bottom