Nilivyoteswa na Uchawi wa Sumbawanga!-9
ILIPOISHIA Nikamsikia mama anapiga kelele kule nje. "Nakufaa!" Mzee Balinaba akawa anacheka kama vile anajisifu kwa ushindi. Mimi nikashindwa kufanya lolote. Nilikuwa nimegandishwa na sauti haikutoka. Hata hivyo, niliweza kuipima sauti ya mama kwamba alikuwa anapiga mayowe huku akikimbia.
Mimi kule ndani nilibaki kama sanamu. Sikuweza kufanya chochote! Sauti ya mama iliisha na ikafika wakati nikawa simsikii tena. Dakika chache za ukimya zilikatika, baadaye kwa mbali nikamsikia mzee Balinaba akija huku akiongea kwa hasira. Alisikika kwa ukaribu kadiri muda ulivyokuwa unasogea.
Sauti ya mzee Balinaba ilisogea hadi mlangoni, lakini kabla sijamuona yeye, yule nyoka mkubwa aina ya chatu alitokeza na kunizunguka! Alianza kunibana, na alipohakikisha mwili wote amenidhibiti, alitoa ulimi na kunilamba kwenye tundu za pua. Dalili za kifo nikaziona, nikaona nakufa kama mnyama.
Nilikuwa nimekwishaandaliwa kifo! Nilimsikia mzee Balinaba akizungumza wakati akidhani nipo usingizini. Alisema lazima animalize ili anikomeshe kwa sababu eti, nilikuwa kimbelembele kwa sababu mara kwa mara nilishtukia ‘ishu' zake za kichawi! Alidai nataka kujipima nayeye.
Najua tukio lililomuuma zaidi ni pale nilipoamka na kumkuta akiwa taabani bila fahamu. Usiku uliopita ambapo alipambana na wapinzani wake kwenye masuala yao ya uchawi na kuzidiwa nguvu, hivyo akaangushwa angani na kuangukia chumbani. Hiyo ilimuudhi sana, kwani alitegemea mimi ningelala kama pono kwa sababu alinipaka dawa za kichawi.
Vile nilivyokuwa siwezi kufanya chochote, yule chatu aliendelea kunitawala, alinibana pumzi ikaisha. Kwa wakati huo, nilitamani mzee Balinaba atokee, kwa maana niliamini angekuja angeweza kumfukuza yule chatu, hivyo kuniacha nikipumua! Kuchelewa kwake kungemaanisha kifo changu.
Mzee Balinaba nilimsikia akizungumza peke yake nje! Alikuwa anafoka utafikiri kuna mtu alikuwepo mbele yake. Alichokuwa anazungumza sikukipata vizuri kwa sababu yule chatu alikuwa akinibana na kunipotezea umakini wa kumsikiliza. Aliponilamba tundu za pua, mwili wote ulisisimka.
CHATU ANANINYONYA MATITI!
Nilikuwa nimevaa kanga moja! Wakati yule chatu akiendelea kunisulubu, ghafla alibadili uelekeo, akaanza kuacha kunibana. Taratibu akawa anajikunjua. Kitendo hicho kilinipa unafuu mkubwa. Kwani nikaweza kupumua. Nadhani angeendelea kunizunguka kwa dakika chache ningekufa!
Mzee Balinaba hakuwa na habari kabisa, aliendelea na mambo yake kule nje. Kwa mpita njia angedhani alikuwa anamfokea mtu aliyemuudhi mno! Angefanikiwa kumuona na kuona anavyofoka, angeamini amechanganyikiwa, lakini mimi kwa sababu namjua, ule uchawi! Napenda watu wajue kuwa uchawi unapumbaza akili ya kawaida.
Mchawi hasa akili zake huwa fyatu! Na hivyo ndivyo alivyokuwa mzee Balinaba. Kusema ule ukweli, pale alipokuwa, hata siku moja hakuwahi kufikiria kufanya jambo la maendeleo. Yeye ni habari za kichawi na kuua. Leo, akikwambia kuna watu wamemuudhi anataka kupambana nao, kesho atakupa hadithi za kutaka nyama ya mtu, eti sadaka kwa wachawi!
Kwa maana hiyo, wakati mzee Balinaba akiendelea kupiga kelele kule nje, huku ndani, yule chatu alijifungua kabisa mwilini mwangu. Nikawa huru. Akaanza kuniangalia kwa macho fulani ambayo sikuyaelewa barabara. Maskini ya Mungu sijui lugha ya nyoka, kwahiyo sikuambulia chochote.
Hata hivyo, kiwango cha woga kilikuwa juu mno! Jamani nikisema ni chatu mkubwa elewa ni mkubwa mno! Urefu wake kwa kuukadiria ni futi 18 na upana ni zaidi ya nazi kubwa iliyokwishafuliwa! Kuna wakati alijaribu kunisukuma, nadhani lengo lake lilikuwa nianguke lakini hakuweza. Nilibaki nimeganda.
Haa! Kweli ni nyoka wa miujiza! Na kuna uwezekano ni mtu kabisa ambaye aligeuzwa vile kwa njia za kishirikina! Jitihada za yule chatu kuniangusha ziliposhindikana, alidaka kanga niliyokuwa nimevaa kwa mdomo wake na kuivuta. Haikuchelewa kuvuka, na sikuweza kuizuia kwa sababu mwili haukuwa na kazi yoyote.
Baada ya kuvuta kanga na kuondoka kabisa, yule chatu alinizunguka kama vile alikusudia kunibana. Hata hivyo, wakati huu hakuniminya kama alivyofanya mwanzo. Alipanda taratibu na alipofika kifuani, alitulia kwa sekunde kadhaa halafu akaniangalia usoni. Bado macho yake hayakuwa na tafsiri yoyote kwangu, ingawa kwa haraka nilihisi alidhamiria kunimeza.
Macho yangu hayakuwa na uwezo wa kukapua wala kuhamisha mboni kutoka upande mmoja hadi mwingine, kwa maana hiyo tulipokutanisha macho na kugeuka kufanya vitu vingine mimi sikuwa nikimuona, zaidi nikabaki kuhisi kwa sababu ni mwili wangu na hisia zilikuwepo ingawa sikuweza kujitikisa.
Hakika nazungumza kwa msisitizo kwamba yule ni nyoka wa miujiza! Akiwa bado yupo pale kifuani kwangu, mara nikasikia nyonyo yangu ya mkono wa kushoto inaguswa. Mwili ukasisimka! Ikageukia upande wa kulia, hali ikawa ile ile! Kumbe ni nyoka alikuwa ananinyonya matiti.
Aliendelea kufanya hivyo, mwili wote ukawa unasisimka! Woga wa ajabu ulikuwa unanishika, kwani nilihisi anaweza kung'ata pale kwenye matiti na kuniachia ulemavu. Wakati huo ndiyo akawa amechanganya, na ni wazi alifurahia kutokana na jinsi mkia wake ulivyokuwa unatikisika. Yaani hisia zilitoka kichwani hadi mkiani.
Yule nyoka akaendelea kuninyonya matiti, ghafla mzee Balinaba aliingia ndani na kushuhudia. Alihamaki! Alichukizwa mno na kile kitendo. Akapiga mluzi wa kwanza lakini hakusikia, aliendelea kufanya mambo yake. Wa pili, chatu aligutuka, alipomsogelea mzee Balinaba, alimpiga kibao kikali sana. Alitoa sauti kali kisha akajikunja.
Itaendelea baadae
Nilivyoteswa na Uchawi wa Sumbawanga!-10...