Nilivyoteswa na Uchawi wa Sumbawanga!

Nilivyoteswa na Uchawi wa Sumbawanga!

Mh!!...aisee kumbe dunia ina mambo hv?? Sumbawanga ckanyagi ng'o..ila kama una nguvu ya Yesu haya mambo hayasumbui!!!
 
Ni dunia ya mikiki mikiki. Kuchelewa kufa ni kuona mengi lakini usiombe kukutana na viroja vya Wachawi wa Sumbawanga. Katika kipindi ambacho nimeishi kwenye ulimwengu ambao wengi wanadhani ni wa kufikirika, nimeweza kuuona uchawi na kujua tafsiri yake.
Fanya ibada unavyoweza ili wachawi wakae mbali na wewe, vinginevyo utageuzwa chakula kilichoungwa viungo vya kupendeza. Namshukuru Mungu nipo hai, nadunda duniani tena navuta pumzi safi, hewa ya oksijeni. Asante Mungu kwa kunipigania.

Leo hii pengine ningekuwa nalima shamba la wenyewe. La, basi ningekuwa marehemu. Chokochoko ndogo ya kukataa kuolewa na Kibabu cha Sumbawanga ndiyo ilisababisha niingie kwenye mapambano na watu ambao wanaamini wao ni wababe kuliko chochote chini ya jua.
Naitwa Helena Nsuzuguye, mzaliwa wa Sumbawanga katika familia iliyoishi kwa imani ya kati, yaani tulimuamini Mungu lakini si kwa kiwango kikubwa. Mama alihudhuria Kanisani kila Jumapili, baba haikuwa muhimu kwake na zaidi ya kushinda kwenye vibao vya kahawa na pombe.
Baba alikuwa mlevi wa pombe za kienyeji, hiyo mara nyingi ikawa inaleta usumbufu nyumbani. Mama ndiye aliyekuwa akijituma kuhangaikia familia yetu. Kutafuta riziki ya kutuwezesha kuweka chochote tumboni, pia kutuhudumia mahitaji ya shule.

Mimi na ndugu zangu watatu, yaani kaka yangu na wadogo zangu wawili kusoma kwetu ilikuwa tabu tupu. Shule tulienda bila kuvaa viatu, sare zimechanika na haikuwa shida sana kwani tulipiga moyo konde na kuendelea na masomo yetu.
Kufika darasa la sita mambo yakabadilika. Kuna kibabu tulichozoea kukiita, Mzee Balinaba (Barnabas), kwa muda wote ambao nimekua na kumuona, alikua hana mke wala mtoto. Nyumba yake ilizungukwa na shamba kubwa la miembe, michungwa, michenza, mistafeli, mipapai na michikichi michache.

Yule mzee ni mkubwa kuliko hata baba yangu, ni kibabu hasa! Nikiwa darasa la sita, siku moja baba aliwahi nyumbani tofauti na kawaida yake. Alionekana mchangamfu na mkononi alishikilia kifurushi. Alikuwa amebeba nyama ya nyati.

Alipofika alisalimia, akataka aonane na wanaye wote. Tukakusanyika, kila mmoja akampa shilingi 50, baada ya hapo akataka wote waende wakalale ila nibaki mimi na mama. Sikuhisi kitu chochote kibaya, kwahiyo nilibaki nikiwa na shauku ya kujua kilichonibakiza.
Baada ya waliotakiwa kuondoka, kilipita kimya cha sekunde kadhaa. Muda wote huo baba alikuwa anatutazama usoni kama vile kuna kitu anataka kutuambia lakini akawa anajishauri jinsi ya kuanza. Alikohoa mara tatu, tukadhani anaweka sawa koo.

Sisi tukabaki kumshangaa na kungoja kwa hamu hicho alichotaka kutuambia. Muda ulipozidi kwenda, ilionekana mama amechoka kusubiri, akaamua kuvunja ukimya: % Itaendelea baadae....

Sumbawanga hii haistawi wewe,,,,,,,,,,,,,,sijui hii hadithi inahusu Sumbawanga ipi??
 
Mh!!...aisee kumbe dunia ina mambo hv?? Sumbawanga ckanyagi ng'o..ila kama una nguvu ya Yesu haya mambo hayasumbui!!!
Karibu sana, huku amani kabisa hii ni hadithi ya kuwatisha ninyi waoga waoga.
 
jamani nilikuwa niko kwa majigo namalizia nitakufa mara ya pili sasa ngoja nielekee uchawi wa sumbawanga
 
Back
Top Bottom