Niliyenaye simpendi ila naogopa kumuacha kwa kuwa anataka kunioa na umri umeenda

Smoerishi ndo unavyojiita sio bila shaka wewe ni member mkongwe ,chakufanya na umri wako unadhani in busara kweli! Nakushauri mwache huyo mshkaji awe huru ,bila shaka yupo anaemzidi tatizo hana uelekeo wa kukuoa,swali upo kwenye mahusiano ili uolewe?,au upo kwa upendo wa dhati? Hata akikuoa utaishia kumcheat na atakuulia mbali usicheze na hisia za mtu
 
Umri ulio nao umeona jinsi dunia ilivyo na huzuni na furaha kutosha tu, na Mara nyingi hukua unaifurahia huzuni yako.

Je vipi ukiwa na miaka Mara mbili ama zaidi ya umri ulio nao ukiwa na huzuni, ukikaa bila furaha eti kisa tu umekubali kuolewa na mtu usiyempenda na kumfurahia kwa sababu ya umri tu kusogea!!??

Tunaishi Mara Moja tu duniani, hivyi jitahidi kwa kadri uwezavyo kuifurahia dunia kwa kuhakikisha unafanya Mambo yenye kukuletea furaha na si huzuni na unyonge!!
 
Namuonea huruma San huyo mwanaume anavokuwa km sehem ya pumziko (kivuli) cha starehe za muda mfupi na upotevu wa muda, na wala sio nyumba ya upendo was dhati.

Jah awasaidie kwa kweli
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom