Nilivyonusurika Kifo baada ya Mzee kunitimua Nyumbani

Nyie watu ni shida!!
Nilivyonusurika Kifo baada ya Mzee kunitimua nyumbani - 22.


Tuliondoka na gari lile eneo kuelekea ambako tuliambiwa tunakwenda kuchukua pesa ya Bosi.Ile gari baada ya kutembea kwa umbali mrefu hatimaye ilisimama kando ya barabara ya vumbi na ndipo yule jamaa(Jipe)akatutaka tuteremke!.

Jipe "Katusubiri pale mbele ya lile karavati"

Jipe alimwambia yule dereva azime taa kisha akatusubiri kwenye karavati lililokuwa mbele!.Jamaa aliongoza na sisi kumfuata nyuma,mtatiro na Jipe ambao walikuwa na silaha,walikuwa wamevaa makoti marefu ambayo yalifanya zile silaha walizokuwa nazo kutokuonekana kwa urahisi!,sasa baada ya kutembea kwa umbali mrefu kidogo hatimae tukafika kwenye nyumba moja ambayo haikuwa na geti wala fensi!,jamaa alisogea hadi mlangoni akaanza kusukuma ule mlango kana kwamba ulikuwa wazi,baada kusukuma ule mlango na kuzunguka ile nyumba,jamaa alitoa simu akampigia Gabi,baada ya mazungumzo jamaa alitwambia tuondoke haraka maana kumbe tuliingia chaka,eneo lililokusudiwa halikuwa hilo!,tulitembea kwa haraka kuifuata ile gari na hatimaye tukaianza safari kuelekea kulipokusudiwa!.Wakati huo wote mimi sikuwa na silaha zaidi ya kuwafuata nyuma Jipe na Mtatiro ambao wao ndio walikuwa na Silaha!.

Baada ya safari ya dakika kadhaa tukawa tumefika kwenye eneo ambalo lilikuwa na nyumba kadhaa ambazo ilionyesha kabisa walioishi eneo hilo walikuwa na vyanzo vizuri vya Mapato.

Jipe "Kila mtu ajifunge vitambaa"

Aliendelea "Nitakachosema ndicho mtakachokifanya"

Sisi "sawa"

Tuliteremka kwenye ile gari tukaanza kutembea kuelekea kwenye nyumba iliyokusudiwa;Lile eneo lilikuwa limetulia sana kwa wakati huo maana ilikuwa yapata mida ya saa 7 usiku.Tulipofika nje ya geti Jipe alipanda ukuta akawa ameruka kwa ndani,sasa wakati jamaa akiwa ndani nikasikia sauti ya mbwa akibweka kwa nguvu sana,jamaa hakutaka kupoteza muda,nilisikia sauti ya risasi ikipigwa na yule mbwa sikumsikia tena!.

Jipe "Ingieni ndan"

Jipe alituambia kwa sauti kubwa iliyoonyesha msisitizo,basi tulipanda ule ukuta tukaruka kwa ndani!.Baada ya kuingia ndani ndipo jamaa akawa anaangalia namna ya kufanya ili tuingie ndani!.Jipe alianza kupiga lile geti la chuma kwa risasi hadi likaachia ukawa sasa umebaki mlango wenyewe!.Kiukweli mara ya kwanza nilitaka kukimbia baada ya zile sauti za ile bunduki zenye kishindo kikubwa,nilibaki kumtazama Jipe muda huo ambao hakuwa na mchezo kabisa!.

Sasa nilianza kusikia kwa ndani sauti za watu wakilia na kuomba msaada,mahali ilipokuwa ile nyumba kulikuwa na nyumba nyingine ambazo hakukuwa na mtu aliyetoka nje hata mmoja.Wakati jamaa akipambana ili ule mlango ufunguke tuzame ndani,kuna sauti ya kiume ilikuwa inasikika kwa ndani ikisema "Atakaye ingia huyo ni halali yangu!".

Jipe "Hebu nipe hiyo silaha,kamata hii"

Alichukua ile silaha ya Mtatiro akaanza kupiga risasi kwenye kitasa cha ule mlango hadi ukaachia!.Baada ya kitasa kuachia aliusukuma ule mlango kulekea ndani kisha na jamaa akawa ameingia ndani!.

Jipe "Ingieni ndani"

Tuliingia ndani ambako tulifika sebuleni na hatukukuta mtu hata mmoja,sasa jamaa akamrudishia Mtatiro silaha yake kisha akachukua ya kwake ambayo Mtatiro alikuwa nayo!.Jamaa alikuwa jasiri sana na ilionekana hata lile tukio halikuwa la mra ya kwanza,inaonekana alishayafanya sana yale matukio na ndiyo maana alikuwa akijiamimi sana!.Tulitembea kuelekea vyumbani ambako jamaa alituambia tufuatane nae!.Ile silaha ndugu zangu ioneni tu askari wamebeba lakini ni hatari sana,sikuwahi kabisa kusikia ikipigwa karibu,siku hiyo ndiyo nilifahamu kwanini silaha ni hatari sana hadi serikali kupambana na wahalifu!.Pia ni kitu ambacho ukiwa nacho kinakupatia kujiamini kupita maelezo,namna ambazo jamaa alikuwa akijiamini tulivyofika pale haikuwa na mfano,wewe fikiria ile sauti iliyosema "Atakaye ingia ndani huyo ni halali yangu" lakini hakujali kitu!.

Jipe "Magige fungua mlango mwenyewe"

Aliendelea "Nikifungua mimi umeumia"

Sasa kuna sauti ya kiume ikasikika ndani ya chumba ikiwa inajitetea!.

Sauti ya kiume "Tafadhali nawaomba mchukue chochote msiniue!"

Jipe "Fungua mlango unanipotezea muda msenge wewe!"

Basi yule jamaa aliyekuwa chumbani alifungua ule mlango.Baada ya kufunguliwa ule mlango Jipe aliusukuma kwa mguu kwa nguvu ukawa umejifungua zaidi!.Sasa nilibaki kushangaa kwasababu wakati tukiwa nje nilisikia huyo jamaa akisema atakaye ingia ndani atakuwa halali yake nikadhani uenda alikuwa na silaha kumbe ilikuwa zuga tu!.Tulipoingia ndani tulimkuta jamaa akiwa na mwanamke pamoja na dada mmoja na watoto watatu,wa kike wawili na wa kiume mmoja,jumla yao kufanya kuwa watu sita!.

Jipe "Pesa ziko wapi?"

Aliendelea "Usinipotezee muda nataka pesa"

Jipe "Lale chini sitaki mniangalie wapumbavu nyie"

Baada ya kusema vile,niliona yule mwanamke anawakusanya wanae na kulala chini huku wakifunika nyuso zao chini!.Sasa yule jamaa akawa kama anategea kujibu lile swali la wapi pesa ilipo,Jipe alikoki ile silaha akamtandika ya mguuni yule jamaa akaendelea kulia kwa maumivu makali pale chini.

Jipe " Nimekwambia nataka pesa usinipotezee muda"

Baada ya kuona hali inaweza kuwa mbaya zaidi ndipo yule mwanamke akapiga kelele huku akilia akisisitiza tusiwaue na akaeleza pesa ilipo!.Alinyanyuka tukaongozana nae kuelekea jikoni ambako pembeni kulikuwa na stoo!".

Yule mwanamke "Pesa hiyo hapo chini ya vigae!"

Jipe "Oya hebu funua vigae hivyo utoe hiyo hela"

Niliingia ndani ya kile chumba ambacho kilikuwa stoo nikaanza kutoa vile vigae ambavyo vilikuwa vimewekwa juu ya mzigo kwenye gunia.Nilifanya haraka sana maana hatukutaka kupoteza muda kabisa lile eneo!.Nilipofurumusha vile vigae chini,ndipo nikafikia gunia lililokuwa limejaa manguo ikabidi nilinyanyue nikalitoa mle stoo!.

Nilianza kuyatoa yale manguo yaliyokuwa kwenye lile gunia hatimae nikazifikia pesa ambazo zilikuwa nyingi zimefungwa kwenye mabunda ya elfu tano tano na elfu kumi kumi!.

Jipe "Beba tuondoke"

Nikabeba lile gunia na kuondoka eneo la tukio kuifuata ile Mark 2 iliyokuwa imepaki mbali kidogo ikitusubiri.Tuliondoka yale maeneo kwa spidi kali kuikamata njia ya Mwanza na safari ikaanza.Tulitembea kwa spidi kali hadi maeneo ya mgodi ule wa Buzwagi kisha kuikamata njia ya kuelekea eneo tulilokuwa tumemuacha Gabi,baada ya kufika pale jamaa aliniambia nikimbie haraka kumuita Gabi ili tuondoke.Gabi alitoka ndani kwa spidi kali baada ya kumshitua kisha tukaingia kwenye gari na kuondoka lile eneo.

Jipe "Mwanangu hakikisha risasi inakuwa chemba,hatujui kilichoko mbele yetu"

Mtatiro "Iko sawa tayari"

Ile gari ilikuwa inatembezwa kwa spidi kali huku ikiwa imezimwa taa,sasa kuna mahali tulifika Jipe akamwambia dereva asimamishe gari kwanza,gari iliposimamishwa akaniambia nikae siti ya mbele yeye arudi nyuma akae na Mtatiro.

Jipe "Washa taa tuondoke"

Dereva aliwasha taa na safari ikaanza,sasa tulipofika karibu na tinde,Jipe akatoa maelekezo ya kwamba,endapo kuna mtu akatokea akasimamisha gari ahakikishe hasimami!.Namshukuru Mungu pale tinde tulipita salama kabisa,sasa tulipofika mbele kabisa kuikaribia shinyanga jamaa akachukua zile bunduki akanyanyua siti walizokuwa wamekalia akaziweka,kisha tukaondoka kwa spidi kali!.Njiani hatukusumbuliwa kabisa.Tuliingia Mwanza mida ya saa 9 usiku hadi kule kwenye ile nyumba siku ya kwanza tulipoenda na Gabi!.
 
Chuma
1005211026b-1333x750.jpg
 
Kama unao uwezo leta story yako si wasomaji ndo tutaamua kuikubali au kuikataa, tabia ya kuvizia vitu vya watu na kuleta criticism zennu muachage bwana maana haziwasaidii
Bob wewe basi hujaenda shule level za juu au hujasoma vitabu na kuangalia movies. Ni jambo la kawaida sana kupata criticism na wasomi huzichukulia positively na kurekebisha. Waswahili huzichukulia personal na kuona ni chuki binafsi sababu wanajaa unafiki sana.

Mimi nimesoma na nina exposure nafaham the importance of criticism.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom