Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,813
- 11,991
Fuatilia yanayojiri kwenye Bunge la 12, Mkutano wa 11, Kikao cha 53 leo Juni 22, 2023
Mbunge wa Ukonga Mhe. Jerry Slaa amesema Serikali ipokee mawazo mazuri ya wananchi lakini isikubali kuyumbishwa na watu wasioitakia mema nchi yetu.
"Niiombe Serikali ikubali ushauri, isikilize wananchi lakini wakati mwingine isikubali kuyumbishwa na watu wenye nia zao za kuitaka nchi yetu isiendelee kiuchumi, ikubaliane na hoja za msingi za kuendeleza taifa letu, tuwe na uwekezaji na kushirikisha sekta Binafsi kwenye yale maeneo ambayo wenzetu wamebobea, tupate uwekezaji mzuri wa Bandari" amesema Jerry Slaa.
Jerry Slaa, Mbunge wa Ukonga (CCM)Mhe. Slaa ametamka maneno haya wakati akisisitiza umuhimu wa Serikali kushirikiana na Sekta binafsi katika kukuza maendeleo ya taifa huku akitolea mfano wa Hayati Benjamin Mkapa alivyokumbana na upinzani mkubwa wakati wa ubinafsishaji wa benki ya NMB, benki ambayo kwa sasa inajiendesha kwa faida kubwa.
Pia, amesisitiza hadi sasa Serikali haijasaini mikataba ya Utekelezaji uwekezaji wa Bandari Nchini, bali imeingia makubaliano ya awali (IGA), na mikataba ya utekelezaji itasainiwa baadae.
Stahiki za Jeshi la Magereza zitazamwe upya
Mbunge wa viti maalumu Esther Matiko amesema askari wa jeshi la Magereza wanafanya kazi wakiwa kwenye mazingira magumu.
Amedai kuwa kuna Askari Magereza wametumikia nchi kwa zaidi ya miaka 26 bila kupandishwa vyeo huku utaratibu ukidai kila baada ya miaka 3 wapandishwe vyeo.
Esther Matiko, Mbunge wa viti MaalumAskari hawa kwa muda mrefu wamekuwa pia wanadai madeni mengi bila kulipwa na mishahara yao ni tofauti na majeshi mengine. Ameiomba serikali kuwazama upya ili kuboresha maisha yao.
Kupanda kwa Gharama ya Vifaa vya Ujenzi
Mbunge wa viti Maalum, Mhe. Salome Makamba ameshangaa mapendekezo ya Serikali ya kuongeza kodi kwenye vifaa vya ujenzi na Simenti.
Salome Makamba, Mbunge wa viti MaalumAmesema suala hili kitapunguza kasi ya wananchi kujipatia makazi mazuri na inawaumiza watanzania.
Ni muhimu kwa Serikali kutafuta vyanzo vingine vya mapato ili wananchi wawe na uwezo wa kujenga na kuboresha makazi yao.
Unyanyasaji wa Kijinsia, Serikali ichukue hatua
Suala la ukeketaji na ndoa za utotoni limeibuka tena Bungeni ambapo Mbunge Dr. Thea Medard Ntara ameshangaa kwa nini Serikali imeshindwa kukomesha kabisa vitendo hivi na wakati mwingine inawaacha wahusika waendelee kutekeleza unyanyasaji huu.
Amehoji, kama Serikali ilikomesha masuala ya mauaji ya Albino inashindwa vipi kukomesha ukeketaji na ndoa za mabinti wadogo? Dr. Thea ameenda mbali zaidi kwa kubainisha kuwa pengine masuala haya hayapati nguvu kubwa ya serikali kwa kuwa yanahusu sana wanawake na sio wanaume.
Amemuomba Waziri wa fedha kutenga fedha kwa ajili ya ulinzi wa watoto ambao bado upo nyuma ili dawa kwa wanaume walawiti na wabakaji ipatikane, ikiwezekana kuwahasi.
Amehoji, "Mtoto wa miaka 12 anaolewa anakwenda kufanya nini huko? Mbona hakuna uchungu na mabinti... Wangekuwa wanakeketwa wanaume ukeketaji ungeisha..."
Mbunge wa Ukonga Mhe. Jerry Slaa amesema Serikali ipokee mawazo mazuri ya wananchi lakini isikubali kuyumbishwa na watu wasioitakia mema nchi yetu.
"Niiombe Serikali ikubali ushauri, isikilize wananchi lakini wakati mwingine isikubali kuyumbishwa na watu wenye nia zao za kuitaka nchi yetu isiendelee kiuchumi, ikubaliane na hoja za msingi za kuendeleza taifa letu, tuwe na uwekezaji na kushirikisha sekta Binafsi kwenye yale maeneo ambayo wenzetu wamebobea, tupate uwekezaji mzuri wa Bandari" amesema Jerry Slaa.
Jerry Slaa, Mbunge wa Ukonga (CCM)
Pia, amesisitiza hadi sasa Serikali haijasaini mikataba ya Utekelezaji uwekezaji wa Bandari Nchini, bali imeingia makubaliano ya awali (IGA), na mikataba ya utekelezaji itasainiwa baadae.
Stahiki za Jeshi la Magereza zitazamwe upya
Mbunge wa viti maalumu Esther Matiko amesema askari wa jeshi la Magereza wanafanya kazi wakiwa kwenye mazingira magumu.
Amedai kuwa kuna Askari Magereza wametumikia nchi kwa zaidi ya miaka 26 bila kupandishwa vyeo huku utaratibu ukidai kila baada ya miaka 3 wapandishwe vyeo.
Esther Matiko, Mbunge wa viti Maalum
Kupanda kwa Gharama ya Vifaa vya Ujenzi
Mbunge wa viti Maalum, Mhe. Salome Makamba ameshangaa mapendekezo ya Serikali ya kuongeza kodi kwenye vifaa vya ujenzi na Simenti.
Salome Makamba, Mbunge wa viti Maalum