Nilipata ulemavu sababu ya Mapenzi

Nikupe pole tu ndugu yangu....Nakushauri ujikubali uanze upya hivyo ulivyo... Maisha lazima yasonge mbele...huyo hakuwa wako...alikutumia kwa malengo yake....wako wa shida na raha anakuja kama utakuwa tayari kuyaacha yalopita.

Tunaondokewa na wapendwa wetu wa damu kabisa ..tunazika na maisha yanaendelea sembuse huyo.....usikumbatie tatizo...hata ungefanikiwa kuwa nae ungechapiwa vile vile.
 
Labda sikio la kufa! Kama mwanaume umeamua kuwekeza kwa mwanamke ambaye si mkeo basi fanya hivyo kama msamaria mwema ili mambo yakigeuka mezea na songa mbele.
Pia tujifunze kufanya mambo yaliyo ndani ya uwezo wetu, sio kufurahisha wengine wakati unajiteketeza, tuwe na kiasi. Hao waliopo kwenye ndoa tu changamoto sembuse mpenzi?.
 
Amen na asante ndugu kwa ushauri
 
Asante dada angu kwa ushauri.
 
Pole Sana mkuu

Ila kuhusu suala la deni naamini benk nyingi Zina kipengele cha disability kama security ya kutokuendelea ila lazima iwe permanent na iathiri ufanisi wako wa kazi

Ivo fuatilia mkataba maana uwa hatusomagi
 
Amen na asante ndugu kwa ushauri
Kwa kujazi nakushauri ifanye haya..

1. Kama unatumia pombe ili kuondoa mawazo acha!

2. Tafuta hobby ya kukukip busy! Nashauri anza kushabikia mpira! Tafuta timu ya kushabikia, nakushauri kama huna timu anza kushabikia man united na simba kwa bongo!

Yani ikifika weekend jichanganye kwenye kibanda umiza kama huna tv!

Ukitoka hapo akili itakua imetuliaaaa... rudi geto jipange kwa ajili ya kesho!!

3. Anza kuangalia namna ya kujiajiri. Tumia muda mwingi kuweka akili yako kwenye biashara yako.

4. Kaa mbali na mapenzi kwa sasa.

5. Futa kila kitu kinacho muhusu huyo mwanamke... kuanzia namba mpaka picha.. hii ndio hatua ya kwanza ya kumsahau (actually hii nlitaka kuiweka namba moja...)

6. Anza kuwa karibu na Mungu (Muhimu).

Pole sana na nikutakie kila heri.

Mshana Jr Divine... Heaven Sent et al.,
 
Pole Sana mkuu

Ila kuhusu suala la deni naamini benk nyingi Zina kipengele cha disability kama security ya kutokuendelea ila lazima iwe permanent na iathiri ufanisi wako wa kazi

Ivo fuatilia mkataba maana uwa hatusomagi
@Chapati 2 fwatilia huu ushauri..

Hata mimi nilisha sikia hii kitu na sio ulemavu tu mkopo lazima uwe na bima!!

Kwasababu mleta mada hana kazi na ana ulemavu basi aende benki na uthibitisho wa dokta.

Naiman anaweza samehewa deni.

Narudia tena mleta mada soma upya mkataba wa mkopo wako na uende benki ukawape facts juu ya ulemavu wako.
 
Umeongea kwa hisia sana Kaka,Inaumiza sana,Lakini mtumainie Mungu bro atakushindia katika mengi haya maisha kuna wakati yanatugeuka na kutuumiza lakini tumtazame Mungu analo tumaini letu
Honestly nimeumia sana
 
Ishamtokea mwenzetu so mda wa kumalalamikia, sasa nimda wa kumfariji maana hapo alipo anajuta.
Mpe maneno ya faraja so kumtonesha donda.
 
Hii Testimony yako inahuzunisha sana. Imenisilitisha sana. Kiukweli umepitia mengi sana hadi leo. Nakushauri uangalie NGOs zinazotoa misaada kwa walemavu. Wasiliana nao wakusaidie. Wanatoa hata grants za mitaji nk. Sio kirahisi sana, lakini usikate tamaa ukiambiwa hapana hapa na pale. Mwishowe utafanikiwa.

Kiukweli watu wengi mapenzi yanawaharibia maisha. Kuna hata watu wanajiua sababu ya mapenzi. Naomba kuanzia sasa ugundue kwamba matatizo yanatokea katika maisha ili KUTUIMARISHA. Wazungu wanasema, whatever doesn't kill you, makes you stronger. Tatizo sasa ni kwamba kwa baadhi ya watu.. badala ya janga la maisha kukuimarisha linakudhoofisha.

Hapo ndio kosa ulilolifanya ulivyomkuta mpenzi yuko na best yako. Ujue ulemavu wako wala yeye hajali, na hata ungekufa, asingejali. Hakuna mtu wa kujali maisha yako, malengo yako, na mapambano yako zaidi yako ww binafsi. ULIRUHUSU AKAKUCHANGANYA AKILI, HADI UKASAHAU UNAVUKA BARABARA.

Binafsi, natumia changamoto kama hizo zinakuwa MOTO katika maisha yangu ya kuendelea mbele na kufanikiwa sana, na kuwaangamiza kabisa kimawazo wanaonitakia ubaya. T Woods alisema winning takes care of everything.

Inatakiwa mtu kama huyo anakufanya unakuwa IMARA, hata kama inaumaje.. usiruhusu malengo yake ya kukurudisha nyuma yakatimia. Kumbuka ukitetereka NDIO RAHA YAKE
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…