Kiongozi mkuu wa Upinzani ambaye pia ni Katibu mkuu wa CDM Dr Wilbrod Slaa amesema hekima yake ilizuia umwagaji mkubwa wa damu katika taifa hili.Akihutubia umati mkubwa wa watu huko Geita jana alisema baada ya wizi mkubwa wa kura zake za urais mwaka 2010 wananchi walimtaka atoe tamko ili waingie barabarani lakini alikataa katakata.
Dr Slaa aliyekuwa akishangiliwa kwa mayowe na umati huo alisema kwamba kuna watu hawakumuelewa alipokataa suala la kuingia barabarani.Lakini ukweli ni kwamba aliamini maisha ya watanzania ni bora kuliko urais alioporwa.
Dr Slaa amesema anataka Umoja na amani vizidi kutawala katika taifa hili ndio maana aliwatuliza wananchi ingawa kila mtu anajua jinsi matokeo ya kura za urais zilivyokuwa.
Dr Slaa yuko katika ziara kubwa ya kuimarisha uhai wa chama kanda ya ziwa.
SOURCE:TANZANIA DAIMA.