Niliwamiss sana wanajf

Kyachakiche

JF-Expert Member
Feb 16, 2009
983
207
Ndg zanguni wanajamvi, nilipotea kwa kipindi kirefu kidogo kutokana na majukumu yaliyokuwa nje ya uwezo wangu. Pamoja na ukweli kwamba bado sijayamaliza, nimekuwa nakosa mambo mengi sana mliyo yajadili kuanzia kipindi kile cha uchaguzi, baraza la mawaziri, kuibuka tena kwa sakata la DOWANS na sasa nguvu ya umma kuanzia kwa waarabu kuja huku....! Nimepitwa na mengi wala sijui nianzie wapi kwani kama vile nina msongo wa mawazo! Nianzie wapi???
 
Anzia hapa hapa tulipo...mbona unaomyesha una idea na mambo yote?
BTW, karibu sana mkuu, ulipotelea wapi?...ulienda kuoa pale kwenu Msambiazi nini, how waz ze honeymoon?
 
Nashukuru mkuu. Kuoa nilishapita huko miongo mingi kidogo iliyopita, nilikuwa nakabiliwa tu na issue za kifamilia wala siyo asali mwezi( honey moon). Nafarijika kwa kunitia moyo kwamba sijaachwa sana na treni nisije kudandia kwa mbele...
 
Anza na suala la mkuu wa Wilaya mchanga kuliko wote asiye na ujuzi wa masuala ya utawala...mkuu wa wilaya mrembo kuliko wote Tanzania........Fancy....Kama ameweza kuongoza wilaya wewe utashindwa...KARIBU SANA
 
Mkuu hapa umeiacha kidogo, tafaadhali nirudishe kwenye reli. Aksante kwa kunikaribisha tena.
 
Back
Top Bottom