Nimeachana na mke wangu

Daah usimwache mkeo kwa ishu ndogo kama hiyo hapo ukiangalia Mkeo ashawahi kuta sms au chochote kwenye simu yako ndio maana kila unapokua offline yeye anajua upo kwa huyo pisi mwingine ingawaje hawa viumbe hasa wakiwa na mimba wanataka ukaribu wa hali ya juu.

wewe ndio unatakiwa ubadili utaratibu wa kuwasiliana nae mara kwa mara kutokana na hali yake hizo ndio changamoto za ndoa jaribuni wote kujishusha hakuna kombe la NBC mbele yenu hayo ni maisha yenu mjue na maisha ya mtoto wenu watoto wanapenda sana kuwa kwenye familia ya baba na mama pana madini mengi wanapata ingawaje vijana wengi hizi changamoto hamtaki kupitia kwa kuwa unaweza kuishi bila yeye life haipo hivyo huyo ni Mkeo mpigie simu mkauamalize wanawake wengi karibu tabia zinafanana wanatofautiana majina tuu.

kwa hiyo usihangaike na mwingine kutegemea eti yeye ni afadhali anakua kaficha makucha yake baadae mkizoeana anayatoa inakua majuto ni mjukuu .
 
Kama hapo awali hakua na wivu uliopitiliza na maugomvi vumilia mpaka ajifungue ila kama ni tabia yake hiyo toka awali. Piga chini hata usiwaze mara mbili mbili
 
Mtu anagombana tu bila sababu?
Kwani umeoa kichaa?hapana
Basi tufahamishe umemfanyaje mkeo ama aje ajielezee hapa
 
Piga mashine Bob, pendelea kula Nyanya chungu mbichi saa Moja kabla ya show....au bamia mbichi kama utaweza na limau..... Utakuja nishukuru hapa. Hicho ni kiherehere kinamsumbua...na kinatokana na wewe kutomfikisha kileleni.

Sema nini jombaaa sio kesi... kama vipi we mwache wahuni tumshone tukuambukize mi yutiai sugu .....
Oyaa hii nchi watu wamevurugwa
 
nikabeba nguo zangu zote na sidhani kama nitarudi nyumbani tena. Nimeamua kuanzisha maisha mapya hukuhuku nilipoletwa kikazi, nimetafuta nyumba ya 'apartment', nimeichukua nakaa mwenyewe na nimeamua kumuachia kila kitu.
KOSA KUBWA SANA HILI UNAFANYA MKUU
 
baada ya hapo nafikiri ndiyo mengine yatafuta, kama ni talaka au vipi lakini mpaka sasa uamuzi ni kwamba kila mtu aangalie maisha yake.
KOSA LINGINE HILI, HAKUNA MSINGI WA TALAKA HAPO. KUGOMBANA SIO MSINGI WA TALAKA

wewe mwanetu unapotea nakwambia lazima sometimes tuambiane ukweli
 
Epuka kufanya maamuzi ukiwa na hasira wengi hujutia sana hilo

Tafuta watu wazima kama wazazi au viongozi wa kidini mkae na mkeo msuluhishe hilo tatizo achana na huyo dada mtu

Jaribu kuongea na wakuu wako kazini ikiwezekana wakupe likizo fupi waambie hali halisi kwamba lengo lako ni kunusuru ndoa yako.

Cha muhimu pambana kuinusuru ndoa yako. Huyo dogo atakayezaliwa anahitaji sana malezi na upendo wa baba na mama yake
 
Wakongwe tukiwa mbali na wake zetu,tukiona wanaleta visirani tunawapa wapa, genye sio mchezo.
 
Sikatai ups and downs zipo kwenye ndoa lakini baada ya kuwa mjamzito ugomvi umezidi kuliko kawaida
Basi kama ni hivyo unatakiwa upime, kama ugomvi wenu wakati hajabeba mimba ulikuwa wa kawaida badi mvumilie tu atarudi kwenye hali yake ya kawaida baada ya kujifungua!
 
Ni hali ya mimba ndo inayofanya awe hivyo mvumilie akijifungua atakuwa sawa kuna mimba zingine zinakujaga na makasiriko
 
Kijana kaa chini na watu wazima watakuelekeza haya mambo. Najua unapitia changamoto ambazo hujawahi kufikiri kukutana nazo. Enzi za zamani kuepusha haya mwanamke akipata ujauzito alikuwa anapelekwa kwa wazazi wake kuepusha shari kama hizi.

Ujauzito ni kipengele ndugu yangu kuwa mdogo na mvumilie mkeo katika shida aliyonayo. Ukisema unamwacha unakosea sana kwani kipindi hiki ndio ulitakiwa uonyeshe kujali sana na kuwa karibu nae

Tatizo wanaume hatuandaliwi katika maisha ya ndoa na changamoto zake. Siku ya kuona unatoa tu mahari na kwenda kuchukua mke imeisha hiyo. Hufundishwi jinsi ya kuishi na mwanamke, kuishi na mke mwenye ujauzito, hata mtoto akizaliwa hatujui tufanyeje. Mambo haya yalikuwa yanafundishwa jandoni

Mke huyo bado hamjaachana sema tu wewe na utoto wako umeamua kususa kitu ambacho kinadhalilisha sana uanaume wako kwa kumkimbia mke kipindi ambacho ni mjamzito na anataraji kukuletea kiumbe. Ni baba wa aina gani ndugu yangu

Nimesikitishwa sana na hii mada ila ndio hivyo tunafundishana kupitia ujinga wa wengine. Nachoweza ku-conlude ni kwamba Taifa lina watu wa ovyo sana
 
Wengi watasema ni hangover ya mimba lakini umewah jiuliza house girl akipata mimba huo mvurugiko mbona huwa haupo?

Mdogo wangu akipata mimba akiwa kwangu Wala sikugundua na alijitahidi kufichaa hakuna kuchagua chakula au kudeka kama hivyo, nikagundua kumbe wanafanyaga makusudi kupima upepo, kuanza hapo nikasema make wangu haji kuniletea hivyo vitimbwili, akijizima data inakula kwake
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom