Hili tukio lilinichekesha sana japo mwamba aliaibika mno

DeMostAdmired

JF-Expert Member
Oct 7, 2017
1,181
2,946
Habari ya muda huu..

Ilikuwa mwaka 2010 kwetu huko Tabora.
Sisi tulikuwa wakulima wazuri wa zao la tumbaku. Wafanya kazi wetu kwa asilimia kubwa tulikuwa tunawatoa Burundi.

Kulikuwa na huyo jamaa anaitwa Lenard. Jamaa alikuwa mchapa kazi sana lakini alikuwa mlevi pia tena mlevi mzuri tu wa pombe hizi za kienyeji, pombe ambazo ukiwa na buku unalewa wewe na jamaa zako kilingeni.

Kipindi hicho kilikuwa ni cha kukausha tumbaku katika mabani. Kwa wale wazoefu wanayajua mabani na jinsi tumbaku inavyokaushwa. Sasa siku hiyo ilikuwa ni weekend namimi nilikuwa napenda sana weekend kuwajoin wasela kwasababu walikuwa wananichukuwa tunaenda wote kuwinda porini na mbwa na tumekula sana visungura na vindege ndege vya porini.

Sasa siku hiyo ilikuwa jmoc, tumbaku ilikuwa inamalizikia kukauka katika bani ambapo kesho yake bani lilizimwa kwasababu tumbaku ilikuwa tayari ishakauka kikamirifu.
Siku hiyo jamaa huyu Lenard alifua vinguo vyake ili kesho yake jpili aingie kijijini apate pombe asherehekee weekend then j3 arudi shambani.

Lenard alikuwa ni jamaa ambaye akienda kunywa pombe kilingeni ni lazima atafutize ugomvi hata kwa kufosi ili tu apigane na mara nyingi alikuwa anashinda vita so jamaa alikuwa ni mkorofi.

Miongoni mwa nguo ambazo Lenard alifua ni chupi yake, enzi hizo kulikuwa na hizi chupi za tmk wanaume. Sasa jamaa akaanika nguo katika gogo ambalo lilikuwa motoni. Gogo lilikuwa ni refu so akazipanga nguo zake ili zikauke kupitia lile joto la ule moto.

Ile chupi aliitanguliza mbele kutokea kwenye moto then nguo zingine ndo zikafuata.
Jamaa akasema kwamba atajistua baadae ili kuzitoa nguo zisiungue maana gogo lilikuwa linaungua taratibu kuelekea kwenye zile nguo.

Mimi nililala ndani ya nyumba na wao walikuwa nje ili kuangalia maendeleo ya bani. Jamaa usingizi ukampitia lakini kulikuwa na jamaa mwingine upande wa nyuma wa bani alikuwa ametulia zake anapiga fegi mdogo mdogo.
Sasa lile gogo liliungua mpka moto ukaifikie ile chupi, chupi ilianza kuungua lakini kwa bahati nzuri yule jamaa mwingine alikuwa macho bado na alisikia harufu ya nguo inayoungua akaenda na kukuta chupi ya msela inaungua akaivuta na kijiti na akazitoa nguo zingine pia.

Sasa jamaa akamuamsha Lenard, Lenard alipoamka akaikagua ile chupi yake na ilikuwa imeungua kale kajisehemu kanakopita katikati ya mapaja na kalikuwa kameungua na kukatika kote.
Jamaa hakukaacha kale kachupi kake kesho yake na akaibuka kijijini kwenda kunywa pombe.

Jamaa kama kawaida yake baada ya kulewa akaanza kuutafuta ugomvi mpka akaupata.
Sasa wakaanza kupigana na jadi ya Lenard alikuwa akitaka kupigana anavua shat anabaki kifua wazi.

Sasa ile vita ya siku hiyo ilikuwa ni ya kubiringishana chini. Lenard yupo kifua wazi, kale ka chupi hakana kile kijisehemu cha katikati kwahyo chupi ikawa inapanda taratibu kuja juu.
Lenard hana habari yeye anavurugana na mlevi mwenzake pale chini.

Ile chupi ikapanda mpka ikafika usawa wa kifuani... Mamaaah watu wakaanza kucheka na wanawake wengine walikuwa wanaona aibu wanaondoka pale wanaenda mbali ili wasishuhudie ile aibu kwa yule jamaa.

Sasa Lenard alipogundua kuwa tayari mambo yapo hadharani akatoka kwenye mchezo akaanza kutafuta wapi shati lilipo ili ajistili.
Yule mwamba alokuwa anapigana naye akapata mwanya wa kutafuta points 3 muhimu. Jamaa akaanza kuivuta ile chupi ya Lenard huku anampa manguni ya usoni.

Lenard akawa anazidi kutoka mchezoni, jamaa naye alikuwa anafanya kumkomoa aliivuta ile chupi mpka akaitolea upande wa kichwani kwa Lenard anampiga buti la tumboni Lenard kaanguka chini hafu msela akaenda akamrushia chupi yake karibu na alipokuwa amelala.

Watu walicheka sana na wengine walimuomea imani Lenard wakamstili wakamvutia ndani na ile chupi wakaitoa pale nje.

Huu mchezo niliushuhudia mwanzo mwisho nilicheka kimtindo lakini nilisikitika sana kwasabb Lenard alikuwa mwanangu sana japo alikuwa mkubwa sana kwangu lakini zilikuwa zinaiva sana.

Hili tukio ni kama lilikuwa la faida sana kwa Lenard kwani kwanzia siku hiyo Lenard hakukanyaga kilingeni kunywa pombe na mpka leo alishaoa na yupo Tabora hakurudi kwao Burundi yupo bushi tu huko anaendelea na maisha na alifanya utaratibu wa kupata kibali cha kuishi na kufanya kazi Tz na mpka leo yupo na hanywi tena pombe. Nafikiri ni kama alipata uraia kwa tz kwasababu ni miaka mingi sasa yupo tz.

AHSANTENI!!!
 
Mwaka gani ilikuwa nyinyi mimi nawajua na huyo Leonard namjua vizuri tu hiyo siku mimi nilikuwepo hapo
Na mwaka huu mwanzoni nilikuja msibani huko na Leonard tulionana nilimkumbusha hiyo story alicheka sana akifurahi
Sema ni tabora sehemu gani
 
Mwaka gani ilikuwa nyinyi mimi nawajua na huyo Leonard namjua vizuri tu hiyo siku mimi nilikuwepo hapo
Na mwaka huu mwanzoni nilikuja msibani huko na Leonard tulionana nilimkumbusha hiyo story alicheka sana akifurahi
😂😂😂
 
Kama sio wilaya ya kaliua basi ni urambo maana tumbaku hulimwa kwa wingi huko hata kaka yangu alikuwa mkulima wa hilo zao.Na tulikuwa tunatoa burundi tunamix na kigoma wafanyakazi.

Maeneo ya kaliua huko igagala,usinge ,imalamakoye ,imaramihayo.mtoa mada ukipataja hiyo sehemu naijua vizuri.

Ila warundi wanajituma sana kwenye kazi sema tatizo ni migration ndio tatizo watu wanachomeshana.

Kunatukio nikilisema unaweza kunifahamu ngoja nikaushe.
 
U
Kama sio wilaya ya kaliua basi ni urambo maana tumbaku hulimwa kwa wingi huko hata kaka yangu alikuwa mkulima wa hilo zao.Na tulikuwa tunatoa burundi tunamix na kigoma wafanyakazi.

Maeneo ya kaliua huko igagala,usinge ,imalamakoye ,imaramihayo.mtoa mada ukipataja hiyo sehemu naijua vizuri.

Ila warundi wanajituma sana kwenye kazi sema tatizo ni migration ndio tatizo watu wanachomeshana.

Kunatukio nikilisema unaweza kunifahamu ngoja nikaushe.
Upo sahihi
 
Back
Top Bottom