Umesikia mengi lakini bado hujasikia na utasikia tena

Peter Mwaihola

JF-Expert Member
Jun 23, 2022
234
367
Tukiwa High School kuna jamaa mmoja sikumbuki vizuri kabila lake kama alikuwa mkurya au mjaluo.

Ila nakumbuka jina lake tu ambalo nadhani alikuwa anaitwa Daniel Mtatiro.
Sasa yule jamaa bwana tulipofika pale shuleni alikuwa anahudhuria vipindi vya dini kila siku.

Baada ya mwezi mmoja kuyazoea mazingira ya shule yule jamaa ghafla aliacha kuhudhuria vipindi vya dini.
Jioni ikifika alikuwa anatafuta eneo la kujificha mpaka kipindi cha dini kiishe naye anarejea bwenini ama kwenda prepo kujisomea.

Mara kadhaa Viongozi wa serikali ya wanafunzi walikuwa wanamuita na kumuonya kwa tabia yake hiyo lakini bado aliendelea pasipo kujali.

Siku moja majira ya jioni jopo la Viongozi wa dini pale shuleni likambana mbavu bwana Mtatiro ili kumhoji kwanini hahudhilurii vipindi vya dini.

Akatoa sababu mbalimbali akijitetea lakini zikaonekana za kawaida na hazina mashiko.

Unaweza kudhani umeyasikia mambo duniani lakini bado hujasikia na utasikia mengi makubwa.

Bwana Mtatiro alipoona anazidi kubanwa mbavu aeleze vizuri kwanini hahudhilurii vipindi vya dini Mtatiro alisema amesoma sana Biblia na kuimaliza yote hivyo haoni kipya cha kufuata kwenye vipindi vya dini.

Watu wote tukaangua kicheko, baada ya hapo tukasikitika kwa jibu lake ambalo kwa hali ya kawaida hatukutegemea kama lingetoka kinywani mwake.

Dunia ina mengi sana na bado haujayasikia na utayasikia tena na tena zaidi ya haya ya bwana Mtatiro.

Peter Mwaihola
IMG_17063697787793926.jpg
 
Back
Top Bottom