Nimeambiwa nirithi mke wa kakaangu

Nimeambiwa nirithi mke wa kakaangu

Kama umekubali Kwa moyo oa. Ila Mimi kupeleka mshedede alipokuwa anakula kaka yangu naona shida Sana. Kwanza naogopa
 
Bro ameisha tangulia mbele ya haki,mjane yupo huru kuolewa na yeyote,hata wewe,
Mkikubaliana na mlengwa,weka chombo ndani,Pima ngoma kwanza
 
Mbona kuna jamaa alikuwa anaishi na kaka yake hp town. alichukuliwa kijijin bdo mdogo akawa anauza duka la Kk ake bahat mby kaka ake kapata ajali kafa. jamaa mpk leo mke wa kaka ake ndio mkewe
 
Ok ni tabia yetu wachagga.....sawaaa......naomba mkapime mjue afya zenu......ila nilichogundua ulishamtamani shemeji yako hata kaka yako hajatangulia.....na kwa ukahaba wako ambao wasema ni wa siri.....huyo sio chaguo lako bali ni kuokota ndimu chini ya mti wa mwembe.....sababu watumia ndimu utachukua na kuitumia.....japo wajua mti wa ndimu uko kulya seri.....mtoto akikua usimfiche mwambie....
 
Umeuliza kwetu vipi, sisi ilikuwepo lakini ilishakufa zamani. Kama mnapendana na huyo shemeji yako na mila zenu zinaruhusu basi rithi. Wawezakuta uliishaanza kumsaidia kakaako akiwa bado hao.
kwani kuna mila za kiafrika haziruhusu kurithi
 
Habari wana jamvi,

Jana ilikuwa arobaini ya kaka yangu. Kaka alifariki kwa ajali. Kaacha mke na mtoto mwenye miezi 7 wakiume. Walioana mwaka jana.

Mimi ndie nilie mfata broh na ni wa mwisho. Tunatofautiana miaka 3.

Mimi bado sijaoa, na wala sina mchumba zaidi ya mademu ambao sina malengo nao.

Sasa katika kikao cha wazee leo asubuhi, ndio likaja hilo wazo kwamba binti huyu ana mtoto wa miezi 7, hana kazi atakwenda wapi na ataishi wapi? Na pia familia yetu ilimpenda sana na haiko tayari kuja kushuhudia kuolewa na mtu mwingine baki.

Baba ana nyumba mbili Dsm bado alikuwa ajatukabidhi, moja itakuja kuwa yangu, nyingine angepewa kaka, lkn ndo mauti yashamkuta.

Na kiukweli sisi wachaga hatupendi kupoteza mtoto. Ndipo wazee wakaniita na kuniuliza kama nina mchumba, nikawajibu hapana.

Wakanieleza kwa taratibu za mila na desturi za zamani hali kama hii ikitokea ina bidi mdogo mtu arithi jukumu la kaka ili gurudumu liende mbele.

Nilipokuwa namwazia shemeji angu ambae ni mke wa kaka angu jinsi alivyo poa na bado anaita, nikaona sio mbaya kupokezana vijiti.

Kiukweli mimi na shemeji yangu tulikuwa tunaheshimiana sana, kila mara alikuwa anauliza nitaoa lini. Alikuwa kama rafiki yangu, japo sikuwahi waza jambo kama hili laweza kuja tokea.

Wazee wameamua kuwatafuta wa mama wa makamo wamweleze shemeji jambo hili waone msimamo wake.

Kwa upande wangu sina tatizo kabisa, kwani kwa tabia yake, ukarimu, upendo kwa marehemu kaka, namuona ni mke mwema ambae naweza ishi nae.

Nasubiria kikao cha Akina mama na shemeji juu ya maamuzi yake.

Vipi wadau, kwa huko kwenu huu utaratibu upo?
Kwa wewe binafsi unaichukuliaje?
kubali hili wazo
 
Back
Top Bottom