[h=1]Nilivyoteswa na Uchawi wa Sumbawanga!-11-12..[/h]
ILIPOISHIA
Yule nyoka akaendelea kuninyonya matiti, ghafla mzee Balinaba aliingia ndani na kushuhudia. Alihamaki! Alichukizwa mno na kile kitendo. Akapiga mluzi wa kwanza lakini hakusikia, aliendelea kufanya mambo yake. Wa pili, chatu aligutuka, alipomsogelea mzee Balinaba, alimpiga kibao kikali sana. Alitoa sauti kali kisha akajikunja.
Yule nyoka baada ya kupigwa kibao, alijinyonga nyonga, halafu akajikunjua kwa hasira kama vile aliyekuwa tayari kumkabili mzee Balinaba lakini alipofika usawa wa kichwa chake, aliongezwa kerbu nyingine ambayo ilimfanya awe mpole. Chatu kutulizwa kwa kipigo cha makofi! Hayo niliyashuhudia.
Alijikunja kama jongoo, tofauti ni kuwa nyoka huyo alikuwa mkubwa. Mzee Balinaba alipiga mluzi, papo hapo nikamuona chatu huyo anaondoka, akapanda darini mpaka akapotea. Nilimfuatilia kwa jicho langu kamili hadi mkia wake unapotea. Swali tata kwangu, nilijiuliza aliishi wapi huko juu?
Mzee Balinaba baada ya kuhakikisha yule nyoka ameondoka, alinigeukia na mimi. Akanikaripia kuwa tabia yangu ya kujifanya najua vitu vingi itaniponza. Akadai kuwa amenivumilia kwa kiasi kikubwa lakini matokeo yanayojionesha kwa sasa ni kuwa najaribu kumchimba ili nishindane naye ubavu.
Nishindane naye ubavu? Nilijiuliza. Hata siku moja sikuwahi kufikiria kupambana naye. Nilimuogopa kwa kila upande. Kuanzia sura yake, umbo, tabia mpaka vitendo vya kichawi. Harufu ya mdomo wake ambao alikuwa haupitishii mswaki na kile kidonda kisichopona kwenye paja vilinifanya nisisimkwe na mwili kila nilipomfikiria.
Mnataka kunipanda kichwani, naona na mama yako naye ananichokonoa. Tabia gani ya kuja nyumbani kwangu asubuhi asubuhi? Alisema kwa ukali. Macho yake yalibadilika na kuwa mekundu kama nyanya. Muda wote huo sikujibu chochote. Siyo kwamba nilikuwa sitaki, ila sikujua nijibu nini.
Nakuuliza nijibu, aliendelea kusema kwa ukali. Nami nikabaki nimeganda. Nilipotaka kujibu kitu, mdomo ukakataa. Kumbe nilikuwa bado nimeshikiliwa kama sanamu. Sikuwa na jeuri ya kufanya lolote, kwahiyo nilimuangalia kwa jicho la ukali ambalo hata halikunisaidia chochote.
Kumbe hata yeye alikuwa amepoteza kumbukumbu kama alinigandisha. Alinipiga kofi ambalo halikunitikisa. Alipoona hivyo, alisogea karibu yangu na kuniangalia kwa umakini machoni. Akasema: Ahaaa, mpaka sasa bado! Ni Kiswahili chake ambacho hakikunyooka barabara ambapo alimaanisha alielewa.
Akainua kichwa juu, akapiga mluzi halafu akapunga mkono kichwani kwangu! Hapo hapo nikajiona nimeachiwa. Nilipoinua mguu, ukakubali, kwa maana hiyo nikawa naweza kutembea. Niligeuza shingo, pia nalo likaitika. Kwa mantiki hiyo, kila kiungo kilikuwa huru kwa wakati huo. Ilikuwa nafuu kubwa, kwani kabla mwili wangu niliuona ni mzigo.
Umejisikiaje kunyonywa matiti na nyoka? Aliniuliza.
Mateso, nilimjibu.
Mateso, mbona ulikuwa umetulia? Aliendelea kuniuliza.
Sikutulia, ila sikuwa na la kufanya. Wewe mzee ni katili sana, nilimueleza.
Jibu langu likuwa kosa kubwa. Alinipiga kofi zito ambalo lilinipeleka chini. Hakuishia hapo, aliendelea kunishushia kipigo huku akitoa maneno makali ya vitisho na masimango. Kwamba anaweza kunifanya lolote ni nisipate mtu wa kunitetea, akaongeza kuwa kwetu ni masikini na baba yangu ana tamaa.
Siyo unaleta jeuri hapa, shida za kwenu ndizo zimekufanya wewe uolewe na mimi. Mmekula vingapi kwa pesa zangu, nashangaa. Kuna siku nitawageuza wote misukule, alisema mzee Balinaba kwa sauti ambayo haikuwa na sura ya utani. Alimaanisha alichokizungumza. Alitisha kweli.
Akaongeza: Nataka ubadilike kuanzia leo, na mama yako akirudi tena hapa kuleta kimbelembele chake nyumbani kwangu kama alivyofanyua leo, nitamfanyia kitu kibaya ambacho kitabaki ni kumbukumbu ya kizazi chenu, ukoo mzima. Nataka uwe na adabu na uwaambie ndugu zako waniheshimu. Umkanye na mama yako!
Alipomaliza sentensi hiyo aliniuliza: Umenielewa? Sikumjibu. Hilo nalo likawa tatizo kwa sababu aliamka na kunitaka nimjibu haraka. Nilitaka kufanya kiburi, lakini ghafla sura yake ikabadilika. Ikawa si ya binadamu tena bali chui. Uzalendo ukanishinda, nikajibu kwa woga kwamba nimemuelewa.
Nilipomjibu hivyo, alitikisa kichwa kama vile amenielewa. Sura yake ikarejea kama kawaida. Akageuka kutaka kutoka nje lakini kama vile alikuwa amekumbuka kitu, alinishika mkono kwa nguvu na kuniongoza kuelekea chumbani. Ilikuwa ni mfano wa amri za kijeshi na inawezekana ni zaidi, kwa sababu sijapita jeshini ila nasimuliwa tu!
Alinishurutisha hadi chumbani ambako haraka sana aliniamuru kupanda kitandani.
Nilipotaka kupinga, mzee Balinaba alibadili sura yake na kuwa kama chui. Hilo likawa likaniogopesha mno, hivyo kujikuta natii kila aliloniambia. Mwanzoni sikujua lengo lake ni kufanya mapenzi, lakini kumbe ndicho alichotaka.
Nilikuwa nimevaa kanga moja, kwahiyo aliivuta na kuniacha mtupu. Baada ya hapo na yeye alivua msuli wake na fulana na kupanda kitandani ili kunikabili. Alikusudia kufaidi penzi langu. Kumbukumbu za uchafu wake na kile kidonda, ukijumlisha na uchawi, vilinipa hamasa ya kumuwekea kikwazo.
Hata hivyo, nilipotaka kufanya hilo nilikutana na ile sura ya chui. Nikanyewea, hivyo nikamuacha aje kifuani kwangu. Akaingia kwa kujiamini huku akiguna kama vile dume la nyani. Nilijihisi mnyonge. Inauma mno kuwa mtumwa wa ngono, tena unafanyiwa hivyo na kibabu kinachojivunia nguvu za giza.
Picha ya wazi kwangu ni kwamba mzee Balinaba alikuwa na nguvu za ajabu. Na alitaka nimpe ushirikiano wa tendo, kwani angeweza kufanya mwenyewe huku nikiumia na akaniacha baada ya kumaliza shida zake, lakini haikuwa hivyo. Kadiri aliponikaribia ndivyo na akili yangu ilipobadilika.
Nikajikuta nami natamani penzi lake. Nikaanza kumpa ushirikiano. Eti, nikaona joto lake ni maridadi kwangu. Nikamkumbatia kwa nguvu. Hata nyoga nilikata. Alivyo hana utu, naye akawa ananipongeza kwa mahaba niliyompa. Msomaji haikuwa matakwa yangu, ila aliniteka kwa nguvu za giza.
Itaendelea baadae