Niliyoyaona Jijini Mwanza

Ndo vijana wenu kisa yule demu wa huko anakuja kumnaga mitandaoni kama sio ushamba n nn?

Wengi washamba
 
hata mtoa mada katika majiji yoote hapa Tz ameona mji wa kubattle nao ni Arusha, sasa jiulize ni kwanini??

hawa watu ukweli wanaujua basi tu wanakaza mafuvu.
 
Ndo vijana wenu kisa yule demu wa huko anakuja kumnaga mitandaoni kama sio ushamba n nn?

Wengi washamba
Mzee, maandishi yako yanaakisi vile ulivyo.

Ninahakika watu wanaosoma hapa wanaona shida ilipo.

Point ya kuchukua ni hii; jiamini, usiogope watu wengine wanapoamua kuacha unyonge na kujiamini.

A town wameamua kujiamini na kupenda mkoa wao. Je, kuna shida hapo?
 
Daah watu wa Arusha wanaogopwa sana sijui ni kwanini.
Ukweli ni kwamba Arusha ni nzuri sana. Na wana upendo sana kwa watu wa kuja.

Watanzania wanaiponda lakini nchi za nje wanaikubali sana A town.

Mimi sio mzaliwa wa Arusha..japo kwasasa nina makazi ya kudumu Arusha.

Ninsipenda sana kuliko mkoa wowote.

NIlipokuwa naishi Dar nilihisi siwezi kuishibpopote nje ya Dar....na hii ndio dhana ya wengi.

1. Dar ni kubwa na majengo makubwa mengi kuliko Arusha but madhari ya Dar ni mbovu kuliko Arusha.

2. Mwanza ni jiji kubwa, majengo makubwa mengi kuliko Arusha but Arusha ni bora na nzuri kuliko Mwanza.
.........................
........................
Kwani Arusha?
1. Hali ya hewa
2. Mandhari nzuri
3. Watu wake wanawaza na kujali maendeleo kuliko mkoa wowote.
 
hata mtoa mada katika majiji yoote hapa Tz ameona mji wa kubattle nao ni Arusha, sasa jiulize ni kwanini??

hawa watu ukweli wanaujua basi tu wanakaza mafuvu.
Yes man, niligundua hilo.

Binafsi nadhani Mwanza ni mji mzuri na kuna watu wakarimu na watu wabaya.

Juu ya hapo, ninaamini Arusha ni mji wakipekee na ni sehemu bora yakuishi hapa Tz.

Ukizaliwa A town na kukulia hapa hadi ujana wako basi utakuwa na advantege katika kujiamini na kuwa na exposure kubwa kuzidi mamilioni ya vijana toka mikoa mingine Tz.
 
Sasa ushamba na swaga wapi na wapi..hayo maisha ndio watoto wako wanatamani! Vyuo vikuu vingi watu wanatamani wawe wa arusha!
 
Umesema vema. Be blessed brother.
 
Sasa ushamba na swaga wapi na wapi..hayo maisha ndio watoto wako wanatamani! Vyuo vikuu vingi watu wanatamani wawe wa arusha!
Observation nzuri.

Wanafunzi wa vyuo wanaotoka A town wanaonekana wapo mbele kuwazidi wenzao wanaotoka mikoa mingine kwa maana ya lifestyle ya maisha yao.

Nilisema hapo juu, hii hali ya watu wanaoishi mikoa tofauti na A town kujiona inferior inaanzia college.

Binafsi wakati nasoma niliona hii. Wanafunzi wanaotoka mikoa tofauti na A town wanakosa kujiamini wanapokuwa pamoja na students from A town.

Ni shida kubwa
 
Tuwe wakweli Jamani, ukiacha wingi wa Mashoga-rijali ambao wapo kwa wingi sana, ambao Arusha pia ni wengi vilevile....ila Mwanza, ule mji ni mzuri kuliko Arusha, una mchanganyiko wa watu wa kutosha kutoka mikoa yote, na nchi zote za maziwa makuu.
Arusha panabebwa na hali ya hewa, otherwise Arusha na pa kikuda na pa kishamba sana, sikiliza lafudhi za watu wakiongea, halafu bado wana mambo ya kigangwegangwe.
Ukienda bei za lodge, lodge ya 25,000 hadi 30,000 Mwanza, Arusha utaipata kwa 60,000 hadi 70,000.
Mwanza wanajitahidi kwa u smart, Arusha hukawii kukutana na mtu amejifunika godoro mwilini na kichwani kajifunga mto wa kulalia.
Ukipanda bodaboda inabidi wewe uwe kama msoma ramani kwenye mashindano ya magari, ukij8fanya abiria basi bodaboda wake utastukia ameshakupitiliza ulipokua unaenda na amekurudisha ulipomchukua, huo mwendo ni kama vile mmetoka kupiga tukio bank au sheli. Arusha kuna mandhari nzuri, sema watu wake ndiyo wa kindezi sana.
 
Sasa kwani hapendi mkoa wake ..Hata population inaakisi mko wachache wengi mmeondoka kwenu.
 
Bro sema kweli ...ulishafika Arusha ipi?😂😂😂😂
Hujui hata kudanganya mkuu wangu?
Hivi kuna mchanganyiko mkubwa wa watu kama Arusha?
 
Sasa kwani hapendi mkoa wake ..Hata population inaakisi mko wachache wengi mmeondoka kwenu.
Yes, tunasaka fursa.

Sisi tunakuja kwenye mikoa yenu kuanzisha business na kuchukua fursa ambazo ninyi wakazi hamzioni au hamna akili yakutumia hizo opportunity kwa faida za kibiashara.

Jifunze kufikiri kwa kina.

Namna yako yakufikiria ipo chini. Kumradhi nimetumia maneno makali.

Lakini si ndiyo ukweli huo?
 
Bro sema kweli ...ulishafika Arusha ipi?😂😂😂😂
Hujui hata kudanganya mkuu wangu?
Hivi kuna mchanganyiko mkubwa wa watu kama Arusha?
Lijapo swala la mchanganyiko Arisha hauwezi kuifananisha na Mwanza mkuu, tuwe wa kweli.
Mimi nimeongea ukweli wangu, ingawa napenda zaidi kuishi Arusha sababu ya hali ya hewa kuliko Mwanza, ingawa nilivyovitaja ndiyo huwa vinanikata stimu.
Mwanza ni sehemu ya one time tu kwa ajili ya bata, ila kuweka makaazi kule siwezi, lakini kuwekeza ni very pwafect place kuliko Arusha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…