Niliyoyaona siku ya leo Jumanne

Niliyoyaona siku ya leo Jumanne

Kwanza poleni na harakati za hapa na pale kwenye kutafuta riziki.

Kwa kawaida huwa nawahi sana kuamka asubuhi sana na mapema kwa ajili ya kwenda kuweka mwili sawa kwa kufanya mazoezi ya hapa na pale. Huwa nakimbia half marathon eneo ninaloishi sio mbali na uwanja wa taifa. Nakimbia na kurudi nyumbani baada ya hapo ratiba zingine zinaendelea kwa kuwa naishi peke angu kama bachela nina uhuru na muda mwingi wa kufanya vitu kwa wakati.

Ubachela una raha yake kwa mbaliii japokuwa naona umri unaelekea kuwa kwenye mahusiano ya kudumu yani kutafutaa mke sasa tuweze kuwa wawili maana bado sijaona faida ya kubadili wasichana mara kwa mara magonjwa yamekuwa mengi sana.

Leo wakati wa asubuhi niliamua kwenda mimi mwenyewe sokoni (Tandika-stereo) kununua vifaa na mahitaji kwa ajili ya matumizi ya nyumbani (chakula) huwa nikipata vijihela kidogo nanunua kwa jumla. Mabachela wenzangu wananielewa vzuri hapa. Sasa wakati nipo pale sokoni niliona vitu ambavyo dah nilipata surprise kidogo. Nilikutana na vijana wenye umri kama wangu kwa makadirio yetu wengi wetu ambao tumehitimu elimu ngazi ya degree 1(bachelor) lkn cha ajabu mle ndani wale vijana ambao ni tough guy na very handsome miongoni mwao sio mbaya kumsifia mwanaume mwenzio kama ni mzuri.

Wale vijana baada ya kuniona tu wakaanza kunifuata kutaka kunisaidia ile mizigo ya vyakula niliyobeba wafikishe nje ya soko angalau niwalipe ujira kidogo wa pesa kati ya elfu 1 hadi elfu 1500 inategemea na ukubwa wa mzigo

Wengine kazi yao ni kubeba magunia na kuyapakia kwenye magari, mwisho wa siku nikagundua nchi yetu bado ipo kwenye changamoto kubwa sana kwenye suala la ajira.

Mimi tu kijana mdogo nina gari ya kutembelea nimeingia sokoni naonekana tajiri.

NAIPENDA TANZANIA.
Dah tutaona mengi
 
Aisee yani akili za wahitimu wetu hizi daah
Mwajiri wako ana kazi ya ziada...

Mkuu hao watu wamekukarimu vizuri kama mteja sokoni ati weee unaona wamekuona tajiri. Kubeba mizigo, kuuza mifuko nk nk zote hizo ni kazi halali za kuwapatia watu kipato ati wewe unawashangaa kwa kufanya izo kazi nani afanye sasa??

Umejuaje kama hao uliwakuta hapo wote wana degree.
Sijui ungekua na pesa kama boss kiduku lilo ingekuaje😁😁
 
Jamaa amemaliza degree, anafanyaga mazoezi, ana gari la mil 18, yupo single anatafuta mke, anakaa karibu na uwanja wa taifa
Ana hela ya shopping ya jumla...halafu ameshangaa wabebaji Kama vile ni mara ya kwanza kwenda sokoni.....dah
 
Aisee yani akili za wahitimu wetu hizi daah
Mwajiri wako ana kazi ya ziada...

Mkuu hao watu wamekukarimu vizuri kama mteja sokoni ati weee unaona wamekuona tajiri. Kubeba mizigo, kuuza mifuko nk nk zote hizo ni kazi halali za kuwapatia watu kipato ati wewe unawashangaa kwa kufanya izo kazi nani afanye sasa??

Umejuaje kama hao uliwakuta hapo wote wana degree.
Sijui ungekua na pesa kama boss kiduku lilo ingekuaje😁😁
Kilichonishangaza ni vile walivyokuwa wananifata fata hadi ikawa kero sasa kwangu ila yote kwa yote ni jambo la kutafuta rizik tu.
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Kiduku mdogo kaja.
Nimeaoma kwa imakini nione kuna maajabu gani
aaah aah hapana mm sio huyo jamaa.
 
Kwanza poleni na harakati za hapa na pale kwenye kutafuta riziki.

Kwa kawaida huwa nawahi sana kuamka asubuhi sana na mapema kwa ajili ya kwenda kuweka mwili sawa kwa kufanya mazoezi ya hapa na pale. Huwa nakimbia half marathon eneo ninaloishi sio mbali na uwanja wa taifa. Nakimbia na kurudi nyumbani baada ya hapo ratiba zingine zinaendelea kwa kuwa naishi peke angu kama bachela nina uhuru na muda mwingi wa kufanya vitu kwa wakati.

Ubachela una raha yake kwa mbaliii japokuwa naona umri unaelekea kuwa kwenye mahusiano ya kudumu yani kutafutaa mke sasa tuweze kuwa wawili maana bado sijaona faida ya kubadili wasichana mara kwa mara magonjwa yamekuwa mengi sana.

Leo wakati wa asubuhi niliamua kwenda mimi mwenyewe sokoni (Tandika-stereo) kununua vifaa na mahitaji kwa ajili ya matumizi ya nyumbani (chakula) huwa nikipata vijihela kidogo nanunua kwa jumla. Mabachela wenzangu wananielewa vzuri hapa. Sasa wakati nipo pale sokoni niliona vitu ambavyo dah nilipata surprise kidogo. Nilikutana na vijana wenye umri kama wangu kwa makadirio yetu wengi wetu ambao tumehitimu elimu ngazi ya degree 1(bachelor) lkn cha ajabu mle ndani wale vijana ambao ni tough guy na very handsome miongoni mwao sio mbaya kumsifia mwanaume mwenzio kama ni mzuri.

Wale vijana baada ya kuniona tu wakaanza kunifuata kutaka kunisaidia ile mizigo ya vyakula niliyobeba wafikishe nje ya soko angalau niwalipe ujira kidogo wa pesa kati ya elfu 1 hadi elfu 1500 inategemea na ukubwa wa mzigo

Wengine kazi yao ni kubeba magunia na kuyapakia kwenye magari, mwisho wa siku nikagundua nchi yetu bado ipo kwenye changamoto kubwa sana kwenye suala la ajira.

Mimi tu kijana mdogo nina gari ya kutembelea nimeingia sokoni naonekana tajiri.

NAIPENDA TANZANIA.
Wenye gari na nyumba na watoto wanakushangaa na wewe
 
Back
Top Bottom