Niliponea chupuchupu baada ya kula limbwata lenye sumu

green rajab

JF-Expert Member
Oct 16, 2015
11,171
35,491
Binadamu hawana shukrani. Miaka 6 iliyopita nlikutana na binti fulani wa kisukuma baada ku-wrong number kwangu nikamsaka tukaonana mitaa yao ndio nilikuwa na site yangu.

Baada ya hapo tukaingia kwenye mahusiano akanasa mimba, nikamwambia aitoe ikashindika ikabidi aende kwao Nzega akajifungua.

Ilipita mwaka bila kuonana mimi nilikuwa Tanga kikazi, baada ya kurudi Dar nikaamua nikamcheki mtoto nilipe nusu mahari nimchukue tuje tuanze maisha.

Nilifanikiwa baada ya kuonana na wazee wake nikaandika barua ya uchumba nikakubaliwa, mimi nikatangulia Dar baada ya 2 weeks nikatuma nauli akaja bongo tukaanza maisha.

Nilimjali sana kwa kila kitu kama mume, baada ya week 1 nikaanza kuona kama hayuko real kutwa anaongea familia yao kisukuma nikampotezea.

Wiki ya 2 akaaga anaenda kwa ndugu zake kusalimia, nikamruhusu ila machale yalinicheza nikamwambia mdogo wangu niliyekuwa naishi naye kama hiyo safari yake ya wema au ubaya tutajua tu.

Alivyorudi mchana sikuwepo, nikarudi usiku wa saa 2 nikakuta amelala chakula katenga kabisa kipo mezani, nikatilia shaka chakula cha pekee ako ila nikaomba Mungu nikakila. Baada ya masaa mawili tumbo likaanza kuvuruga mbaya nikajua ule msosi sio mzuri, nikamwambia mke lakini hakujali kabisa. Nikasitisha kula chochote hapo ndani nikaenda hospitali nikapatiwa dawa lakini sikupata nafuu.

Siku ya 9 bila mafanikio nakapata wazo la kumfanyia upekuzi mizigo yake yote aliyokuja nayo kwa ghafla, ikumbukwe siku zote hakujali kabisa hata kuniuliza hali na alikataa katakata kuwa ameniwekea sumu kwenye chakula.

Nikaamvizia saa 2 usiku nikamtaarifu nataka nikague mizigo yako yote nijiridhishe, wakuu alitoa macho makali ili anitishe nikaanza kutoa kitu kimoja baada kingine nikakuta mfuko mweusi upo kwenye nguo za mtoto una tunguli 13 zimefungwa kwenye vilailoni ndani kuna ungaunga kila rangi.

Nahisi alikuwa mwanga, nikazimwaga sebuleni nikamuita mdogo wangu akashuhudia nikapiga picha, baada ya hapo nikapiga simu kwao kuwajulisha kilichotokea ajabu hawakujali kabisa wakaanza kumtetea nikawaambia wampokee mtoto wao.

Kesho kulivyokucha mapema nikampeleka Ubungo nikampandisha basi nikafuta namba, nikamblock nikamtupa mazima.

Sasa hivi yupo Dar ana mimba ya jamaa mwingine na mtoto wangu ana 5yrs.

Mimi nilienda kutibiwa Tanga.

Wanaume tusikurupukie wanawake kisa umezaa naye, atakuondoa amiliki mjengo akae na ndugu zake au basha wake. Mwache awe single mother tu.
 
Ye ndio ali wrong kwangu

Sent using Jamii Forums mobile app
Inawezekana hakuwrong number mkuu, huwa naogopa Sana mtu akinipa namba yamtu halafu ikawa sio yenyewe kisha niliempigia kwa kuwrong namba anang'ang'ania kunijua na kupigapiga.

Kingine mtu amewrong number halafu anakutafuta tena na tena then unakuta mko mnakaa eneo Moja huwa napata picha huyu hakuwrong namba kuna jambo analitaka ila hakujua aanze vipi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
15 Reactions
Reply
Back
Top Bottom