The ghost writer
Senior Member
- Apr 5, 2023
- 179
- 263
Habarini! Wakuu natumaini humu wote ni wazima wa afya, jamani mwenzenu napitia nyakati ngumu sana kiasi nahisi hapa ndio mwisho wa maisha yangu.
Iko hivi nikiwa na miaka kumi na tatu nilifanyiwa ushirikina (kurogwa) na mama yangu wa kambo nikawa kama nimepooza kuanzia kwenye kiuno hadi kwenye miguu nikashindwa kabisa kutembea na pia nilipoteza hali ya usikivu kwenye masikio yangu nikawa sikikii vizuri. Kipindi hicho nilikuwa nipo form 1.
Suala hili sitolielezea sana maana ilikuwa ni simanzi na machungu kwangu na kwa mama yangu mzazi, na yote haya sijui nilimkosea nani mpaka nikawa hivi ila yote ni maisha namshukuru Mungu ALHAMDULLILLAH.. Basi miaka mingi imepita sasa takribani miaka 8 na nimeanza kutembea ila sio kivile miguu bado naiona mizito pia utembeaji wangu bado hauko Sawa na pia tatizo la kusikia napo bado lipo. NImepambana sana mpaka nikafika chuo kikuu ILa safari ya masomo haikuwa rahisi.
Kutokana na matatizo haya niliyokuwa nayo hasa kushindwa kusikia vizuri na miguu kunisumbua nimeamua kuacha chuo mwaka huu naona masomo yamenishinda maana kila nikiwepo darasani Mwalimu akifundisha simsikii vizuri na kuwa kama gogo tu darasani nikaona hapa napoteza muda nikawashirikisha wazazi mapendekezo yangu ya kuacha chuo. Wazazi wangu wamekubali japo kishingo upande, sasa hapa option nilikuwa nayo ni kufanya mambo mengi hasa biashara ila nikiangalia matatizo yangu hasa kutokusikia vizuri na suala miguu kunisumbua nakosa morali(hamu) ya kufanya biashara maana nimekuwa mtu wa kujitenga muda mwingi nakaa ndani mwenyewe.
Pamoja na hayo yote hali ya nyumbani sio nzuri kivile, maisha ni magumu japo hatukosi hela ya kula, hali hii inanifanya hata mtaji wa biashara nikose maana wazazi wangu wapi vizuri kiuchumi.
Kipindi hiki nimekuwa mtu wa kukaa ndani tu, nishakata tamaa na maisha najiona mzigo kwa wazazi wangu natamani kufa ili kuwapunguzia mzigo wazazi wangu maana kijana wao wanaomtegemea nimeshakata tamaa na maisha wakuu ni hayo tu nimeamua kushare humu angalau niutue mzigo unaonikabili.