Nilizalishwa na kudhalilishwa

Nilizalishwa na kudhalilishwa

Katika harakati za kutafuta mkate nilikutana na mwanaume ambaye hatimae akawa mzazi mwenzangu, tuliishi kipindi kirefu sana tukiwa kama mke na mume, mwisho wa siku jamaa akaamua kuachana na mimi kwa mbwembwe na udhalilishaji wa kimataifa,mabaya mengi sana alinizushia ili tu azma yake ya kutaka kuniacha kiholela ipate waungaji mkono, Kwa kiasi kikubwa alifanikiwa wengi walimuunga mkono, kejeli matusi vilikuwa vikipishana mitaani vikinisaka mimi ,na haikuwa mimi tu mpaka familia yangu iliunganishwa kwenye hiyo dhihaka, kilikuwa kipindi kigumu sana haijawahi kutokea, maradhi msongo wa mawazo viliandama kiasi kwamba niliichukua dunia, nilijuta kwanini nilizaliwa, wakati mwingine nilitamani nife niondokane na haya mateso, lakini nilikuwa nikimwangalia mwanangu naishia kulia, nawaza nikifa leo huyu kiumbe asiyekuwa na hatia nitamwacha katika mazingira gani? Mungu si James kadri siku zilivyokuwa zinasonga mbele nikawa naizoea hali ile, nikaikubali hali ile na niambiwe au nisikie nini sikuweza kuumia tena, mpaka naandika uzi huu nina amani na yaliyopita yamebaki simulizi tu wala hayaniumizi tena. Kilichonileta kwenu ni hiki -Mpuuzi yule ana kila dalili ya kutaka kujiletaleta kwangu, najua iko siku ataleta swaga zake za kiduwanzi, nimetafakari ikitokea nimjibu nini ili naye ayapate maumivu mara mia ya niliyoyapata mimi nimeshindwa, nisaidieni wana MMU.
Unawaza kulipa kisasi elewa unajiwekea miiba njia unayopita peku..! Why usimkaushie hujui saikolojia huyo mtendee mema mpende ila usimpe nafasi tena..! Siku Mungu anakupa mwenzako ataumia mno..!
 
Kumbuka ni mzazi mwenzio
Always ili mtoto awe vizuri kiafya na kiakili lazima awe nawazaz wote wawili
Nirahis zaid kumtunza mtoto wenu
Poa alafu kitu kingine wanaume wote ndo tulivyo so ni bola kovu moja kutoka kwake kuliko mabusu matamu toka kwa wengine ambao wataishia kukuf@nyia kama yeye
 
Kwa jinsi ulivyoandika huu "uzi" inaonekana wazi kabisa wewe bado unampenda sana huyo jamaa unayemwita "mpuuzi". Maandishi yako yanaonesha kuwa una hamu sana jamaa arudi kukuomba msamaha ili na wewe upate upenyo wa kulipiza kisasi, lakini ukweli ni kwamba jamaa akirudisha majeshi; utampokea kwa mikono miwili, kitu ambacho siyo kibaya.

Mimi ningekushauri kama atarudi na kukuomba msamaha, wewe msamehe tu. Ni bora kusamehe kuliko kulipiza kisasi. Ukimsamehe atajifunza zaidi kwa kuona aibu kwani nafsi yake itamsuta sana kuliko ukimlipiza kisasi.
Ni ushauri pia ila siwezi kuufanyia kazi, asante.
 
Vp kama jamaa nae kamtamani tu sio kwamba anarusisha majesh mazima

Unataka mtoto wa watu awekwe kovu la pili kubwa kuliko????

Hapa ishu ni kusamehe lakini sio kurudiana nae na kama akimsamehe asijichanganye kurudia urafiki nae....atajutaaaaaa

Nmesema msamaha maana wanasaikolojia wanasema msaha umnufaisha mtoaji kuliko alietenda kosa
 
Kumbuka ni mzazi mwenzio
Always ili mtoto awe vizuri kiafya na kiakili lazima awe nawazaz wote wawili
Nirahis zaid kumtunza mtoto wenu
Poa alafu kitu kingine wanaume wote ndo tulivyo so ni bola kovu moja kutoka kwake kuliko mabusu matamu toka kwa wengine ambao wataishia kukuf@nyia kama yeye
Oooooh,so yeye mwanamke ndo ajue hilo nadhan mwanaume angekua anatambua kua n mzaz mwenzie asingefanya alofanyaa,af kwel mtoto anatakiwa alelewe na wazaz wote but inapotokea issue kama hiz no way acha tu mama akomae nae huyo Baba alomshit hana mana hata unafanya tu kama alishatanguliaaa mbele au kupotea kusikojulikana then mengne mtoto akikua ataamua mwenyewe
 
Pole sana mkuu.

Tatizo lenu wakati mnaumizwa, mtasema maneno mengi ya kejeli kwa huyo aliyekuzalisha na kukutupa.
Ila ukianza kuishi na mwingine, hamchelewi kuchemsha kipolo cha ugali.

Akirudi tena kuomba msamaha utamfanyaje?
Nitamsikiliza endapo duniani tutabaki wawili kama ilivyokuwa kwa Adam na Hawa
 
Kisaikolojia ukimsikia mwanamke anasema "anamchukia sana mwanaume fulani basi fahamu kwamba moyoni mwake bado anampenda mwanaume huyo. Wanawake wengi wana udhaifu huo.

Kusamehe ni jambo bora sana, lakini ikiwa watarudiana itakuwa ni bora zaidi. Kumbuka tayari wana mtoto na itakuwa afya zaidi kama watarudiana na kukaa pamoja kama familia.
Mtoto isiwe kigezo,kwani ambao baba zao walifariki wakiwa wadogo wamelelewaje...sion umuhimu WA mtu ambaye hakuitambua thaman ya mzaz mwenzie wala kuthamin damu yake kwa kipnd hicho af Leo hii anamhitaj tenaa
 
Back
Top Bottom