Wakuu habari zenu.. mimi ni kijana tu wa makamo naombeni msaada wenu kwa hili maana ata sielewi nifanye nini ingali kuna msemo unasema "akienda mwache aende na akiludi muulize kasahau nini"
Nilikuwa kwenye Mahusiano na dada moja hiv wa mbeya (post zangu za nyuma rejea) alinipenda sana inshort tulipendana sana.
Sasa kipindi tupo kwenye Mahusiano naye alinipaga namba ya dada yake ambaye ni dada yake wa kwanza, basi huyo dada yake tulikuwa tunawasiliana kwa kunyata sana maana me ata cmjui ila yeye ananijua sababu mdogo mtu alimtumiaga picha zangu.
Baada ya kama miezi michache kupita huyo girl wangu akaniambia dada anakuja dar kutafuta kazi huku nikamuuliza atafikia wapi? Akasema atafikia kwake.. basi siku ilipofika dada kuja dar alibembeleza twende tukampokee ila sababu mimi mazoea na ndugu wa mtu wangu sipendagi kabisa so sikuenda.
Basi baada ya wiki moja hv girl wangu akaniomba niende nikamuone dada yake.. basi siku hiyo jioni nikaenda kumuona dada yake.. uh ni mtu mzima kidogo ila ana kamwili kadogo Sana.
Naomba nifupishe mambo.. sababu yapo mengi.. baada ya muda dada yake alianza kuniita beby wetu, mala honey n.k me nikajuaga masiala masiala.. siku akaniita nyumban kwa girl wangu ( girl anafanya kazi radio hvyo anaingia kipindi cha saa 1 usiku) basi akaanza kunieleza kuwa ananipenda cjui nn, full kumponda mdogo wake alivyokuwaga huko mbeya yaan hatari hatari.. kiukweli mimi nilikataa kabisa kwanza ni mtu mzima umbo alikunidanganya kabisa.
Nafupisha!! Baada ya mwezi mmoja kupita huku mm na dada huyo tukiwa atuna mawasiliano kabisa, siku moja girl aliniambia ingia WhatsApp dah ile kuingia nakutana na ujumbe mzito huo kuwa nimemtongoza dada yake sijui nimelala naye .. inshort ni mambo mengi sana (unajua kama kitu ujafanya kiukweli hauna presha kabisa) basi mm nikamjibu "Ok nenda kwa amani"
Sasa now wiki ya pili analudi kuomba msamaha kuwa alikulupuka tu, mala dada yake ni mtu mbaya sana (yaani imekuwa wanatupiana mipila wenyewe kwa wenyewe) bac yeye swali lake kubwa anasema why mimi nilijua kuwa dada yake ananitaka why nisimwambie?? Mimi nilimjibu hivi " ningekwambia ungemchukia dada yako kama ulivyonichukiaga mimi"
Naombeni ushauri mkuu niludiane naye au niachana naye maana maneno aliyoniambiaga kwenye WhatsApp ni hatari.. afu pia yeye na dada yake mpaka sasa awaongei kabisa