Niliyoyaona siku ya leo Jumanne

Niliyoyaona siku ya leo Jumanne

Mkuu tembea uone. Watu wanachapakazi masaa12 viwandani na kwenye ujenzi kwa ujira wa 3000 hadi 5000. Hao wakibeba mizigo saba kwa masaa matatu wameshawin na kutengeneza mtaji mzuri tu kwa masaa mengine saba
payment yao haiko fixed wala sio permanent salary sioni ajira yao iko wapi???
 
Kununua tu ki-passo imekuwa shida..hadi umetafuta njia ya kisanii ya kutujulisha hilo..aisee lipia tangazo hili tafadhali.

Kidding.

Ila seriously,graduates wa kipindi hiki waliotoka familia zetu choka mbaya wanapata tabu sana..Hii mentality ya kusoma upate kazi ya ofisini inabidi tuibadilishe.
 
Mkuu tembea uone. Watu wanachapakazi masaa12 viwandani na kwenye ujenzi kwa ujira wa 3000 hadi 5000. Hao wakibeba mizigo saba kwa masaa matatu wameshawin na kutengeneza mtaji mzuri tu kwa masaa mengine saba
very true, kabla sijapata ajira ya kudumu niliwahi kufanya field kwenye kiwanda cha unga cha azam hapa tazara milling mle ndani kuna wale wabebaji wa unga kutoka kwenye streka kupakia kwenye magari na kwenda mikoania na nchi za jirani uzuri wa hawa jamaa wako chini ya kampuni wana sare na pesa yao inaeleweka kwa siku.
 
Kununua tu ki-passo imekuwa shida..hadi umetafuta njia ya kisanii ya kutujulisha hilo..aisee lipia tangazo hili tafadhali.

Kidding.

Ila seriously,graduates wa kipindi hiki waliotoka familia zetu choka mbaya wanapata tabu sana..Hii mentality ya kusoma upate kazi ya ofisini inabidi tuibadilishe.
siwezi tumia kigari kama icho bora niwe na kodi bolt tu uber per initembeze weeeeh then nilipe.
 
Kitaalam inaitwa conversation implicature ulichotaka kusema na ulichomaanisha ni vitu viwili tofauti
Ngoja nikuuelezee taratibu
Ulichotaka kusema ni TATIZO LA AJIRA HASA KWA VIJANA
ulichomaanisha wewe ni-athlete... pia uko single alafu unajiweza na utofauti na vijana wengi masikini.
Ajira ajira ajira
 
Jamaa amemaliza degree, anafanyaga mazoezi, ana gari la mil 18, yupo single anatafuta mke, anakaa karibu na uwanja wa taifa
[emoji16][emoji16][emoji16][emoji16]
 
Kwanza poleni na harakati za hapa na pale kwenye kutafuta riziki.

Kwa kawaida huwa nawahi sana kuamka asubuhi sana na mapema kwa ajili ya kwenda kuweka mwili sawa kwa kufanya mazoezi ya hapa na pale. Huwa nakimbia half marathon eneo ninaloishi sio mbali na uwanja wa taifa. Nakimbia na kurudi nyumbani baada ya hapo ratiba zingine zinaendelea kwa kuwa naishi peke angu kama bachela nina uhuru na muda mwingi wa kufanya vitu kwa wakati.

Ubachela una raha yake kwa mbaliii japokuwa naona umri unaelekea kuwa kwenye mahusiano ya kudumu yani kutafutaa mke sasa tuweze kuwa wawili maana bado sijaona faida ya kubadili wasichana mara kwa mara magonjwa yamekuwa mengi sana.

Leo wakati wa asubuhi niliamua kwenda mimi mwenyewe sokoni (Tandika-stereo) kununua vifaa na mahitaji kwa ajili ya matumizi ya nyumbani (chakula) huwa nikipata vijihela kidogo nanunua kwa jumla. Mabachela wenzangu wananielewa vzuri hapa. Sasa wakati nipo pale sokoni niliona vitu ambavyo dah nilipata surprise kidogo. Nilikutana na vijana wenye umri kama wangu kwa makadirio yetu wengi wetu ambao tumehitimu elimu ngazi ya degree 1(bachelor) lkn cha ajabu mle ndani wale vijana ambao ni tough guy na very handsome miongoni mwao sio mbaya kumsifia mwanaume mwenzio kama ni mzuri.

Wale vijana baada ya kuniona tu wakaanza kunifuata kutaka kunisaidia ile mizigo ya vyakula niliyobeba wafikishe nje ya soko angalau niwalipe ujira kidogo wa pesa kati ya elfu 1 hadi elfu 1500 inategemea na ukubwa wa mzigo

Wengine kazi yao ni kubeba magunia na kuyapakia kwenye magari, mwisho wa siku nikagundua nchi yetu bado ipo kwenye changamoto kubwa sana kwenye suala la ajira.

Mimi tu kijana mdogo nina gari ya kutembelea nimeingia sokoni naonekana tajiri.

NAIPENDA TANZANIA.
Biashara ni matangazo,naona vijana mnakuja kivingine,unazunguka sana, alafu kuwa na gari siyo fasheni kwa sasa.alafu utakuwa mhaya ww
 
Biashara ni matangazo,naona vijana mnakuja kivingine,unazunguka sana, alafu kuwa na gari siyo fasheni kwa sasa.alafu utakuwa mhaya ww
Mimi sio mhaya mkuu, Mimi ni myao pure.
 
Back
Top Bottom